Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

kuna binti aliagiza mabia bar kwa kunikomoa .sasa mfukoni nikawa na buku ten tu bill ikaletwa kama 35 elfu.enzi hizo ni ela mingi. nikavizia kaenda toilet nichukue handbag yake nichomoe ela tushare pamoja bill.akanifuma naingiza mkono kwenye mkoba.nilipata aibu ya mwaka.nafwaaa
[emoji23] [emoji23] [emoji23] kaah
unatupwagaa
 
siku moja nikiwa china tumeenda shopping nikawakimbia masela , nikaingia kwenye mall moja kubwa sana nikapanda lift huyo hadi maduka ya ghorofani... nimemaliza shopping nikapotea na nisijue pa kutokea na huku nje jamaa wananitafuta kuona hawanipati wakatoa taarifa polisi then wale polisi wakawataarifu wenzao waliomo ndani ya ile mall kuwa wakiona black man wam'escort to the exit. Kimbembe kimekuja hapa sasa, askari alivoniona akawa anakuja na mm nikaanza kumkimbia aisee tulitimuana mle ndani sitakaa nisahau. Mpaka nimechoka jamaa akanipeleka kwa masela huku nimepata aibu ya karne
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mimi nakumbuka nipo chuo Iringa wakati wa group presentations si unajua tena ushapiga jumba lako jeusi ili uongezee marks walau, sasa shughul ikawa tunataka kupanda group zima stejini lecturer akasema no need apande tuu mmoja...straight akanipoint mimi na hata kazi nlikua siijui inafananaje 🙂
Macho yalinitoka na lisuti lako kijasho kwa mbali..basi ile hofu kupanda stejin nikaikosa ngazi nlibiringita hadi chiniiii..kuficha aibu wallah sikuinuka nkajifanya kuzimia!!!
...that was my embarrassing moment ever

Nakumbuka primary darasa la 5 huko unyakyusani kwa bibi yangu kyela vijijini. Shule nzima tulikua tunaongea kinyakyusa ikabidi waanzishe kampeni ya kuzuia matumizi ya kinyakyusa shuleni. Walitengeneza ubao ambao mwanafunz ukiongea kinyaki unavalishwa na viboko juu, hali ikawa ngumu sana kwetu tusiojua kiswahili vizuri.

Kuna siku nilipiga chafya ya kinyakyusa darasani (ejooo) hata haikuisha vizuri mtu huyo hapa na ubao wa kunivalisha shingoni, japo nilibisha bila mafanikio.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]. Pole sana mkuu
 
  • Thanks
Reactions: lcm
Nakumbuka nikiwa darasa la 4 kipindi cha mwisho kabla ya mapumziko ya saa nne nimebanwa na mkojo hatari, kwenda kuomba ruhusa lazima useme kwa kingereza maana ilkua kipindi chake,
Uvumilivu ukanishinda nkatoka kwenda kwa mwalimu kuomba ruhusa, sasa lugha inanipiga chenga nkasema kwa kiswahili akanichapa fimbo mguuni akitaka niseme kingereza nikajikuta nimeumwaga palepale kiasi, nkatoka nduki sikurudi tena darasani nikaenda kujificha vichakani hadi kaptula ikauke maana ilkua ya kaki huko njiani wangeniona,
Na nilikua na demu darasani ambae ni binamu yangu, asubuhi nampitia tuende shule akanicheka huku akisema hanipi tena nkamtandika vibao akasema kwa shangazi yake sababu ya kumpiga nikajiongezea tena aibu kwa wajomba wakajua nilijikojolea shuleni.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Niliwahi kwenda na rafiki yangu kwa ndugu zake ilikuwa Area c Dodoma sasa kumbe rafiki yangu alikuwa amebanwa tukapiga hodi tukakaribishwa wenyeji tukawakuta sebuleni.Rafiki yangu alisalimia na haraka haraka akaendelelea na safari ya kwenda chooni mie nami nikachanganya supu namfuata mwenyeji akauliza na wewe unakwenda wapi? mwenzio anaenda chooni! nilipata aibu ya mwaka nikakoma kufuatafuata watu.
Hilo neno la kuchanganya supu umenifurahisha sana mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: lcm
Nakumbuka primary darasa la 5 huko unyakyusani kwa bibi yangu kyela vijijini. Shule nzima tulikua tunaongea kinyakyusa ikabidi waanzishe kampeni ya kuzuia matumizi ya kinyakyusa shuleni. Walitengeneza ubao ambao mwanafunz ukiongea kinyaki unavalishwa na viboko juu, hali ikawa ngumu sana kwetu tusiojua kiswahili vizuri.

Kuna siku nilipiga chafya ya kinyakyusa darasani (ejooo) hata haikuisha vizuri mtu huyo hapa na ubao wa kunivalisha shingoni, japo nilibisha bila mafanikio.
Mkuu nimecheka mpaka mtoto ameamka.
 
kui pita mtaa huu 🙂🙂

Back
Top Bottom