Je, Uchawi una mchango wowote katika kukuza Biashara?

Hasa usafiri wa poor countries
Kaka mimi nina practice ujasiriamali, ninaweza kuwa vijana wachache wenye CPA lakini nikaamua kuwa mjasiriamali na kujikita kkoo, na sikuwahi kutaka kwenda kwa mganga, niliangaika sana karibu miaka sita napanda, nashuka, maisha hayasogei.
Nilikuja kuanza kuona mafanikio baada ya kukubali kuwa mtakatifu kweli, mimi lazima niwe na maombi asubuhi nusu saa, usiku nusu saa.
Biashara zangu hazigusiki na hili shetani analijua.
Mimi kabla ya kufungua duka, lazima niwe na siku 30 za maombi ya kufunga ndio nianze biashara mpya, bila kufanya hivyo najua hiyo biashara haitasimama.
Kila mwaka mwanzoni kabisa lazima nifunge siku 30 kuikabidhi biashara kwa Mungu. Hapo sijakuambia kwa habari ya sadaka.
Kama hizi sheria huziwezi usije kariakoo, otherwise nenda kwa waganga.
Sasa wewe njoo na maarifa yako bila nguvu ya kiroho kama hujafirisika mpaka Ukose hela ya nauli
 
Usidanganye watu hakuna biashara inayosimama bila zindiko.
 
Hapa utanipa maneno tu lakini uhalisia unaujua mwenyewe.
Mimi nimesimama bila nguvu za giza,
Inawezekana ila sio rahisi.
Kama unataka nikuelimishe nakueleza nimewezaje
 
Hapa utanipa maneno tu lakini uhalisia unaujua mwenyewe.
Wewe una maarifa upande wa pili.
Kwa upande wa Mungu mafanikio yanawezekana kama ukiwa muombaji na mtoaji na utakatifu, inawezekana kabisa.
Bila Baba yangu mzazi(marehemu sasa) alikuwa mchungaji, yeye nilipomwambia nataka niwe mjasiriamali, aliniambia kabisa mwanangu please kaajiriwe, sababu utaashia kuwa mshirikina tu, na itakuwa aibu mtoto wa mchungaji kuwa mshirikina.
Nikamwambia baba sitaenda kwa mganga.
Akaniambia ukitaka kuwa mfanyabiashara inabidi uache huo ulokole wa kusali jumapili, inabidi uwe muombaji wa kila siku.
Nikaanza biashara na ulokole wa kuunga unga kilichonipata, niliuza mpaka gari yangu, kiwanja changu nilivyovipata kwenye ajira, baba yangu akaniambia, nilikuambia mwanangu rudi kwenye ajira, biashara inahitaji uchawi sana au muombaji sana.
Kwa mara ya kwanza nikaanza kufunga na kuomba.
Unajua Nini nilifunga siku 30 ili nirudi kwenye biashara again....
Nilifanikiwa lakini ilinichukua almost 3 years kurudi kwenye ramani.
Leo hii, mimi siwezi kufungua duka bila kupitia Kijitonyama KKKT, kusali misa ya asubuhi. Ijumaa lazima niende kwenye mkesha, yale yale aliyoniambia baba yangu ilinidi nikubali ili biashara iende
 
Mkuu unataka kubiambia nawe Una kinga?
 
hizi ni porojo tu au hadithi za abunuwasi
 
Kwamba if you can't fight against them join them.
 
Mkuu naruhusiwa kuja PM nijikite kwa maombi Zaid .
Wana wa Mungu unitie Moyo ..Usemavyo Ni kweli inabid upige maombi kweli kweli ukilegea kdgo Unafilisika haraka Sana
 
Kuamini uchawi ni ujinga wa kiwango cha lami.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…