Hiyo post haitoi hoja kuwa hakuna Mungu bali umetaka uthibitishiwe kama kuna uumbwaji yaani umetoka kwenye swali la je kuna Mungu na sasa upo kwenye swali la je tumeumbwa?
Sasa mimi nataka hoja za kwanini wewe useme hakuna Mungu? Swali bado lipo palepale.have onether try
Onyesha wapi Mungu kasema Kaumba watu wakamilifu?
Mwenyezi Mungu katuumba tukiwa na mapungufu mkamilifu ni yeye tu. Kwahiyo hiyo point yako mbona ndio inathibitisha uwepo wa Mungu maana Mungu kasema yeye ndiye mkamilifu na kweli ukiangalia sisi tuna mapungufu kama ulivyosema hivyo Mungu kasema kweli.
Umetoa mifano ya watoto kufa, meli kuzama n.k wewe nani alikuambia kuwa watoto wadogo kufa , meli kuzama, mafuriko kuua watu kuwa ni mambo mabaya? Unaweza kuthibitisha kuwa mtoto mdogo kufa ni jambo baya??
Nisome vizuri hapa
Umetoa maelezo ambayo wewe umedai ndio sababu ya kusema Mungu yupo.
Maelezo hayo uliyaelezea kwa mfano wa mtu na simu, ukisema simu imetengenezwa viwandani basi na mtu aliyetengeneza hiyo simu lazima awe ameumbwa.
Ambapo ukaenda kuhitimisha kuwa huyo mtu ameumbwa na Mungu.
Then ukaniambia nikupe sababu kwanini mimi nasema hakuna Mungu.
Majibu yangu yalikuwa ni haya.
Kwasababu neno "kutengeneza" imekuwa ni neno linalowakilisha kitendo ambacho kimekuwa kikifanyika katika shughuli zetu basi hatuwezi kuona utata wa hilo neno.
Hivyo tutaenda kwenye maswali mengine
1. Kwanini tunasema simu inatengenezwa?
2. Je simu inahitajika kutumika kama reference kuthibitisha uwepo wa mtu au mtu mwenyewe tunaweza kuthibitisha uwepo wake bila kutumia uwepo wa kitu kingine kama reference?
3. Tunaweza kuthibitisha simu imetengenezwa?
4. Je tunaweza kuthibitisha mtengenezaji wa simu yupo?
5. Je tunasema hivyo kwasababu tumeikuta tu simu hatujui imefikaje fikaje hapo ilipo?
6. Au tunasema simu imetengenezwa kwasababu tuna uthibitisho ambao upo na unaweza kuwa observed?
7. Je simu kuwa na chanzo maana yake na mtengenezaji naye lazima awe na chanzo?
8. Je kila chenye complex ni lazima kiwe na chanzo?
9. Haiwezekani kilichopo kikawepo bila chanzo?
10. Kama inawezekana kwanini tujisumbue kutafuta vyanzo wakati tushajua kuwa chanzo sio necessary kwenye kufanya kitu kiwepo?
****************
Bila shaka tunasema simu imetengenezwa kwasababu kwanza kuna elimu juu ya utengenezaji simu, mtu yeyote anaweza kujifunza na kuna viwanda vipo vinatengeneza simu.
So mpaka hapo tushajua kuwa haiwezekani simu ikawepo tu bila kuwa na chanzo kwasababu tumejua nini kinafanyika mpaka simu inakuwepo.
∆∆∆∆∆∆∆∆∆∆∆∆∆
Hoja kuhusu Mungu
Sasa unaposema mtu aliumbwa na Mungu unatakiwa ujiulize maswali yale yale tuliyojiuliza wakati tunatafiti kujua simu imefikaje fikaje.
1. Kuumbwa ni nini?
Kuna uthibitisho wowote uliowahi kuwa recorded kuonesha uumbaji upo?
2. Na huyo Mungu anayefanya uumbaji tunaweza kuthibitisha uwepo wake?
3. Au hatuwezi kuthibitisha uwepo wake na hivyo tupo katika hatua za kutumia uwepo wa mtu ili usimame kama uthibitisho wa kuonesha Mungu yupo?
4. Kama haiwezekani kuthibitisha Mungu yupo bila kutumia rejea ya vitu vingine ambavyo vipo na vinathibitishika, huoni hiyo itamaanisha mwanzo wa hivyo vitu ndio mwanzo wa Mungu?
5. Tukikubaliana kuwa Mungu yupo (japo bila uthibitisho) je tukitaka kujua chanzo cha huyo Mungu amewezaje kuwepo, itawezekana?
6. Kama itawezekana basi hicho chanzo chake kitajwe lakini bado unafikiria huyo Mungu atabaki kuwa Mkuu wakati yupo aliyemfanya awepo?
7. Kama haitawezekana Mungu kuwa na chanzo basi hakukuwa na sababu ya wewe kuhoji chanzo cha mtu wakati unafahamu ni rahisi kitu kuwepo bila chanzo.