Je, umewahi kubadili mtazamo juu ya kitu fulani ambapo hapo awali uliuamini sana? Kwanini?

Je, umewahi kubadili mtazamo juu ya kitu fulani ambapo hapo awali uliuamini sana? Kwanini?

Katika maisha kila mtu ana amini katika kile anachokiamini kuanzia kwenye maisha binafsi, dini, uchumi, siasa n.k.

Kuna watu wanaamini biashara bila ndumba haiendi, kuna wanao amini mapenzi bila pesa lazima mwanamke Aku cheat n.k.

Mimi kwa upande wangu nilikuwa naamini kutumia miti shamba kujitibu ni ujinga tena nikihusisha na ushirikina lakini kwa sasa hapana siamini hivyo nimejua kuwa miti na mimea kwa ujumla ina siri nyingi na ni tiba sana.

Vipi wewe kwa upande wako Ulishawahi kubadili mawazo yako na kuacha kuamini kitu ambacho ulikiamini awali ? na Kwanini?
Dini aisee mi saiz pagan kabisa
 
Aya gani kwenye Qur an inasema muhammad alioa mtoto wa miaka sita? 🤣Ehe tuelimishane mjuzi
Soma hadiths ..na usijifanye kusema hadiths sio za ukweli coz hata Quran haielezei jinsi ya kuswali lakini waislamu Wana swali...so usiongee kujikosha
 
Hakuna sehemu nimemtaja Mungu be humble 😁 , maswali yangu yoote nimeuliza kwa sababu nina kiu ya kutaka kufahamu.

Anyways unaweza kunitajia any new evolution phenomenom discovered ukiacha ambazo tayari zinajulikana??
Fatilia bacterial evolution au virus..coz ni wadogo inaweza ikawa observed, wanaita mutation coz ipo chap lakini it plays the same part..
 
Alafu hawa watu wanaojifanya wanajua haya mambo ya mungu ni wanafki kishenzi , hakuna watu wenye roho chafu kama hawa , juzi kati kuna nabii uchwara nilimnasa kibao kwa kulazimishia story zake za abunuasi mbele yangu.🤪
🤣Wataishia kukuambia hujui jua limetoka wapi...so Mungu wangu katengeneza
 
Mimi binafsi nilikuwa naamini mungu yupo ila nikaja kugundua ni hadithi tu za alinacha za kutunga zisizo na ukweli wowote.

Biblia ni kitabu kilichotungwa na watu. Quran kama inavyoeleza yenyewe iliandikwa na watu ambao hawakufika hata darasa la pili, thinking yao ni kama ya watoto wa chekechea.

Mungu hayupo, ni hadithi tu zisizo na kichwa wala miguu.
Na mimi pia ni kama wewe.
 
🤣 Haya maswali ni ya kijinga Sana mpaka tushayazoea.. ushaona upepo sijui akili...🤣bro huwezi ona ubongo wako labda CT scan huko..Ila kuuona hivi huwezi ila tukipasua kichwa tukautoa ubongo na wewe haupo...sijui unanielewa..tunajua ubongo upo coz tumeuona kwa wanyama mbalimbali ikiwemo binadamu
Akili na ubongo ni tofauti
 
Umewahi kuiona akili yako?
Akili ni dhana ya kufikirika HAIPO.

Binadamu tuna vichwa vyenye ubongo.

Neno Akili ni la kufikirika, halipo katika uhalisia.

Ni sawa na kusema umewahi kuona Hasira, wasiwasi au hofu.

Vitu hivi vyote havipo katika uhalisia bali katika dhana ya kufikirika.
 
Mungu hatoi mali, kwa vile Hayupo

Watu hupambana kutafuta mali.

Mifano yako hii haina mantiki yeyote kuonesha uwepo wa huyo Mungu.
Kuna watu wanapambana kutafuta na hawazipati hao nao vipi? Ukizingatia wametumia kanuni sawa na wengine ambao wanazipata
 
Mungu hatoi mali, kwa vile Hayupo

Watu hupambana kutafuta mali.

Mifano yako hii haina mantiki yeyote kuonesha uwepo wa huyo Mungu.
The same hoja yako pia haionyeshi Mungu hayupo kwani ili Mungu awepo ni lazima atoe mali kwa watu wote?
Haya chukulia ndio katoa kwakuwa umeamua kupinga uwepo wake bado ungesema hizo mali watu wote wametafuta kwa juhudi zao.
Hapa ni vizuri kuelewa kuwa jitihada hazizidi kudra, Mungu ndio mmiliki wa hali zote, zote kwa maana ya zote na yeye ndio aliyesema tokeni mkatafute riziki hapa ndio watu huchanganya mambo wengi hudhani kuwa rizki ni mali tu, Kumbe rizki ni mjumuisho wa mambo mengi kama elimu,Afya,mali, n.k
Ndio maana utakuta mtu ana elimu lakini hana mali mungine ana mali lakini hana afya, Sasa usichukulie Mungu anagawa mali tu uka hitimisha kwa kuwa watu wengine hawana mali basi hayupo my friend logic ya wapi hiyo ? Mungu kuwa muweza wa yote na mwenye upendo wote sio sasa ndio watu wasife, ndio watu wawe na mali wote n.k, Yeye anabaki kuwa muweza wa yote tu hata kama wewe hauna mali, hata kama mtoto wako kafa kwenye ajali n.k
Alafu maswali yote hayo Mungu mwenyewe kashayajibu kwenye vitabu vya dini kuwa Yeye ndie Mola wa ulimwengu, Ametuumba wanadamu ili tuishi katika hii dunia na akatupa akili ili tuitumie kudhibiti matamanio yetu hivyo tumuamini yeye na kumuabudu, baada ya hayo ndio kuna maisha ya umilele na furaha kwa waliotumia akili zao vyema kumuabudu Mungu na hapo ndio hayo maswali yako yanapojibika kwa urahisi kuwa.. Baada ya kukuumba na kukuweka duniani kisha ukafa sasa unaenda kuishi tena katika umilele huko hakuna hizo ajali unazolalamikia huku duniani, Huko kuna mali unazoziangaikia huku duniani.
 
Akili ni dhana ya kufikirika HAIPO.

Binadamu tuna vichwa vyenye ubongo.

Neno Akili ni la kufikirika, halipo katika uhalisia.

Ni sawa na kusema umewahi kuona Hasira, wasiwasi au hofu.

Vitu hivi vyote havipo katika uhalisia bali katika dhana ya kufikirika.
Nadhani utakuwa umeshamjibu yule aliye uliza kuhusu Mungu hayupo kwa sababu haonekani.
Milango yetu ya fahamu ina limit macho hayawezi kuona kila kitu, masikio hayawezi sikia kila kitu n.k vipi sasa kutaka kuyalazimisha macho mpaka yamuone Mungu ndio useme yupo??
Hasira, Woga, Akili ni vitu vipo iwe kwa dhana ya kufikirika kama unavyodai lakini vipo na hatujawahi kuviona why sasa tuseme vipo? Mngeitimisha tu havipo Kama mnavyoitimisha kuwa Mungu hayupo.
 
Soma hadiths ..na usijifanye kusema hadiths sio za ukweli coz hata Quran haielezei jinsi ya kuswali lakini waislamu Wana swali...so usiongee kujikosha
Lakini wewe ndio uliyesema aya sio Mimi anyway..Hadith gani iyooo embu tuwekee hapa tujifunze na sisi.
 
Back
Top Bottom