Kipindi niko o level nlikuwa mtukutu sana,alafu ilikuwa boarding zile za sheria kali,basi waliletwa samaki skonga wamejaa katenki kadogo kale saizi ya mwisho kwaajili ya waalimu na wenye shule walikuwa na kongamano,basi wahuni wakaiona fursa,wakantafuta msuka mipango,tukaona haiwezekani waalimu wale vinono ilhali sie wanafunzi ni mwendo wa nguna na wali arage deile kama wafungwa.Tulivyokuwa vichwa ngumu badala ya kuchukua kidogo tukajaza samaki ndoo kubwa ile nzima tena misamaki ya haja,kimbembe kikawa kwenye logistics sasa,long story short tulikuja kukamatwa red handed tukiwa tunawaoka wale samaki,hapo tushakunywa sana michemsho ya samaki,alafu alie tukamata ndo mwenye shule sasa,mnoko kama nini,outcome ilikuwa eitha tukatangazwe mstarini mbele ya mademu au tule sanspaa,au adhabu zote kwa pamoja.nlimpiga jamaa saundi sijawahi kumpiga mtu tokea nijue kuongea,mpaka jamaa akatusamehe.