Je, unajua kuwa wabongo wengi hawasikilizi ili waelewe, bali wanasikiliza ili wajibu?

Je, unajua kuwa wabongo wengi hawasikilizi ili waelewe, bali wanasikiliza ili wajibu?

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
13,682
Reaction score
41,162
Changamoto nyingi za maisha zina sababishwa na tone (namna ya kuongea) Sio maneno tunayosema yenye umuhimu mkubwa, bali ni jinsi tunavyo yasema. Badilisha tu namna unavyosema, utaona mabadiliko katika maisha yako ebu nitowe mfano moja:

Afisa wa jeshi la Polisi alikuwa akizungumza na mkulima mzee mkoa wa Mara akamuambia Nahitaji kukagua shamba lako kwa sababu kuna madai ya mmea wa bangi unaolimwa kinyume cha sheria.

Mkulima akasema, "Sawa kabisa, ila tafadhali usiende kwenye lile shamba kule..." huku akionyesha kwa kidole mahali aliko maanisha.

Polisi akamjia juu kwa sauti ya hasira, "Bwana, nina mamlaka kutoka kwa Serikali!" Kisha akaonyesha kwa kiburi kitambulisho chake. "Unaona hiki Kitambulisho? Hiki kinaniruhusu kwenda popote ninapotaka. Usiniulize maswali wala usitegemee majibu! Je, nimeeleweka? Unanielewa?"

Mkulima mnyenyekevu akatikisa kichwa kwa adabu, akaomba msamaha, kisha akaendelea na kazi zake.

Muda si mrefu, vilisikika vilio vikubwa vya hofu
Mkulima alitazama juu, akamwona afisa wa polisi akikimbia kwa uoga mkubwa, akiwa amezungukwa na jeshi la nyuki pori.

Afisa huyo alikuwa anaonekana kabisa kuwa amepanic. Mkulima akaacha zana zake, akakimbia hadi kwenye uzio, kisha akapiga kelele kwa sauti kubwa sana...
"Acha kukimbia! Waonyeshe Kitambulisho Chako!"

1. Ukosefu wa unyenyekevu huleta fedheha.
2. Kiburi hutangulia anguko.
3. Kua na cheo serikalini halikufanyi kutokua binaadamu tena.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Jesus said "love your enemy more than you love your self" true or false?
Sasa huyo Jesus ni nani kwangu ,mbona huyo babu unamwita mnyenyekevu baada ya huyo pot kuumwa na nyuki alitoa kejeli pia😁
 
Obama ni mweusi ila ni humbe down to earth sio weusi wote, sema wabongo mpe cheo utaona rangi Zake halisi,
Unamfahamu vizuri obama na aliyoyafanya kipindi cha uongozi wake?? Kasome na ufanye utafuti alafu uje utuoneshe hiyo "humbleness" yake
 
Sasa huyo Jesus ni nani kwangu ,mbona huyo babu unamwita mnyenyekevu baada ya huyo pot kuumwa na nyuki alitoa kejeli pia[emoji16]
Mkuu hujui kwamba Jesus ni Mungu kamiri katika Dini zingine anaabudiwa kabisa.
 
Uko Imara sawa ila huoni kwamba trump iko kwenye mfumo ule ule ila ni very arrogant racist en sturbon
Trump yupo sahihi mlikuwa mnataka mpewe USAID ili mzotumie hizo hela kuishi kifahari huku lengo alifikiwi .

Watu Kama,trump ni,smart and visionary na,sio arrogant
 
Back
Top Bottom