Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa JF katika maisha ya uhalisia (Jamii)?

Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa JF katika maisha ya uhalisia (Jamii)?

1.2019 nipo kwenye Coaster natoka Arusha kwenda Moshi...Nilikaa ile siti karibu na mlangoni...nipo JF kuna Uzi mmoja ulikuwa hot sana na Dada mzuri Heaven Sent kuna ushauri alikuwa anautoa kwenye hiyo mada..nikawa nafuatilia kwa makini sana wakati huo sikuwa active sana hapa jukwaani...kufika Machame road kuna Abiria akashuka Mkaka( si haba)[emoji2]wakati anashuka akaniambia kumbe wewe ndiyo Makiseo( ID yangu ya mwanzo).

2. Kibaruani kwangu...Kuna mmojawapo alinibamba...Kipindi App ikiwa ipo poa...Ila hakuona ID...Akaniambia kumbe Familia[emoji1]
Hiyo ya 1 huyo mkaka noma kwa uchunguzi.
 
Kuna mada moja ililetwaga humu miaka kama 4 au 5 iliyopita
Kipindi hiko humu Jf kila mwanamke anajiita pisi
Jamaa akaomba mchezo na pisi moja pm, akakubaliwa, kumbe bwana ulikuwa mchongo.
Yule dada kafika lodge kumbe jamaa kategesha camera chumbani.
Yule dada hatakuja kusahau ile aibu halafu wote tulikuwa tunamuona bonge la demu na mkali balaa hapa jukwaani, kumbe hakuna kitu na ni aibu sana.
Pia kosa kubwa alilofanya yule dada ni kuchati kupitia Pm mpaka sura yake.
Jamaa aliscreenshot kisha akaja na uzi wenye naked video ya yule dada pamoja na picha zake.
Jamaa alikula life ban na ile Id ya yule dada last seen yake imesimama July 2019 mpaka leo.

Kwahiyo hizi ndizo sababu za wengi kukataa kufahamika
Huu umbea ni wa mwaka gani? Siamini kama ulinipita.

And kwanini walimfanyia hivyo? Yarabi !
 
Hivi kumbe jf ni mtandao wa Siri sana
Habari za muda huu wanajamvi!

Je, umewahi kukutana na mtumiaji wa Jamii Forums katika maisha ya uhalisia (Jamii)?
🔹 Ulijisikiaje?
🔹 Ulijitambulisha kuwa na wewe ni mwanachama, au ulifanya kama hauijui kabisa?
🔹Baada ya kujitambulisha mlikuwa na mazungumzo ya aina gani?

Nimeuliza hivi kwa maana watumiaji wengi wa JF hutumia huu mtandao kwa Siri sana

Share nasi uzoefu wako! 📢👇
Naamini kila mtu ana hadithi ya kipekee ya kusimulia.

#JamiiForums #Jamii #Uhalisia #UzoefuWako
 
Back
Top Bottom