Mkuu kwanza kabisa futa hiyo kauli kuwa wanaume wanalalamika kwa sababu ya kuwahurumia wanawake futa kabisa, HAKUNA mwanaume anayefanya jambo kwenye mahusiano kwa maslahi ya mwanamke narudia HAYUPO acheni kuwadanganya wanawake kwenye hili, ukiona mwanaume analalamikia jambo kwenye mahusiano ujue linamuumiza yeye ila ni vile tu huwa mnatumia kitu kinaitwa self serving reverse psychology trick ili ionekane kama vile mnawasaidia wanawake ili wafanye mnachotaka
Tuanze kwanza na hili kama mngekuwa mnawahurumia wanawake basi mngekuwa mmeshaacha kuwatongoza kwa lengo la kuwachezea lakini kwa bahati mbaya mkiambiwa hivi mnakimbilia kusema, "oo mwanaume hawezi kujizuia mwanamke akitongozwa ndiye anatakiwa akatae sababu yeye ndiye anayeumia zaidi" kitendo cha kutoa hiyo kauli maana yake hamna huruma kwa wanawake, kwa sababu kama ninyi mmeshindwa kujizuia mnategemea mwanamke aweze vipi kwani yeye ameumbwa na kitu gani special cha kumfanya ajizuie na majaribu na vishawishi kwani naye si binadamu
Tukija kwenye suala la ndoa waliosusa ndoa ni wanaume na siyo wanawake maana vinara wa campaign ya kataa ndoa ni wanaume na lengo la wao kufanya hivyo siyo kwamba hawataki ndoa kweli, ila wanataka eti kuwakomoa wanawake ili wajirudi wawe wife materials ndio waolewe sababu wanajua wanawake wako desperate na ndoa hivyo wako tayari kufanya chochote ili waolewe, sasa mimi ndio nawaambia kwamba hao walikuwa ni wanawake wa zamani hawa wa siku hizi ukiwasusia ndoa nao watatafuta njia ya kuwa na furaha bila ndoa they do not care
Kama ni upweke na matatizo ya akili haviwapati wanawake tu tena wanaume wakikosa wanawake ndio wanakuwa wapweke kuliko wanawake wakikosa wanaume na tukiangalia uhalisia wanaume ndio wanaihitaji sana ndoa kuliko wanawake, ila hawataki kuadmit kama nilivyosema wanatumia self serving reverse psychology trick ili kufanya ndoa ionekane ni muhimu kwa wanawake tu, ila ukiuliza huo umuhimu ni upi hasa ambao kwa mwanaume haupo hakuna jibu la maana utapewa lakini tukija kwenye uhalisia kisaikolojia wanaume ndio wanaihitaji sana ndoa kuliko wanawake
Ni kwa sababu wanaume huwa mnaitafuta furaha kwa wanawake na siyo kwa watu wengine au kwenye vitu vingine tofauti na wanawake ambao wao wanaweza kupata furaha toka kwa watu wengine kama watoto na vitu vingine kama pesa, ndio maana kwenye ndoa mke akizingua tu kidogo mwanaume anavurugwa akili na ni ngumu kumvumilia na kusamehe badala yake atatafuta furaha kwa mchepuko ambaye naye pia ni mwanamke, wakati mwanaume akizingua ni rahisi mwanamke kumvumilia na kusamehe na atatafuta furaha kwa watoto wake na watu wengine wa karibu au kazi au biashara yake
Wewe hujawahi kusikia huu msemo kwamba mwanaume kadiri anavyozidi kupata pesa ndivyo anavyozidi kutaka kuwa na wanawake wengi ila mwanamke anavyozidi kupata pesa ndivyo anavyozidi kutaka kujiweka mbali na wanaume, mkuu kwenye mahusiano au ndoa wanaume ndio mnapenda kupetiwa kubembelezwa na kauli kama "pole na uchovu mpenzi" sijui "karibu chakula mume wangu" na huwa mnategemea kuzipata toka kwa wanawake tu, na kuna wanaume seriously kabisa wanachepuka kisa tu hawapati romantic gestures kama hizo toka kwa wake zao wakati wanawake mara nyingi huwa hawajali kuhusu hizo gestures
Sasa unaposema kwamba utazalisha mwanamke halafu utamuacha awe single mother kisha utaoa binti mbichi una uhakika gani huyo binti ndio atakuwa decent na hatakusaliti unataka kuniambia wanaume wote wazee waliooa vibinti wanafurahia ndoa zao kuliko waliooa single mothers, na kama mnajua kuwa wanawake decent wapo sasa mbona malalamiko ni mengi kwamba siku hizi wanawake wameharibika si muwaoe hao hao wanawake mnaowaona decent ujue mkuu ifike mahali wanaume muache kuishi kwenye fantasies mje kwenye reality, mkubaliane na ukweli kwamba wanawake hawatarudi tena enzi za bibi zetu na huko tunakoelekea hali ndio itakuwa mbaya zaidi acheni kujifariji it is either ninyi ndio mkubali kucompromise au muendelee kulalamika hadi mwisho wa dahari