Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Sasa ulikuwaje maarufu church ilihal hujui kujibu ''mwili wa Kristo?''?
Umaarufu Church na kujibu maswali ni tofaut brother, padri mwenyewe kakaa kibabe so nilikua natetemeka, mpaka hv siendagi kula bisibisi tena
 
Umaarufu Church na kujibu maswali ni tofaut brother, padri mwenyewe kakaa kibabe so nilikua natetemeka, mpaka hv siendagi kula bisibisi tena
Duh! mimi hayo mambo zamani saaana, kabla ya kuondoka kanisani.

Ila ukweli ni kamba kuna mapadre watukutu kinoma.
 
Daaah mm kanisan maramoja moja sana coz it is just miyeyusho lkn I BELIEVE IN GOD lkn sio hao mapadre wapigaji
Hilo neno kwenye red nahisi unalitumia purposely ingawa haijawa rahisi kuling'amua.

Mkuu maana na ya 'Miyeyusho' ni nini?
 
Niliwahi kununua barafu kwenye mji mmoja hivi kipindi hicho mgeni ndani ya mji, sikuwahi kujua kama barafu ina ubaridi kiasi kile ,basi mwenzenu nikang'ata nusu nzima nikaweka mdomoni dah ,mbele yangu yupo mgambo wa jiji pembeni kuna pipa la taka yaani nasikia kichwa kizima kimeganda.

Nilimeza kipande cha barafu kizima "sitaki ujinga kuchafua mazingira kwa kutema ovyo mjini"
 
Du mie mpaka nafanya kazi zaidi ya miaka 10 ndio nikatry tena baada ya kuona dharau zinazidi.
Kazi gani yaani ya kupitia elimu au nguvu mkuu? maana hata house girl nae huanza hako kamchezo mara nyingi akianza kazi
 
Nakumbuka primary darasa la 5 huko unyakyusani kwa bibi yangu kyela vijijini. Shule nzima tulikua tunaongea kinyakyusa ikabidi waanzishe kampeni ya kuzuia matumizi ya kinyakyusa shuleni. Walitengeneza ubao ambao mwanafunz ukiongea kinyaki unavalishwa na viboko juu, hali ikawa ngumu sana kwetu tusiojua kiswahili vizuri.

Kuna siku nilipiga chafya ya kinyakyusa darasani (ejooo) hata haikuisha vizuri mtu huyo hapa na ubao wa kunivalisha shingoni, japo nilibisha bila mafanikio.
 
HEBU SIKIA HII
Mwaka juzi 2015 ilikua ijumapili padri akiendesha misa kwenye kigango cha GUNGU kigoma, Basi bwana ikafika ule muda wa kwenda kupokea mkate wa mwili wa yesu {Eukarist takatifu} Sasa wakat wa kupokea padri anasema "mwili ya yesu" unatakiwa ujibu "Amina" basi mm nikajibu "Tunauabudu" akarudia tena nikajibu vilevile, ikabidi anipeleke kwa KATEKISTA pembeni akanielekeza hapo wame baki kama watu watatu kwenye msitar, katekista akanielekeza nikarudi, kuulizwa nikasema tena tunauabudu weeee nilitimuliwa mbio kidogo nile vibao. Padri akanitangaza kanisani, halafu ukichangia nilivyo maarufu kanisan niliaibika sana, mpaka leo naogopa kula ule mkate usio kua na chai wa blueband CHARMILTON
Nimechekaaaa mnoooo aisee
 
siku moja nikiwa china tumeenda shopping nikawakimbia masela , nikaingia kwenye mall moja kubwa sana nikapanda lift huyo hadi maduka ya ghorofani... nimemaliza shopping nikapotea na nisijue pa kutokea na huku nje jamaa wananitafuta kuona hawanipati wakatoa taarifa polisi then wale polisi wakawataarifu wenzao waliomo ndani ya ile mall kuwa wakiona black man wam'escort to the exit. Kimbembe kimekuja hapa sasa, askari alivoniona akawa anakuja na mm nikaanza kumkimbia aisee tulitimuana mle ndani sitakaa nisahau. Mpaka nimechoka jamaa akanipeleka kwa masela huku nimepata aibu ya karne
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mimi nakumbuka nipo chuo Iringa wakati wa group presentations si unajua tena ushapiga jumba lako jeusi ili uongezee marks walau, sasa shughul ikawa tunataka kupanda group zima stejini lecturer akasema no need apande tuu mmoja...straight akanipoint mimi na hata kazi nlikua siijui inafananaje 🙂
Macho yalinitoka na lisuti lako kijasho kwa mbali..basi ile hofu kupanda stejin nikaikosa ngazi nlibiringita hadi chiniiii..kuficha aibu wallah sikuinuka nkajifanya kuzimia!!!
...that was my embarrassing moment ever
Daah aisee, ukaamua uzimie[emoji23] [emoji23]
 
Hahahahahahaha...noma sana
 
Back
Top Bottom