Je, uliwahi kukutana na changamoto gani katika kutafuta ajira

Je, uliwahi kukutana na changamoto gani katika kutafuta ajira

Mimi nilikutana na matangazo haya ya ajira kwenye nguzo za umeme bhn mshahara 410k. Nikapiga simu, wakaniambia niende kwenye interview kesho yake pale Chang'ombe Junction saa 12 asubuhi na niwe smart sana, wakaniasa.

Kesho yake, kama kawaida, nikaenda kutimba pale Chang'ombe. Nikampigia jamaa, akanipa maelekezo hadi nikafika pale. Mmmh, nikaanza kupata wasiwasi tu kwa muonekano wa ofisi ile. Kuangalia kushoto, naona watu wamejipanga mstarini—yaani ni kama parade hivi! Daah!

Nikakaza moyo, nikaulizia alipo huyo jamaa maana aliniambia nikimuulizia tu nitaelekezwa alipo. Basi, kufika kule, jamaa akaniambia nitafanya interview kwa njia tatu tofauti: Oral (maswali ya mdomo), darasani kwa maandishi, na kwa vitendo. Nikajibu, "Sawa, hamna shida kiongozi."

Oral tukaanza. Mara wakaitwa wengine watano na mimi, tukawa sita. Anauliza swali, unanyoosha mkono ukiwa unajua jibu, anayejibu anapewa maksi.

Swali la kwanza likawa: "Unatakiwa kufika kazini saa ngapi?"

Nikajiuliza, "Mtu ndo nimekuja, wananiuliza muda wa kuja kazini kweli?" Kusikia sauti, "Saa 2! Saa 2!" Nikageuka, kuna mdada nilimuona ananinong’oneza kimoyomoyo. Nikasema, "Kama anajua, si anyooshe mkono ajibu jamaa?" Ila hakuna aliyejaribu kufanya hivyo kati ya wale ili tusionekane wote viazi.

Mimi nikanyoosha mkono, nikajibu, "Saa 2, kiongozi." Akasema, "Safi safi!" Wale wenzangu wakaanza...

Itaendelea: 2
Wewe jamaa story yako ni kama yangu nilikimbia 😂😂😂😂
 
Inaendelea part 2,
Wale wenzangu wakaanza Kunipigia makofi na hakuna aliyewaambia wafanye hvo nikawa nazidi kuvurugwa juu ya wale watu je n wenyew wanataka kaz au ni akina nan bs mkuu akauliza swali la pili. Ni nini majukumu/wajibu wa mfanyakazi kama kawaida nikasikia mtu ananongoneza 'kuwahi kazini' kuwa nadhifu' na 'Kuheshimu viongozi' lakini hakuna hata aliyenyoosha kidole nikasema OK ngoja nijibu nikajibu kama nilivyosikia kiongozi akasema safi sana wewe kwenye oral ushapita subiri nje hapo bs nikatoka nje wale wengne wakabaki kama dkk kadhaa tukaitwa tukapewa peni na rim paper 1,Maswali yameandikwa kwenye kaubao hv kuyasoma ndio yaleyale mawili niliyojibu ndani OMG nikasema ni nini hiki jaman nikajibu vizuri nikakusanya na kusubir pale nje wakati nasubiri akatoka yule interviewer wa oral akaniuliza dogo ushakunywa chai nikajibu bado bro Basi kama kuna sehemu nilikosea ni hapo jamaa akasema twende nikamfuata akaninunulia supu ya 2500 na chapati 2 nikapiga nilipomaliza kidogo tukaitwa tena tukaambiwa hongereni wote mpo vizuri kila mtu tutamkabidhi kwa senior ambae ndie atafanya nae interview kwa vitendo
Inaendelea.....
Ila unanichekesha na kunikumbusha mbali😂😂
 
Inaendelea part :3.......
Mimi nikapewa senior wangu kidada flani kibonge kinaongea harakaharaka kakaniambia twende huku ndo tukaenda huko sijui ndo warehouse tukakuta mavyombo haya ya kila aina mabeseni, majagi, mavikombe, masahani na mengine mengine yule dada akaongea na yule store keeper pale,Mara akatoa mabeseni mawili makubwa yana mavyombo vyombo mengine ndani yake kile kidada kikasema beba hilo wallah nilikua siamini nikabeba akasema leo kuna wateja tutawasambazia huu mzigo ko usiwe na wasiwasi utakuwa na mimi nitakuelekeza kila kitu Kimoyo moyo nikasema no no!Lakini ile supu niliyokunywa ikawa inanihukumu moyoni nikasema OK let me do it today kesho sitakanyaga hapa abadani bs tukatoka na yale mabeseni hadi barabarani akasema tunaanzia buguruni sa mm kimahesabu naona buguruni mbali isitoshe tuna mizigo veta pale hd buguruni mhh!
Nikamwambia si tupande daladala sister kama shida nauli mm nitalipa wueh yule dada akanigeukia akaniambia io ela itakusaidia baadae we twende nifuate bs nikatii nikamfuata ile barabara yote hd junction tukakunja hv tukaanza kufuata nyerere road hd Mtava kumbuka hapo nina beseni.
Alafu nimevaa official kinouma yaani official official kweli yaani maombi yangu yalikuwa watu wa kwenye daladala zinapita pale asitokee hta mmoja ananijua maana dhaaa bs tukaenda hd Mtava pale kuna chocho unakatiza hd buguruni hpa kati kuna mitaa mitaa bs yule kijeba akaanza..
Itaendelea...
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Inaendelea..5
Baada ya kula nikashangaa ananyooshea kidole njia ya kuelekea ilala boma nikamuuliza vipi akanijibu kwani we umemaliza mzigo wako ebu Acha utoto nikamtukana sana ila kimoyomoyo ila ustaarabu ukaniongoza basi tukaanza kufuata ile njia mpaka marapa bungoni tukapita hd mbele kuna mtaa unaitwa Arusha, huo mtaa una waarabu kibao inaonekana ni mtaa wake pendwa maana kila tulipogonga walikuwa wanafahamiana nae kuna house moja tuligonga ikatoka Mali hiyo asikwambie mtu akasema dada mambo leo umekuja na mkaka mpya kapendeza jmn ! hapo mm natamani kusema kitu but gubu liko moyoni kucheka nataka kulia nataka! Confidence nakosa kbsa nikaishia kuuchubua tu of course tuliuza uza pale ilala na mimi sasa ule mbeseni wangu ukanunuliwa ko nikamuomba jeba vile vyombo vyangu vichache vyenye vimebaki niweke kwake na nikahisi kuanzia hapo nitakuwa free from loads daah jeba likakunja Eti ooh ukiweka hvo basi unabeba nikasema famililah! ,wacha nivishike tu ilikuwa ni chupa ya chai , glass za kunywea maji zile zimebebanishwa na vikunio vya karoti na nyanya hivyo basi ndugu yangu jeba likasemaje eti twende hadi junction ya karume then tukunje had ofisini kwa mguu lahaula walakuata illabillah! nikajisemea sakwe leo ninalo Kusema kweli hapo mm nilikuwa tyr miguu iko hoi to the maximum nikagoma nikamwambia hapana tupande daladala hapo boma shule lkn jeba akawa hataki nikamwambia sikia kama hutaki shika vyombo vyako mm naondoka akasema we unampa nan kakabidhi ofisin upewe na posho nikamjibu Sina shida na posho yenu mimi sitaki chochote jeba akawa mpole akasema basi punguza hasira twende tukapande daladala wakati tunaenda kuna mwanangu mmoja nilisoma nae advance mlandizi pale mm nilimuona anasogea pande nilipokuwa sema yeye hakuniona nilishukuru maana angenichalazia sana😅yule mwamba kwenye group letu la WhatsApp,Ndo kupanda daladala hadi veta tukafika ofisini tukaenda kukabidhi vile vitu vikabaki store kule tukaambiwa tumsubiri cashier nae yuko site huko ndo aje kutupa posho kukaa hadi saa moja kasoro cashier ndo anarudi yuko hoi kiatu kimoja mkononi kimekatika daah akatupa buku 2 Kila mmoja pale sikuamini yaani nimengoja for more than 1 en half hour iyo buku 2 daah nilikuwa hoi sana ile buku2 nikapanda boda hadi ngozi pale then nikapanda daladala hadi Gongolamboto ndo nilikuwa nikiishi huko enzi hizo hallo! ni siku sitaisahau yaani Nikiona haya matangazo kwenye nguzo huwa yananikumbusha hii story na nikiona mtu anauza vyombo yuko smart kavaa mpaka tai reminds me of this story 😄 sitasahau sitasahau sitasahau ukiwa Huna ajira maisha huwa weird mnoo 🙌🙌END
Wenu katika ujenzi wa taifa
SAKWE..
~Mwisho~
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Kuna madogo wengine nilikuta wamepewa peni wauze.

Wale wa viti ndio karibu daily nakutana nao, wamebeba viti kibao.

Wengine ndio ninyi wa mavyombo vyombo.
Hizi biashara za kuzunguka mitaani zina faida ila biashara iwe yako usiwafanyie hao wanyonyaji.
 
Hahaaaa!!!

Nilipataga mchongo wa kazi ya udereva kwa wahindi, nilivyoitwa kwenye interview nikajua labda itakua kawaida tu.

Nipo nje nasubiri, akatoka mkurugenzi mwenyewe(muhindi) na mafaili yake, akanipa funguo za gari akaniambia washa gari twende shoppers plaza.

Nimechukua funguo naangaza ni gari gani maana kulikua na gari kama 8 zimepaki, akanioneshea kimaruti(vile viko kama mkate) kipyaaaa na makaratasi yake.

Mie kufika kwenye gari nikaanza na mikwara eti nakagua maji, naangalia kama kuna upepo, hapo kanji ananichora tu, nikapanda nikawasha jino moja tu chuma ikawaka.

Kimbembe kila nikitia rivasi, nikiachia clutch kinazima, yaani mpaka kurudi nyuma kukiweka sawa kimeshazima mara nne 🤣 😂 (hapo bado kwenda mbele.)

Muhindi akapanda, kuondoka kikazima kama mara mbili, tayari nikawa nishapanic, tumeenda njiani nikakuta foleni kmmmmmk hii ilikua ni siku ya kufa nyani , yaani ulikua ni mwendo wa kuzima na kuwasha, mpaka tunafika shoppers kimeshazima zaidi ya mara kumi 😄 🤣 😂 😆.

Aliposhuka tu, nikaanza mazoezi pale pale parking za shoppers wakati namsubiri mshua, naenda mbele, narudi nyuma(tatizo kilikua kipyaaaa clutch yake inanyanyukia juu, ukiachia kidogo tu kinaruka)

Mshua alivyorudi tukaanza safari ya kurudi ofisini kinondoni, ni mwendo wa kuzima na kuwasha mpaka tunafika.

Tulipofika mkurugenzi akashuka bila kuniambia kitu huyooo akaingia ofisini,(nikajua tu hapa tayari nimeshapoteza dili) baada ya dk kama 10 hivi secretary akaniita akaniambia nenda nyumbani tutakupigia simu(hapo ki moyo moyo najua nimeshakosa kazi)

Baada ya kama siku nne nashangaa simu yangu inaita minamba ina 222222 ya ttcl nikaona hawa jamaa vipi? Kama interview nimeshafeli, hiiiì nashangaa wananiambia kesho niende kazini kuanza kazi. asee nilishangaa sana, sijui yule muhindi aliona nini kwangu.

Baadae nikawa ndio dereva wake, madereva kibao niliwakuta ila nikawa dereva wa mkurugenzi, ikawa sio kuendesha mkate tena ni mwendo wa v8.
Nimecheka kwa hiyo ukawa unafanya tizi pale shoppers la kwenda mbele na kurudi nyuma wakati unamsubiri bosi!
 
Nikajiuliza, "Mtu ndo nimekuja, wananiuliza muda wa kuja kazini kweli?" Kusikia sauti, "Saa 2! Saa 2!" Nikageuka, kuna mdada nilimuona ananinong’oneza kimoyomoyo. Nikasema, "Kama anajua, si anyooshe mkono ajibu jamaa?" Ila hakuna aliyejaribu kufanya hivyo kati ya wale ili tusionekane wote viazi.

Mimi nikanyoosha mkono, nikajibu, "Saa 2, kiongozi." Akasema, "Safi safi!" Wale wenzangu wakaanza...
Nilikutana na👇
1739402860090.png
 
Inaendelea..5
Baada ya kula nikashangaa ananyooshea kidole njia ya kuelekea ilala boma nikamuuliza vipi akanijibu kwani we umemaliza mzigo wako ebu Acha utoto nikamtukana sana ila kimoyomoyo ila ustaarabu ukaniongoza basi tukaanza kufuata ile njia mpaka marapa bungoni tukapita hd mbele kuna mtaa unaitwa Arusha, huo mtaa una waarabu kibao inaonekana ni mtaa wake pendwa maana kila tulipogonga walikuwa wanafahamiana nae kuna house moja tuligonga ikatoka Mali hiyo asikwambie mtu akasema dada mambo leo umekuja na mkaka mpya kapendeza jmn ! hapo mm natamani kusema kitu but gubu liko moyoni kucheka nataka kulia nataka! Confidence nakosa kbsa nikaishia kuuchubua tu of course tuliuza uza pale ilala na mimi sasa ule mbeseni wangu ukanunuliwa ko nikamuomba jeba vile vyombo vyangu vichache vyenye vimebaki niweke kwake na nikahisi kuanzia hapo nitakuwa free from loads daah jeba likakunja Eti ooh ukiweka hvo basi unabeba nikasema famililah! ,wacha nivishike tu ilikuwa ni chupa ya chai , glass za kunywea maji zile zimebebanishwa na vikunio vya karoti na nyanya hivyo basi ndugu yangu jeba likasemaje eti twende hadi junction ya karume then tukunje had ofisini kwa mguu lahaula walakuata illabillah! nikajisemea sakwe leo ninalo Kusema kweli hapo mm nilikuwa tyr miguu iko hoi to the maximum nikagoma nikamwambia hapana tupande daladala hapo boma shule lkn jeba akawa hataki nikamwambia sikia kama hutaki shika vyombo vyako mm naondoka akasema we unampa nan kakabidhi ofisin upewe na posho nikamjibu Sina shida na posho yenu mimi sitaki chochote jeba akawa mpole akasema basi punguza hasira twende tukapande daladala wakati tunaenda kuna mwanangu mmoja nilisoma nae advance mlandizi pale mm nilimuona anasogea pande nilipokuwa sema yeye hakuniona nilishukuru maana angenichalazia sana😅yule mwamba kwenye group letu la WhatsApp,Ndo kupanda daladala hadi veta tukafika ofisini tukaenda kukabidhi vile vitu vikabaki store kule tukaambiwa tumsubiri cashier nae yuko site huko ndo aje kutupa posho kukaa hadi saa moja kasoro cashier ndo anarudi yuko hoi kiatu kimoja mkononi kimekatika daah akatupa buku 2 Kila mmoja pale sikuamini yaani nimengoja for more than 1 en half hour iyo buku 2 daah nilikuwa hoi sana ile buku2 nikapanda boda hadi ngozi pale then nikapanda daladala hadi Gongolamboto ndo nilikuwa nikiishi huko enzi hizo hallo! ni siku sitaisahau yaani Nikiona haya matangazo kwenye nguzo huwa yananikumbusha hii story na nikiona mtu anauza vyombo yuko smart kavaa mpaka tai reminds me of this story 😄 sitasahau sitasahau sitasahau ukiwa Huna ajira maisha huwa weird mnoo 🙌🙌END
Wenu katika ujenzi wa taifa
SAKWE..
~Mwisho~
nmecheka hadi machozi yametoka 🙌🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom