Mimi nilikua Msange Tabora, kwa afande Kashandago ...mchoooovu!
I think in-take yetu ilitwa "Azimio la Arusha" 1987/88
Tabora bwana kuna nyoka (afande wa porini) acha mchezo. Alafu zambarau nyingi lakini ukizila kwa wingi zina ziba haja kubwa, so you have to program some days off for haja kubwa, otherwise it is mission impossible!
Ukienda msalani (vyoo vya shimo) inabidi uende half naked, with less clothing. Maana ukienda na nguo ukirudi hanger lote linanuka!!
The most memorable thing I can remember is nilishea godoro (nikisema tulilala pamoja inasoundi vibaya) na jamaa kama wiki mbili hivi bila kujua sura yake maana tulikua tukiamshwa saa kumi usiku (giza), na kurudi kulala Saa 4 usiku, pia gizani. Sikumoja tukisaga mahindi, nikaitambua sauti nakumwambia "babu unajua tuna shea godoro" basi wote tukashaangaa na kucheka sana - having spend over 10 nights together, but without knowing each other's face!
Mestini bwana was probably the most important item you could have. Yani hiyo unanawia uso na kupiga mswaki, unanywea chai, chakula, unaijaza mkaa iliipate moto alafu unapigia pasi nguo, unaitumia kuogea, kufulia, kuandikia barua ukiwa porini, kulalia kama mto ukiwa umetoroka porini, n.k. Yani ukipoteza mestin your life is done. Mimi nilikuwa naikumbatia usiku maana walikuwa wana ziiba sana.
Walinipa grade ya "D" - tabia hafifu!
Those were the days!