Je, ualimu ni kwa ajili ya watu maskini?

Tatizo ni marupurupu hasa yale ya upigaji! Utauza chaki? Utapewa rushwa ya nini? Kwa ujumla hakuna pesa nje ya mshahara. Angalia TRA mwisho tu wa siku anatoka na kitita.
 
Kuna mmoja alimuuliza mwanae unataka kuja kuwa nani akamjibu Mwalimu. Du yule Mzazi akasema kumbe gharama zote hizi nazotumia ndoto yako ni mwalimu sinibora uende kayumba tu maana najua hata huko ualimu unaweza kupata tu
 
Uko sahihi kabisa
 
Heri uo ualim kuliko kuishi kwa kuunga unga kwa kukosa kazi kisa umesoma kozi inajina zuri
 
Nimesoma kichwa cha habari tu, na ninakijibu kama ifuatavyo,

Hapana, kuna waalimu matajiri.

Utajiri hauangalii kazi unayofanya, ndio kuna masikini karibu kila fani.
 
Sasa Kwa hizo sababu kwa nini watu waendelee kuipenda hyo kazi SI ya laana hiyo akuna kitu kipo sawa
Wapo wanaofurahia kazi ya ualimu ila kwa wanaofuata maslahi lazima uichukie hio kazi maana hamna utakachokipata zaidi ya kuishi umri mrefu tu sababu ya kula vyakula vya asili na kufanya mazoezi ya baiskeli na kusimama muda mrefu kila siku.

Ualimu pekee hautakupa uwezo wa kula junk foods kama chips mayai na broiler wa kukaanga😁! We ni mwendo wa viazi vya kuchemsha, ugali,tembele, mchicha na dagaa. Karanga kwa mbali pamoja na maji mengi tu.
 
Walimu wenye akili hio ni 0.0005% ya population yote ya walimu.

Walimu wanaotoboa wengi ni wale waliojiongeza, wamiliki wa stationeries za shule kama madaftari na kalamu. Anajiongeza anaweka na picha za passport kisha anahamia kwenye u MC kabisa. Hao ndio waalimu waliotoboa na wana maisha mazuri.
 
Kuna kazi ukizichagua,kwa Gavoo yetu ni Sawa na umechagua umasikini,sijasema ualimu lakini....!
 
Asikudanganye mtu!kazi yeyote inamtoa mtu inategemea nidhamu, Baraka na kutokua na mikosi ya kuuguza hasara n.k!

Kama Kila mkopo unaouchukua unafanya malengo uliojiwekea ni dhahiri utafanikiwa!

Kama wewe ninmtumishi wa imma usipende kuishi kwenye miji mikubwa au kati kati ya majiji coz viwanja au space ya kuendelea ni ndogo sana!

Nenda vijijini au kata zinazoendelea!nunua viwanja,mashamba jenga nyumba za kupangisha,Lima fuga huwezi kufa njaa na utaucheka wakati ujao!!

Lakini ukiendelea kung'ang'ania miji mikubwa viwanja kama Mil 10 na zaidi!utapanga sana,lipa bills kibao,Bado hujasomesha n.k!!
 
Wiki iliyopita nilikua nafanya ishu moja na waalimu, aisee walimu wanapigana sana majungu waume kwa wake. Sijui wana matatizo gani ni kama vile watoto wadogo. Mpwayungu Village atusaidie tatizo ni nini kwa hawa ndugu zake
 
Wiki iliyopita nilikua nafanya ishu moja na waalimu, aisee walimu wanapigana sana majungu waume kwa wake. Sijui wana matatizo gani ni kama vile watoto wadogo. Mpwayungu Village atusaidie tatizo ni nini kwa hawa ndugu zake
Wengi akili zao zinakuwa za kitoto kama wanafunzi wao tu. Wanapigana mashine sana pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…