Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Je, ulishawahi kuaibika katika mazingira mabaya?

Kati ya thread zooote nilizowahi kusoma hapa jamii forums, this is the best!!! [emoji1544][emoji1544][emoji1544][emoji1544][emoji1544][emoji1544][emoji1544][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122] kwa mleta uzi!!
Wewe labda mgeni humu
 
Another day, ilikuwa siku ya kwanza kukwea pipa from Dsm to Doha-Qatar na Qatar Airways... Nimekaa zangu mda nikabanwa na haja (big call) nikafikiria nimuite mhudumu anioneshe toilet zilipo?? nikaona utakuwa ushamba wa kiwango cha lami... nikainuka huyo to the cockpit... nikakuta kimlango kiko labeled 'occupied' nikageuka nyuma nikakuta 'unocupied' mzee nikazama. Sababu nilikuwa nimebanwa mda mrefu fasta nika unload mzigo.. kimbembe sasa [emoji23][emoji23] kucheki sioni sehem ya kuflahia, no kikamba cha kuvuta no button bas mzee nikabaki nimeduwaa tuu.. kuchek pembeni kunasehem imewekwa kilabel cha duara ile kugusa tuu kitu hicho [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nikavuta pumzi (kumbe mi mjanja)... Sasa imebaki kazi moja 'kujiswafi' na nikicheki hamna 'horse' ya maji ya kutawadhia [emoji33][emoji33] asee nilifungua kale kamlango nikabaki namwangalia tuu yule hostess sielewi nianzie wapi.. nikajifungia nikaloesha tissue paper nikamaliza kazi ile natoka yule mdada anacheka tuu kwakweli kile kinjia kuja kuikuta seat niliona kama kilometa hivi..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji1] [emoji1] mtakuja kujikuta mnafungua milango ya emergency door sikunyingine
 
Nakumbuka iyo siku nimetoka kukoga na futa geto limeisha ikabidi nivae suruali fasta nifate mafuta duka lilipo jirani na nipoishi,nikavaa na kuchomoka haraka nilipofika dukan nikakosa mafuta niliyokuwa nahitaj nikazingunga kama maduka3 hivi yalipo mbali kidg nikapata duka moja wapo sasa ile narud tu home ile nataka fungua kifungo cha suruali kujicheki maeneo ya zipu kupo wazi na jimuwa linaonekana kabisa live bila chenga,nikakumbuka kuna baadhi ya maduka niliyopita kuna kinadada walikuwa wakiangua vicheko pacpo mimi kujua nn kiliwafurasha.....OGOPA SANA KUSAHAU KUFUNGA KUFULI.
Ah ah ah ah jmn nimevuta picha nikapasuka kucheka pole aisee
 
Haha ikabidi tu utoe hela mwee. Umenikumbusha story ya kimini

Kuna siku nilikuwa darasa la 5 au 6 hivi, nikawa napita mitaa ya sokoni. Nimevaa kakimini kangu ka kuchanua, najishaua tu. Basi bana kuna kichaa fulani hivi, akaninyatia kwa nyuma huyoo akanifunua mwaaaaaa, jamani nashukuru nilivaa teitei. Miguu ilistuck jamani, I felt so embarrassed khaa
Khaa, jamani,mweee ah ah ah pole dearest na ww min ulikuwa unapenda za kuchanua.
 
Hahahah na tuskirt twangu twa kuzungusha, sijui nilikuwa naficha wembamba. Alikuwa yule kichaa Mwanaisha, niliaibika khaa
Aah kwan mwanaisha alikuwa na tabia ya kufukuza watu?
Na sijui kafa cz sijamsikia au kwavile hatupo huko ndio maana.
Pole mwaego. Nipo nasoma comment za watu nacheka uhiii watu ns vimbwenga vyao
 
Chuo presentation mbele ya lecture wangu Dk Clement Mashamba (kabla ya kuteuliwa kua Wakili Wa Serekali)... Picha linaanza suruali imechanika makalioni halafu sina taarifa, mwenzangu tupo nae kwenye stage tunataka kupresent akaiona, kosa alivonishtua, material zote kichwani zilipotea kwa mshtuko, sikujua nianzie wapi na nimalizie wapi, hapo kijasho, presha, mwili kutetemeka e.t.c.................. Kilichofata naomba nisimalizie, maana nikikumbuka roho bado inanishtuka sana!!!!
 
Aah kwan mwanaisha alikuwa na tabia ya kufukuza watu?
Na sijui kafa cz sijamsikia au kwavile hatupo huko ndio maana.
Pole mwaego. Nipo nasoma comment za watu nacheka uhiii watu ns vimbwenga vyao
Sijasikia hata kama yupo au laah. Huu Uzi ni utacheka hadi basi, ukimaliza huu nishtue nikupe link nyingine uchekeeeee
 
Hahahaa , afadhari wewe Mimi nilishawahi kujinyea darasan halafu nilikua nakaa bench moja na mtoto wa kike, nakumbuka ilikua ni standard 3

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii usiombe, pindi nipo darasa la kwanza, half time tumepewa uji na mwalimu, tukaugonga darasa zima, mimi ukanikata tumbo kweli, ila baada ya kumaliza mwalimu akatupa ruhusa ya kwenda kujisaidia kama kawaida yake, kufika chooni watoto wamejaa kila kona, mi tumbo lika beep ya kwanza, nikipiga jicho bado kuna nyomi halafu hawaondoki, wala hawapungui, lika beep mara ya pili, jasho likaanza kunishuka huku machozi yakinilenga

Miscall ya tatu sikuisikia, nakuja kutahayari nimesha chafua miguu yote mpaka kwenye viatu

Mwalimu ikabidi aniogeshe, nguo na viatu havifai, ikabidi anivalishe kanga lubega (kama shuka za kimasai wanavofunga) peku peku mpaka home, mdogo mdogo huku wanafunzi wakiniimbia "kajinyea eh eh kajinyea eh eh kajinyea".... Nililia kilio sio cha nchi hii, hatari[emoji31]
 
Mimi nakumbuka nipo chuo Iringa wakati wa group presentations si unajua tena ushapiga jumba lako jeusi ili uongezee marks walau, sasa shughul ikawa tunataka kupanda group zima stejini lecturer akasema no need apande tuu mmoja...straight akanipoint mimi na hata kazi nlikua siijui inafananaje 🙂
Macho yalinitoka na lisuti lako kijasho kwa mbali..basi ile hofu kupanda stejin nikaikosa ngazi nlibiringita hadi chiniiii..kuficha aibu wallah sikuinuka nkajifanya kuzimia!!!
...that was my embarrassing moment ever
Hahahahaha....
 
Hii usiombe, pindi nipo darasa la kwanza, half time tumepewa uji na mwalimu, tukaugonga darasa zima, mimi ukanikata tumbo kweli, ila baada ya kumaliza mwalimu akatupa ruhusa ya kwenda kujisaidia kama kawaida yake, kufika chooni watoto wamejaa kila kona, mi tumbo lika beep ya kwanza, nikipiga jicho bado kuna nyomi halafu hawaondoki, wala hawapungui, lika beep mara ya pili, jasho likaanza kunishuka huku machozi yakinilenga

Miscall ya tatu sikuisikia, nakuja kutahayari nimesha chafua miguu yote mpaka kwenye viatu

Mwalimu ikabidi aniogeshe, nguo na viatu havifai, ikabidi anivalishe kanga lubega (kama shuka za kimasai wanavofunga) peku peku mpaka home, mdogo mdogo huku wanafunzi wakiniimbia "kajinyea eh eh kajinyea eh eh kajinyea".... Nililia kilio sio cha nchi hii, hatari[emoji31]
Ah ah ah ah ah pole aisee
 
Back
Top Bottom