Uchaguzi 2020 Je, Uchaguzi utakuwa huru na wa haki hata kama vyombo vya habari vitaendelea na katazo la kutangaza habari kampeni za vyama mbadala?

Wewe P toka Wajumbe wamwkufyeka naona hata uwezo wa kufikiri Umepungua Hakuna Uchaguzi huru Tanzania Suala la kuzuia Vyombo vya Habari tu ni Ushaidi Tosha Watanzania sio Wajinga Kama TBC ambayo ni Ya Walipa Kodi Inabagua Vyama unatarajia Nini?
Nimeuliza jee kuna uthibitisho wowote wa CCM kuzuia vyombo vya habari kutangaza habari za vyama vingine?. Tusilete hoja based on hisia!.

P
 
Lipeni vyombo vya habari viwatangaze acheni kutunga uongo ohh vimesusa sio kweli Kama mnataka airtime ya bure Hakuna kitu Kama hicho

Mnagombea uraisi,ubunge na udiwani mpate pesa Sasa kwa Nini mtake bure?
 
Halafu huo ushahidi waupeleke wapi?[emoji88][emoji16]
uwepo uhifadhiwe mahali.. kuna siku utahitajika kumika.

kujiamini sana kwa Lissu usikuchukulie poa. ndiyo maana watawala wamechanganyikiwa hawajui wafanyeje maana kumstopisha hawawezi.

Lissu anajua anachokifanya na anajua exactly the right time ya kukamata masaburi ya mtu!
 
Nimeuliza jee kuna uthibitisho wowote wa CCM kuzuia vyombo vya habari kutangaza habari za vyama vingine?. Tusilete hoja based on hisia!.
P
a good question.

ndiyo maana mimi nimewashauri wapinzani wahakikishe wanazi file communications zote (written, audio, virtual, video, etc) kama ushahidi huko mbeleni.

Lissu is a smart fella - nina uhakika wa 100% kuna mahali na siku ataja kamata saburi la mtu!

Cc
John Mnyika
CHADEMA
 
Kwa tabia za huyu mkulu na CCM tunafurahi kwa tamko lake na tunaomba iwe hivyo lakini wapinzani watakosea sana kumuamini lazima wafuatilie kwa umakini matendo ya serikali na xhama tawala. Mtu alisema ataua vyama vya upinzani ni mtu hatari, tukumbuke 2020 haijakwisha na uchaguzi huu uko ndani ya 2020. Walifanikiwa serikali za mitaa watataka wamalizie na uchaguzi mkuu kuwafuta bungeni na uraisi.
Paskali unanichekesha hapo eti tuna tume huru, rejea Hayati B. Mkapa kwenye kitabu chake. Niambie tume huru ya uchaguzi inayo amini kuwa vyama 5 kwa masaa zaidi ya 5 wameshindwa kurudisha form za wagombea kwenye offisi waliochukulia hizo form kwenye mji mdogo kama Korogwe ni ya kuamini. Cha kuchekesha mgombea wa CCM walikuwa nae lakini yeye kafanikiwa kurudisha fomu.
TBC na Daily News na Habari leo vyombo vya umma-wewe unaviona ni vyombo huru? Labda una definition yako tofauti. Hata hivyo vyombo binafsi vinatakiwa viwaambie watanzania vinasimama upande gani sio kujifanya wako neutral. Tumeona matangazo yakikatishwa kwa sababu kinachotangazwa hakiifurahishi serikali. Huu ni upuuzi uliotukuka.
 
Hauwezi kuwa na uchaguzi huru bila level playing field. Nenda uendako... Huu ni uigizaji wa uchaguzi huru.
 

Kiongozi, tafadhali, declare kwanza interest kwamba wewe ni ccm, halafu mengineyo ndio yafuate...
Viashiria vya kutokuwa na free and fair election, vinanyumbulishwa na control ya media na mambo mengineyo... pongezi kwa JPM kwa kuutangazia ulimwengu kwamba uchaguzi huu utakuwa free na fair, sasa hebu na tuone practicality ya aliyokuwa anasema... labda atawaagiza NEC waufanye kwa style ya CCM na CDM- kura za wazi bila kificho....
 
It does really matter aliyevizuia. Iwe shetani, CCM, dikteta.... matokeo ni yale yale. Uchaguzi tayari siyo huru na wa haki. Kama umewahi kusoma ripoti za waangalia wa uchaguzi utagundua kuwa huwa kuna assessment ya mazingira ya kisiasa kabla ya siku ya kupiga kura. Na hiyo ina include freedom ya media ku-cover habari na sera za vyama vyote. Fairness (ama lack of fairness) imekwishaanza muda huu.
Nimeuliza jee kuna uthibitisho wowote wa CCM kuzuia vyombo vya habari kutangaza habari za vyama vingine?. Tusilete hoja based on hisia!.

P
 
tatizo sio kukataza hao wanalipwa na CCM so kama upinzani unaweza kuwalipa media sioni tatizo
 
tatizo sio kukataza hao wanalipwa na CCM so kama upinzani unaweza kuwalipa media sioni tatizo

..mambo makubwa ya KITAIFA vyombo vya habari vinatakiwa viyatangaze.

..ila kama chama cha siasa kitataka coverage maalum then kitatakiwa kulipia.

..kwa mfano, mikutano yote ya mikubwa ya kampeni inatakiwa itangazwe na vituo vyote kwa usawa.

..baada ya hapo kama kuna chama kinataka kurusha tangazo maalum, au documentary, basi kinaweza kulipia.

..na hata kama wamelipia kurusha hicho kipindi chao, kituo cha habari hakitakiwi kukatisha matangazo ya mikutano mikubwa ya kampeni.
 
Tujiandaeni kuingia road tu watakapopindua kura zetu
 
Wewe acha kujitoa akili
Tume Huru ya Uchaguzi tanzania ipo wapi
Ya huyu mwenyekiti anayechaguliwa na raisi .Bila yeye asinhekuwa hapo anaenda kulipa fadhila tu
Wakurungezi wote ni kada wa CCM
Eti ni wenyeviti wa uchaguzi kila wilaya wamechaguliwa na raisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…