Je, uliwahi kuwa maarufu shuleni?

Je, uliwahi kuwa maarufu shuleni?

Umaarufu shuleni niliupata kwa kichukua dem pini shule nzima.
 
ndio maana jf ina great thinkers, nenda facebook unao wataka uta wapata

Great thinkers wote JF walikua wanakua wa kwanza darasani?

Hii ni Self Grandiose which is a narcissistic disease ,you need therapy!

Ulikua wa kwanza amongst who?

Kua wa kwanza among wajinga nayo ndio u-great thinker wewe Mr Great Thinker?
 
Kabisa, yaani unakuwa unaona kama dunia ni yenu tu. Halafu home kwao na kwetu tulikuwa tunajulikana, akipewa kitu anapewa na changu, mimi pia naambiwa mpelekee na fulani.
Inafurahisha sana mkuu. Mimi nilikuwa na demu o level. Nyumbani kwao walikuwa wananifahamu. Mida ya jioni naenda kwaotunapiga story na wazazi wake, wanapika tunakula.l ikifika mida ya saa nne anasindikiza nyumbani. Siku ya mahafali kidato cha nne mama yake alinitafuta sana nipige naye picha. Ila naomba Mungu anisamehe kwa kilichotokea baada ya hapo.
 
Secondary; ni vingi tu vilivyofanya nijulikane shule nzima hata shule jirani lakini kubwa ilikuwa mwandiko mzuri shule nzima....ilifikia hatua watoto wa kishua wananiletea barua za kwenda kwa maboyfriend wao niwachongee mwandiko( ila kwa sasa navyoandika bata ana nafuu)

Kingine ni muonekano ukibebwa na guu kweli, shule ilikuwa ni day ...muda wa kutoka shule baadhi ya watu waume kwa wake walikuwa wakitoka nje kuniona tu ( ule uzuri uliisha baada ya mahudhurio ya leba)

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa
 
Awali-Bosi mpole (Sababu nilipewa 1000 nikalisha darasa zima huku nikishangaa hela haiishi.

Msingi kimbembe nilijulikana mzee wa bomu: Hiyo darasa la saba mwalimu mnaa wa hesabu alirushiwa baruti ya mkono(imetengenezwa na choki ya pikipiki. Jioni hiyo akiwa kwenye veranda anaelekea darasani ngoma ilirushwa ukutani!, Ticha chali na mbio kali uzuri tulipewa adhabu ya bakora na kudeki veranda.

O-level mpole sana na mkimya hiyo nature yangu hadi leo huku issue za warembo sio sana.

A-level nikijulikana kama Mjerumani: Hiyo ilikuwa baada ya kutoroka event flani ya shule na ni muhimu sana, Sasa kulikuwa na wajerumani walikuwa na crash program kama patinazi, Sasa huyo mtasha alikuwa zamu event yenyewe ilikuwa ni kusoma wa kwanza hadi wa mwisho haijalishi ni Hkl,Pcm etc wote mnaunganishwa sasa wa science tulikuwa wa mwisho mwisho, nikashangaa huyo dom nikagoma kwenda kwenye hiyo event kulichotokea basi tu sikufukuzwa shule.

University: Mr Projector Amekuja lecturer mshamba mshamba hajuui set projector na pindi inabidi lisonge projector imewashwa ni blurish akatokea mtani wangu kaaangaika pale na projector akashindwa: Huku audience ikishangaa Nikaamka nikaenda zungusha kitu flani issue hiyo tokea siku hiyo ni Mr projector na kozi ilikuwa inachukua zaidi ya degree prog nne.Project
 
O level nilikua bingwa wa Debate kudadadeki mpaka jamaa wakasemaga natumia ndumba maana sio kwa kukariri mabombastic vile ..... halafu form four watu wakategemea zawadi ya English nachkua nikawasurprize nikachkua ya physics...toka hapo wakawa wananiona nimeshindikana
 
Dah, kweli hakuna anayependa kusifika kwa mabaya. Kweli kwa posts zote hizi hakukuwa na vilaza kabisa wa mwisho?
 
Primary...Nilijulikana kwa kuijua ipasavyo hesabu
Sekondary...Nilijulikana kwa kuijua hesabu na kuandika assay ndefu na kuongeza booklet zakutosha
Advance, Nilijulikana kwa ukipanga wa physics
Chuo ,,,Nilijulikana kwa kubadilisha mabinti na kukosa vipindi vingi mno na hapo ndo umarufu wa kijinga uliponipeleka kusiko
 
Back
Top Bottom