Mkuu Joka Kuu, Uchanguzi Mkuu wa October, utakuwa ni uchaguzi huru na wa haki. Hakikisho hili limetolewa na Amiri Jeshi Mkuu wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli.
Tanzania tuna Tume huru ya uchaguzi na tuna vyombo huru vya habari, ikitokea vyombo vya habari kwa kuutumia uhuru wake, vikaona habari ni ya CCM tuu, then be it huo ndio uhuru wenyewe.
Unless kama una ushahidi wowote hata wa kimazingira tuu, kuthibitisha CCM imevikataza vyombo vya habari kutangaza kampeni za vyama vingine, lakini siamini kama hoja hii ina ukweli.
Tuna vyombo vya habari vya umma na vyombo binafsi. Vinavyotakiwa kutoa haki sawa kwa vyama vyote ni vyombo vya habari vya umma tuu, lakini kwa vyombo binafsi viko huru kufanya upendeleo watakavyo.
Kuelekea Octoba 2015: Je, Sasa ni Wakati wa Media Zetu Kufanya Endorsement ya Wagombea?.
Uchaguzi Mkuu ni Kipindi Cha Neema kwa Media!. Ni Kipindi cha Mavuno!. Jee Bahasha Hizi Ni Halali?!.
P