IFRS
JF-Expert Member
- Dec 19, 2014
- 2,915
- 5,233
Kaka mimi nina practice ujasiriamali, ninaweza kuwa vijana wachache wenye CPA lakini nikaamua kuwa mjasiriamali na kujikita kkoo, na sikuwahi kutaka kwenda kwa mganga, niliangaika sana karibu miaka sita napanda, nashuka, maisha hayasogei.Hasa usafiri wa poor countries
Nilikuja kuanza kuona mafanikio baada ya kukubali kuwa mtakatifu kweli, mimi lazima niwe na maombi asubuhi nusu saa, usiku nusu saa.
Biashara zangu hazigusiki na hili shetani analijua.
Mimi kabla ya kufungua duka, lazima niwe na siku 30 za maombi ya kufunga ndio nianze biashara mpya, bila kufanya hivyo najua hiyo biashara haitasimama.
Kila mwaka mwanzoni kabisa lazima nifunge siku 30 kuikabidhi biashara kwa Mungu. Hapo sijakuambia kwa habari ya sadaka.
Kama hizi sheria huziwezi usije kariakoo, otherwise nenda kwa waganga.
Sasa wewe njoo na maarifa yako bila nguvu ya kiroho kama hujafirisika mpaka Ukose hela ya nauli