Je, unajua kuwa Roho huwa ina kawaida ya kutoka tulalapo?


roho huwa haitoki unapolala kinachotoka ni nafsi. nafsi ndio hutoka na kuzinguka. roho hutolewa na mtoa roho siku yako ya mwisho malaika mtoa roho
 
Mmh hiyo ya kufika sehemu na kuhisi siyo mara ya kwanza naona kila mtu anasema lake wengine husema inahusiana na reincarnation
 
roho huwa haitoki unapolala kinachotoka ni nafsi. nafsi ndio hutoka na kuzinguka. roho hutolewa na mtoa roho siku yako ya mwisho malaika mtoa roho
Kwa mujibu wa Qur'an kila tunapo lala roho huenda Kwa Mwenyezi Mungu na huyo ndo mwenye roho zake.

Kwa Sisi Waislamu kwakuwa ni Kitabu chetu tunaamini hivyo
 
Na kuna Ile unaweza kulala chali ukafake ubongo wako ujue kama umelala halafu unaanza hisi ganzi miguuni inapanda kuja mdogo mdogo nasikia ukikomaa Bila kuogopa unajikuta unatoka ndani ya mwili
Hiyo astral projection
 
Neville Gorddad
 
Yeah ila hiyo huwa ni voluntary process na si kila mtu hufanikiwa kuifanya
Yeah nilijaribu one time nikafeel ganzi inapanda toka miguuni inapanda kuja juu dah nikaogopa nikaona isiwe tabu nikajitingisha na kusitisha zoezi Ila nitajaribu tena
 
Yeah nilijaribu one time nikafeel ganzi inapanda toka miguuni inapanda kuja juu dah nikaogopa nikaona isiwe tabu nikajitingisha na kusitisha zoezi Ila nitajaribu tena
Haha ila mkuu si inasemekana kufanya hivyo ni dhambi
 
Lipo wazi, roho inaweza ikapiga trip nyingi Sana sehemu nyingi duniani kwa dakika chache, ndoto ni maisha halisi yanayoendelea duniani.
 
Roho ikikamatwa na wachawi ikiwa inazunguka duniani, mwili hauwezi amka ndio unasikia mtu alilala kalala jumla kufa usingizini. Means roho haikufanikiwa kurudi kwenye mwili.
 
Pili mtu akilala usikurupuke usimstue kumuasha kwa nguvu ni hatari kama roho iliacha mwili.
Dunia Ina mengi still bado sayansi haijatupa majibu
 
Write your reply...Mimi roho yangu inaonana na watu ila nakua siongei,napata raha kwenye kupaa.mda mwingine nakutana na wadada wazuri ila sijawahi wagusa
 
Roho ina ubongo? Kama haina utendaji wake unaongozwa na nn?
 
Haha ila mkuu si inasemekana kufanya hivyo ni dhambi
Kwakwel sijui kama ni dhambi Ila nilidhibitisha kitu kimoja kuwa,kwanini tukiota usiku tunakimbia au kucheza au kupigana mbona huwa mwili umetulia Tu kitandani?

Kumbe mara tuanzapo kulala kuna ganzi ya asili ambayo huja mwilini na Kutofanya mwili utulie la sivyo tungekuwa tunaamka na majeraha Sana kutokana na ndoto tunazoota.

Binafsi mara moja moja Sana hujikuta narusha mguu usingizini na kugonga kitanda huenda ganzi ya asili huwa inapotea kiaina
 
Roho ina ubongo? Kama haina utendaji wake unaongozwa na nn?
Mkuu mambo ya roho au elimu ya roho imefichwa Sana na Mwenyezi Mungu.

Watu walimuuliza Mtume kuhusu roho,Allah akajibu kuwa elimu ya roho iko kwakwe na watu hawajui elimu yake isipokuwa Ile ndogo waliyopewa.

Kwahiyo hatuna zaidi tunachokijua zaidi ya kile kidogo alichotufahamisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…