Je, ulishawahi kulazimisha mpenzi au rafiki aendelee kubaki maishani mwako?

Hahahaha wewe mbona ni kama mimi tu yaani mimi sijawahi hisi napendwa na mtu japo kuna watu baki huwa wanasema eti wananipenda ila si unajua moyo wa mtu kichaka

Hauwezi jua kama mtu kamaanisha au la hivyo hata mie mtu baki akiniambia eti ananipenda au amenimiss huwa namuitikia tu lakini moyoni nashituka na najiuliza anipende au animiss kwa kipi hasa nilichomfanyia au kwa sababu gani labda

Japo mie ninaweza nikampenda mtu from nowhere sababu ya kitu kidogo tu hata kama simjui vizuri na mimi nikimpenda mtu huwa sina tabia ya kutaka eti naye arudishe ule upendo kama nilionao mimi kwake yaani sinaga expectations hizo

Unasubiri nini kwenda JWTZ ndugu yangu mimi huko kunaniita na maisha kama hayo nahisi ndiyo maisha niliyoyachagua na ndiyo niliyopangiwa kuwa nayo hadi nakufa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa work mates ni kawaida hilo...
Sehemu yoyote yenye kipato hawata penda ona ukiwazidi na wivu upo juu yao.

Fanya work mates ni wafanyakazi wenzio tu na si wakufanya urafiki real, katika kazi na kipato na ukuwaji wa kiuchumi hakuna rafiki wa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sijui ila Nadhani maybe sijapenda au nimeukomaza moyo wangu kwa mitazamo ya kua mpweke pweke.
Mfano..
Hua najisemea I'm useless one, nobody needs me! So kwa mentally hii hata mpenzi akiniacha najua tu I'm no tdestined to he loved.
mmmh mkuu.
 
Mbona waguna
maneno yako yamenifanya nitafakari hii mentality anayo mdogo wangu natumia nguvu kiukweli to make her feel normal and valued, maana kwake naona imezidi sana hua ni rahisi kukata tamaa, kujitenga, na mwisho huweza kujidhuru pengine I always pray for her natamani anizidi vitu vingi nilivyonavyo katika maisha kwa upande wangu nahisi si nzuri kujiona useless.
 
Mmelelewa na mtu mmoja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…