Je, Unajua hapo kabla wananchi waliibia sana Serikali, kwa sasa Serikali inawaibia wananchi kwa kushirikiana na taasisi na mashirika ya fedha?

Je, Unajua hapo kabla wananchi waliibia sana Serikali, kwa sasa Serikali inawaibia wananchi kwa kushirikiana na taasisi na mashirika ya fedha?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kwa miaka kadhaa iliyopita watumishi wengi wa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali, waliibia sana serikali.

Hii ilitokana na kukosa udhibiti wa miaya ya rushwa, kukosa uadilifu na kuruhusu matumizi yasiyo ya lazima.

Kiongozi wa nchi aliyetangulia kabla ya huyu aliyepo sasa, alijitahidi kuziba na kudhibiti miaya ya rushwa na kuyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kulipa gawio kwa serikali.

Hata hivyo kwa sasa hali ni tofauti na huwezi kuamini kirahisi. Serikali kwa kushirikiana na taasisi na mashirika ya fedha kama vike bank, mitandao ya simu, michezo ya kubahatisha, wamekuwa wakiwaibia wananchi kwa njia mbalimbali.

Mojawapo ni kukata tozo au kodi zaidi ya mara moja. Mfano kwa mtumishi wa umma anayepokea mshahara wake benk, anakatwa tozo ya kutoa ilihali mshahara huo umeshakatwa kodi. Hii si sawa.

Fedha inatumwa na ndg au jamaa kwa mtandao wa simu, fedha hiyohiyo inakatwa tozo wakati wa kuweka na kutoa. Huu ni wizi!

Kwenye michezo ya kubahatisha huko ndio balaa kabisa. Mshindi anayetakiwa ni mmoja, wanacheza watu mamilioni na wanakatwa fedha na tozo ya serikali,( mfano ukicheza tsh 1000 unakatwa sh 110).

Na wengi wanaocheza ni wale wa hali za chini wakiwa na matumaini ya kupata zaidi. Huu nao ni wizi!

Unaweka fedha kwenye simu kwa ajili ya muda wa maongezi kabla hata hujatumia, unakatwa kiasi fulani, kama sio wizi ni nini?

Je, inamaana mianya ya wizi huko serikalini imekosekana? Au waliokuwa wanaibiwa wameshtuka? Kwanini wameamua kuwaibia wananchi?
 
Kipindi ya Magufuri nimekula sana Rushwa, utaniambia nini
 
Ilifanyika katika kila nchi, na sio jambo jipya. Hakuna haja ya kushangaa. Ukweli wake.
 
Beberu kaweka mifumo dunia nzima ili serikali ziwe na uthibiti zaidi, nafikiri tutaelewana mbele ya safari....
 
Mimi mshahara wangu ukiingia bank ushakatwa kodi, nikienda kuutoa nakatwa tena kodi.

Kali zaidi, mshahara huo huo nikiutoa CRDB kuupeleka AMANA bado nakatwa tena kwa kuweka bank hiyo.

HAITOSHI; mshahara huo huo nikija kuutoa AMANA nakatwa tena kodi IT'S NOT FAIR.
 
Back
Top Bottom