Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Another day, ilikuwa siku ya kwanza kukwea pipa from Dsm to Doha-Qatar na Qatar Airways... Nimekaa zangu mda nikabanwa na haja (big call) nikafikiria nimuite mhudumu anioneshe toilet zilipo?? nikaona utakuwa ushamba wa kiwango cha lami... nikainuka huyo to the cockpit... nikakuta kimlango kiko labeled 'occupied' nikageuka nyuma nikakuta 'unocupied' mzee nikazama. Sababu nilikuwa nimebanwa mda mrefu fasta nika unload mzigo.. kimbembe sasa [emoji23][emoji23] kucheki sioni sehem ya kuflahia, no kikamba cha kuvuta no button bas mzee nikabaki nimeduwaa tuu.. kuchek pembeni kunasehem imewekwa kilabel cha duara ile kugusa tuu kitu hicho [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nikavuta pumzi (kumbe mi mjanja)... Sasa imebaki kazi moja 'kujiswafi' na nikicheki hamna 'horse' ya maji ya kutawadhia [emoji33][emoji33] asee nilifungua kale kamlango nikabaki namwangalia tuu yule hostess sielewi nianzie wapi.. nikajifungia nikaloesha tissue paper nikamaliza kazi ile natoka yule mdada anacheka tuu kwakweli kile kinjia kuja kuikuta seat niliona kama kilometa hivi..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Likizo ya mwezi wa sita form three mzee alinipa kazi ya kulipia mambo yake TRA, kama mnavyokumbuka mwanzoni mwa 2000's kulipia TRA ilikuwa na milolongo mingi sana mtu ukiwa bize unaweza ukazira. Kwa hiyo mzee alinipa ya usumbufu pamoja na rushwa.
Basi nilipomaliza kila kitu nikawa nimebaki na chenji ya kutosha kabisa. Siku hiyo nimetoka TRA narudi hom, njiani nimekutana na classmate nammezeaga mate sana nikasema leo nina nyenzo nang'oa huyu mtoto.
Tukasalimiana nikamkaribisha kwenye hoteli jirani hapo tule lunch wala hakuvunga. Msosi ukaletwa chips kuku nusu mara mbili bonge la advataizi, niksona hapa ndo wakati wa kuchomekea kama JPM. Ile sijamaliza hata mistari yangu mtoto akasimama kwa hasira akaanza kunifokea kwa sauti kali sana. Hapo meza zote zimejaa wafanyakazi wamekuja lunch wote wamegeuka wanashangaa hawa watoto vipi! Mimi hata cha kujibu sina mate yamekauka. Nakumbuka maneno machache tu "yani vichipsi vyako ndo unitongoze?" mengine sikusikia kwa kweli. Akaondoka zake mimi sielewi cha kufanya, akaja dada mmoja mhudumu na mfuko akaniambia lipia mdogo wangu tukufungie.
Sikutongoza tena hadi form five na huyo huyo akawa girlfriend wangu wa kwanza.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Eti vichipsi vyako ndio unitongoze!!
 
Mimi sitosahau kipindi nabarehe, ilikuwa darasa la saba kitambo sana enzi hizo nikiwa na miaka 16 nilimtongoza mtoto wa kiarabu hapo class maana walikuwa wengi sana class, akanikataa kisha akawaambia wenzake ikawa kila nikimsogelea ananikimbia huku wenzake wakinicheka. Nilitoroka shule sikurudi hadi jtatu maana ilikuwa ijumaa, na home nilishindwa kula chakula kwa jinsi kibuti kilivyoniingia
 
Nakumbuka Nikiwa Darasa la tatu asubuhi nikiwa Primary school shule moja Kyela huko vijijini Basi tukawa tumechelewa kuhesabu namba. Ile mwalimu anaanza kupiga walochelewa nikalala haraka chini akapiga fimbo kama tatu nikatoa kituko ambacho niliona ni ujanja........ Itaendelea [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Bila shaka ilikua bujonde huko
 
Nakumbuka primary darasa la 5 huko unyakyusani kwa bibi yangu kyela vijijini. Shule nzima tulikua tunaongea kinyakyusa ikabidi waanzishe kampeni ya kuzuia matumizi ya kinyakyusa shuleni. Walitengeneza ubao ambao mwanafunz ukiongea kinyaki unavalishwa na viboko juu, hali ikawa ngumu sana kwetu tusiojua kiswahili vizuri.

Kuna siku nilipiga chafya ya kinyakyusa darasani (ejooo) hata haikuisha vizuri mtu huyo hapa na ubao wa kunivalisha shingoni, japo nilibisha bila mafanikio.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] etata etata ukonywile mbavu zangu....ishawahi kunikuta hyo ngamanga moja duuh mi nilibisha hadi issue ikaenda kwa mwalimu
 
Another day, ilikuwa siku ya kwanza kukwea pipa from Dsm to Doha-Qatar na Qatar Airways... Nimekaa zangu mda nikabanwa na haja (big call) nikafikiria nimuite mhudumu anioneshe toilet zilipo?? nikaona utakuwa ushamba wa kiwango cha lami... nikainuka huyo to the cockpit... nikakuta kimlango kiko labeled 'occupied' nikageuka nyuma nikakuta 'unocupied' mzee nikazama. Sababu nilikuwa nimebanwa mda mrefu fasta nika unload mzigo.. kimbembe sasa [emoji23][emoji23] kucheki sioni sehem ya kuflahia, no kikamba cha kuvuta no button bas mzee nikabaki nimeduwaa tuu.. kuchek pembeni kunasehem imewekwa kilabel cha duara ile kugusa tuu kitu hicho [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nikavuta pumzi (kumbe mi mjanja)... Sasa imebaki kazi moja 'kujiswafi' na nikicheki hamna 'horse' ya maji ya kutawadhia [emoji33][emoji33] asee nilifungua kale kamlango nikabaki namwangalia tuu yule hostess sielewi nianzie wapi.. nikajifungia nikaloesha tissue paper nikamaliza kazi ile natoka yule mdada anacheka tuu kwakweli kile kinjia kuja kuikuta seat niliona kama kilometa hivi..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Unatakiwa uwe na chupa tupu ya maji kwenye begi unaenda nayo,wenzetu wanachambia karatasi badala ya maji
 
Back
Top Bottom