Je, umewahi kutamani kifo chako kiwe cha namna gani?

Je, umewahi kutamani kifo chako kiwe cha namna gani?

Kuna kifo na kufa..
Siogopi kifo naogopa kufa..
Hatuzungumzii issue za kuogopa kifo ipo wazi kila mtu anaogopa

Lakini kuogopa haisaidii hata

Kinachozungumziwa hapa je kama ungekua na chaguo unatamani ufe kifo cha namna gani?

Au unaogopa kusema unahisi utakufa kesho kama ukisema 🤣🤣🤣
 
Hatuzungumzii issue za kuogopa kifo ipo wazi kila mtu anaogopa

Lakini kuogopa haisaidii hata

Kinachozungumziwa hapa je kama ungekua na chaguo unatama ufe kifo cha namna gani?

Au unaogopa kusema unahisi utakufa kesho kama ukisema 🤣🤣🤣
Painless..
 
Kutamani kifo chako kiwe cha namna gani ni jambo lisilo na maana sana hasa kwa nchi zetu masikini za Africa zilizojaa ajali na matibabu duni.
Kutamani ni kama ndoto na sio kila ndoto inatimia mkuu

Lakini kutamani sio makosa wala zambi
 
Argentina wanafika fainali, na watakutana na "The Trio"....
Mbappe+Olise+Dembele... 😊
Ndio safari yao itakapoishia hapo.
Acha basi usiseme hivyo

But kwa Mpira wa leo sidhani kama Fainal watafika

Magori ya leo kama miujiza
 
We babu wa makamo hulali tu😊

Mbona hata sioni kama nimawazo ya makubwa jamani

Ulevi wangu mie ni boli, boli linaendelea mimi nalala vipi!!!
Kuhusu mada; Haya mawazo yako mapana sana; inaonyesha unawaza sana. 😊
 
Binadamu tuna ndoto, malengo na matamanio mengi kuhusu maisha Tunapanga kuwa na nyumba nzuri, gari, ardhi, biashara na mafanikio mengine mengi


Lakini umewahi kujiuliza kuhusu mwisho wa safari yako?

Umewahi kutamani kifo chako kiwe cha aina fulani?


Mara nyingi husikia watu wakisema,

Yule amekufa kifo kibaya
inasikitisha sana🥲

Hapo unajiuliza, kama kuna kifo kibaya, je, kuna kifo kizuri?


Labda kile kisichoambatana na maumivu makali, mateso ya muda mrefu au taabu nyingi

Je, hicho ndicho kifo kizuri?


Pia, kwa nini kuzungumzia kifo huonekana kama uchuro?


Kuna mtu aliwahi kujinunulia jeneza lake mapema na akaonekana kama ana matatizo ya afya ya akili au kama anajichulia

Lakini ukitafakari, hata usipolinunua mapema bado ukweli ni kwamba siku moja utakufa tu

Kwa nini jamii hulichukulia jambo hilo tofauti?


Cha kushangaza ni kwamba watu wengi husema

Nataka nioe /kuolewa nipate watoto na nyumba kalii gari kaliii
Biashara zaidi yaani uwekezaji wa kila namna (na hii sio mbaya ni sawa kabisa kua na future)

Lakini ni nadra sana kusikia mtu akisema anatamani kifo chake kiwe cha namna fulani

Maana ukweli ni kwamba baada ya yote hayo mwisho ni kifo!

Lakini sasa ikitokea mtu akasema anatamani kifo chake kiwe cha namna fulani watu humuona kama hayuko timamu

Na akisema hivyo, wengi huanza kuona kama hayuko sawa kiakili

Sijui kwa nini huwa hivyo🤔


Binafsi, sitamani kufa sasa😅

Natamani niishi miaka mingi zaidi kwa sababu sijui chochote kuhusu maisha baada ya kifo

Sehemu ninayoijua ni hii dunia, na ningependa niendelee kuwepo kwa muda mrefu zaidi

Lakini pia najua ipo siku moja nitaondokana wewe pia utaondoka📌

Ila sasa kwa upande wangu siku hiyo ikifika

Natamani au ningependa 👇

Nife kwa amani🤗

Nisiwe na chuki wala kinyongo na mtu yeyote

Sitamani kuugua magonjwa ya muda mrefu yanayomchosha mgonjwa mwenyewe na kuwachosha wanaomlea& wanaomuuguza


Pia sitamani kifo cha ajali au kifo chenye maumivu makali sana

Kama ni kuugua, basi iwe kwa muda mfupi

Hii huwapa nafuu hata wanaobaki, kwani hawabebeshwi mzigo mkubwa wa muda, nguvu na gharama za kukuuguza


Kama ningekuwa na choice, ningependa siku yangu ifike nikiwa nimelala kwa utulivu, kisha niondoke kimya kimya bila kelele, bila taharuki na bila mateso makubwa


Je, wewe umewahi kuwaza kuhusu kifo chako? Kama ungepewa nafasi ya kuchagua, ungependa kifo chako kiwe cha namna gani?


Team
Messi 🔥🔥🔥🔥

ShesRise_1 🤚
Kwa mada hii tu kisaikolojia nishajua wewe ni dume ila umejipa ID ya kike na hapa jamiiforums unatambulika kama mwanamke maalumu mkali "...." Ila Kwa Elimu yangu wewe ni mwanaume wanawake ni nadra sana kuwaza kifo tena Cha future na kukiandika Kwa mapana yake katika predictions. Superbug Boston's
 
Acha basi usiseme hivyo

But kwa Mpira wa leo sidhani kama Fainal watafika

Magori ya leo kama miujiza

Wanakutana na timu mbovu; hapa watakutana na Uswisi/Colombia. Watatoboa na Uingereza watampasua, fainali wanakutana na Ufaransa. 😊
 
Ulevi wangu mie ni boli, boli linaendelea mimi nalala vipi!!!
Kuhusu mada; Haya mawazo yako mapana sana; inaonyesha unawaza sana. 😊
Tena Yuko 45+ ndio wanaowaza kufa kwahiyo kama ni demu ni mbibi ila my psychology tells me he is a man with oldies.
 
Kwa mada hii tu kisaikolojia nishajua wewe ni dume ila umejipa ID ya kike na hapa jamiiforums unatambulika kama mwanamke maalumu mkali "...."
Mkuu nimechekaaa 🤣🤣🤣🙌
halafu leo tokea morning nakutana na comment au vitu vya kunifurahisha 🤗
Ila Kwa Elimu yangu wewe ni mwanaume wanawake ni nadra sana kuwaza kifo tena Cha future na kukiandika Kwa mapana yake katika predictions. Superbug Boston's
Nikuambie au 😜
 
Back
Top Bottom