Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Nilikuwa nachukia sana mchakamchaka wa asubuhi. Nilikuwa nakimbia mara chache sana.

Nyinyi ndio mlikuwa mnaitwa Maselule!!
Mchakamchaka ndio utamu wa JKT..mnakimbia huku mnaimba..wala hamchoki!!...Mnakumbuka Malele wangu namtafuta..n.k
 
Siamini kamwe kuwa wanao-miss JKT wanazungumza toka moyoni. Licha ya mazoezi mazuri ya kijeshi na ukakamavu, lazima ikubalike pia kuwa waliokosa JKT waliepukana na mateso, uonevu na unyanyasaji. Kama ningewajibika kurejea nyuma na kwenda JKT nikijua ninayoyajua sasa nisingekwenda na ningemshangaa sana yeyote yule ambaye angekwenda tena kwa ridhaa yake.
 
heeee binti maringo usiniambie na weee ulibahatika kuwa geshini!!!!!!!!!!! si tunaambulia stori tu kama hivi maskini tulikosa mengi pamoja na ya kusimamisha minazi hahaaaaaaaaaa!!! (we veri naughty_)

Bht!...it was good experience kwa kweli!...aaah eeh ile giza giza likifika watu walikwua busy kusimamisha minazi nakwambia...mademu wanakwenda angani wanajiremba kwenda kusimamisha minazi yao....miye na group yangu tulikuwa don't care tulikuwa tunapanga mikakati ya kutoroka tuu!.....yaani Bht omba jeshi lirudi ujiunge ni kazi sana ila ukishatoka unaona raha yake...too bad hata experience ya kupiga range sikuipata...if i would i could!!

AlMusoma....I thinkwatu wanaongelea ile experience waliyoipata wakiwa jeshini...pia nadhani jeshi kwa upande mwingine limefundisha wenfi kuondokana na uselule....maselule wengi walikuja kuwa wakakmavu sana....me personally sikujua hata kama ningekuja kulima mraba mrefu like 2 miles hivi na kumaliza...zile first 2 month ilikuwa inanichukua like whole day kulima mraba mmoja tuu hapo wenzako wameshamaliza like 2 hours ago miraba 2 tayari....jeshi linakufanya uwe mkakamavu sana...miye limenifanya niwe strong and independent kwa kweli!....though ilikuwa miezi 6 tuu basi...
 
Bht!...it was good experience kwa kweli!...aaah eeh ile giza giza likifika watu walikwua busy kusimamisha minazi nakwambia...mademu wanakwenda angani wanajiremba kwenda kusimamisha minazi yao....miye na group yangu tulikuwa don't care tulikuwa tunapanga mikakati ya kutoroka tuu!.....yaani Bht omba jeshi lirudi ujiunge ni kazi sana ila ukishatoka unaona raha yake...too bad hata experience ya kupiga range sikuipata...if i would i could!!

dah mi nahisi ningefia huko bana!!!!

hapo kwenye bold hapo inaonekana we wa kiivo sana (sungura) hahaaaaa!!! nice!!

wee mbona jamaa mwingine hapo juu kanitisha eti atashangaa kusikia mtu anajiunga on his/her own accord?? nikapata picha huko kulikua balaaaa!!!
 
dah mi nahisi ningefia huko bana!!!!

hapo kwenye bold hapo inaonekana we wa kiivo sana (sungura) hahaaaaa!!! nice!!

wee mbona jamaa mwingine hapo juu kanitisha eti atashangaa kusikia mtu anajiunga on his/her own accord?? nikapata picha huko kulikua balaaaa!!!

hahaha Bht kufa ufi ula cha moto utakiona...wee muda ule umshamaliza kula unataka kwenda kulala umechoka unaambiwa kwanza lazima uende kuimba na kuitwa roll call...Kitu kilichokuwa kinaniudhi ilikuwa wakati wa kula lazima upige kwata ile unapitwa mbele ya RS....Kusema kweli uongo mbaya nilikuwa selule nilikuwa mgonjwa everyday na pia nilikuwa na take advantage ya my uncle kusema kweli alikuwa brigedia na alikuwa anogopeka sana hiyo ndiyo advantage niliyoipatia ndiyo maana mraba nikawa namaliza muda naotaka na nilikuwa ansaidiwa pia....

Nilipata pass ya one week my grandfather ali pass away hiyo ilikuwa ndiyo opportunity ya mimi kuondoka na kuingia mgulani kambi ya maselule...aah huko bht ilikuwa raha sana maana nipo home kila weekend upo home tukirudi usiku ile jumapili tunatoroka tunaingiza club mjini..unakuja kupitiwa na marafiki wanakuwa wanakubiria nje (kuna tundu lilikuwa linaitwa tundu la nyerere)...kasheshe wakati wa kurudi unarudi unanyata kishenzi usije kushikwa na afande hahaha great momeny kwa kweli..utoto raha sana!
 
Sanctus mimi ninachokumbuka nikiwa Makutopora ni afande wa kilimo kutupeleka kumwagiam mizabibu wakati mvua inakarabia kunyesha. Jamaa alikua sadist. Halafu kuna mwingine afande Chuwa Mkibosho mwenye sauti ya kukwaruza halafu kanuna masaa 24. Mbabe ambaye adhabu anazokupa ni wewe mwenyewe kuchimba shimo lenye urefu wako halafu unaingia. Anamwagiza kuruta mwingine kukufukia hadi shingoni na kukuacha hapo jua linakupiga hadi jioni. Jamaa alikuwa katili kweli.

Nakumbuka kuagizwa kwenda kuvaa green vest nyeupe. Mkuu wetu alikuwa Brigadier Mwakanjuki.Tulikuwa tunampenda sana kwa sababu alikuwa anapoongea na sisi anaongea English na maafande wanatoka kapa. Hiyo ilikuwa inatupa raha sana. Wakiuliza hivi mkuu kasema nini? Tunawaambia katuambia mkitunyanyasa twende tukashtakie kwake. Hahaha.

Nilikuwa napenda sana kufanya kazi jikoni kwa sababu ya kuonja michuzi na kunywam chai kula mikate ya tanbond. Ilikuwa starehe kweli.Na kwenda kufagia banda la kuku wa mayai. SIku nzima twachemsha mayai. Mimi sio siri JKT nilinenepa haswa. Sikuwa na mawazo hata chembe. Niliwaachia maafande wafikiri kwa niaba yangu. Kila ninachoagizwa natii lakini wakati wa kutekeleza natumia akili yangu. Kanuni ya kumpeleka punda mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji ndiyo nilikuwa naitumia.
 
.........Nimependa story zenu za JKT..........sijui kwa nini serikali waliondoa hii kitu, wengine tumekosa huu uhondo.......lol!!
 
Thread nimeipenda sana hii, hasa kwa mtu km mimi ambaye life iko frustrated kiasi cha kucheka hata mara moja kwa mwezi. Nimecheka sana na sijawahi kucheka namna hii tangu nianze kusoma posts hapa jf.
Well mimi nilikuwa bulombora mwaka 92/93 operation vyama vingi. Nilianzia danger coy hatimaye nikawa niko hq kwenye kitengo cha chokaa, ziwani ndani kabisa tukiwa na afande mayila.

Nawakmbuka sana hasa wasichna wa dander coy sku moja afande makoba wakamwambia cock-up, neno amablo alikuwa analitumia yeye kutukana, halafu issue yote ika-end up combineer nzima kujenga reli tukiwa uwanja wa damu.

Nakmbka sana pia afande RSM yule mwembamba kabisa aliyekuwa anapiga maki-time kwa kishindo sana kuanguka akitoa demonstration ya namna service men wanavyotakia kutembea, hatua (za kasi, ndefu) 120 kwa dakika, halafu mwenyewe kusingizia kuwa alikuwa ana-demonstrate namna askari mzembe anavyoweza kufanya, NA BAADA YA PALE ndiyo watu wakapata kisingizio cha kutoa kicheko ambacho walikuwa wamelazimika kukibana.

Ucheke RSK kaanguka? ikabidi walipuke. Nawakumbuka sana rafki zangu wapenzi tuliokuwa nao hasa waimbishaji wa changer jioni D- coy akina Yasinta John, Esther Koroti, Winfrida Bita, Bahat Katani, Mbogo Mnubi na wengine wengi. Anayejua yasinta yuko wapi anaweza akani-pm
 
Mie nilikuwa Mafinga JKT 1991/92,Kombania DANGER - Operesheni Miaka 30 ya Uhuru. Mliokuwa Mafinga mnawakumbuka CO Mlay, Saa Meja Ndosa, Staff Sajenti Sagaya? Waliokuwa Kombania A, mnamkumbuka OC Singano? Mafinga ilikuwa na Winta la ajabu. Unaamshwa saa 10 usiku kufagia, huoni takataka kutokana na giza nene, lakini unafagia hivyo hiyo. Kukicha ni kusafiiiiiiiiiiii ajabu.
 
Nilikuwa Ruvu JKT miaka ya 1975 wengi wenu hamjaona mionzi ya jua kabisa, tulikuwa tunapangwa kwenye kazi mbalimbali. Kwenye mabanda ya kuku tukajifunza kula mayai mabichi kama kenge kila ukicheua ni mayai tu. Ikatokea rafiki yangu mmoja akaona aibe mayai kiasi akayaweka kwenye jungle hat akaivaa akawa anatembea kwa uangalifu sana. alipofika eneo fulani akakutana na afande akaambiwa mbona kofia yako haijakaa vizuri? Kabla hajajijbu afande akaivuta ili ikae vyema kichwani. Mayai yalivunjika na yakaanza kuchuruzika usoni na mwili mzima. Ilikuwa adhabu tosha hata afande hakumfanya kitu tena. Mambo ya JKT hayo....
 
Nilikuwa Ruvu JKT miaka ya 1975 wengi wenu hamjaona mionzi ya jua kabisa, tulikuwa tunapangwa kwenye kazi mbalimbali. Kwenye mabanda ya kuku tukajifunza kula mayai mabichi kama kenge kila ukicheua ni mayai tu. Ikatokea rafiki yangu mmoja akaona aibe mayai kiasi akayaweka kwenye jungle hat akaivaa akawa anatembea kwa uangalifu sana. alipofika eneo fulani akakutana na afande akaambiwa mbona kofia yako haijakaa vizuri? Kabla hajajijbu afande akaivuta ili ikae vyema kichwani. Mayai yalivunjika na yakaanza kuchuruzika usoni na mwili mzima. Ilikuwa adhabu tosha hata afande hakumfanya kitu tena. Mambo ya JKT hayo....

Mkuu, miaka hio jeshi si lilikuwa ni miezi sita tu? Hivyo hamkuvunwa sana.
Mjomba wangu alikuwa Ruvu miaka hiyo ...nakumbuka aliniambia CO alikuwa Major Makame Rashid (wakati huo).
 
Binti Maringo,
Binti Maringo Kumbe Karubi uncle wako ehe!. Mie nilikuwa oljoro 89/90, nikikumbuka tu hilo shamba la dunia nakua siamini kama nilikuwa naweza kumaliza mraba on time. Nilikuja kunyaka kitego cha Generator kule farming kwa hiyo nikawa na kazi ya kumuwashia umeme tu Brig Karubi!.
 
Mimi nilikua Msange Tabora, kwa afande Kashandago ...mchoooovu!
I think in-take yetu ilitwa "Azimio la Arusha" 1987/88

Tabora bwana kuna nyoka (afande wa porini) acha mchezo. Alafu zambarau nyingi lakini ukizila kwa wingi zina ziba haja kubwa, so you have to program some days off for haja kubwa, otherwise it is mission impossible!

Ukienda msalani (vyoo vya shimo) inabidi uende half naked, with less clothing. Maana ukienda na nguo ukirudi hanger lote linanuka!!

The most memorable thing I can remember is nilishea godoro (nikisema tulilala pamoja inasoundi vibaya) na jamaa kama wiki mbili hivi bila kujua sura yake maana tulikua tukiamshwa saa kumi usiku (giza), na kurudi kulala Saa 4 usiku, pia gizani. Sikumoja tukisaga mahindi, nikaitambua sauti nakumwambia "babu unajua tuna shea godoro" basi wote tukashaangaa na kucheka sana - having spend over 10 nights together, but without knowing each other's face!

Mestini bwana was probably the most important item you could have. Yani hiyo unanawia uso na kupiga mswaki, unanywea chai, chakula, unaijaza mkaa iliipate moto alafu unapigia pasi nguo, unaitumia kuogea, kufulia, kuandikia barua ukiwa porini, kulalia kama mto ukiwa umetoroka porini, n.k. Yani ukipoteza mestin your life is done. Mimi nilikuwa naikumbatia usiku maana walikuwa wana ziiba sana.

Walinipa grade ya "D" - tabia hafifu!
Those were the days!
 
Wakati wa operation"JIHAMI" mkuu wa kambi ya JKT Mgambo alikuwa anaitwa Kanali Mtono. Huyu bwana ilikuwa vigumu na nadra sana kumkuta akicheka hata kama yupo na maofisa wenzake na wote tuliamini kwamba jamaa hacheki. Siku moja tukiwa na disco jamaa aliendelea na tabia yake ya kuuchuna muda wote alipokuwa anacheza na mabinti mbalimbali. Lakini alipokuja mke wake(ambaye alikuwa lance coplo) na kumwomba wacheze naye jamaa alisimama na kucheza huku meno yoote 32 yakiwa nje, Kila mtu alishangaa alipoona kitendo hicho kilichoonyesha NGUVU ISIYO YA KIJESHI WALIONAYO MAMA ZETU.
 
Wazalendo na Wanataaluma,

Miaka miwili baadaye kila ninapopitia thread hii, inanipa burudani ya namna yake.

Sijui kama bado wanaopenda kushare experiences zao za JKT ili tujikumbushe?
 
Nakumbuka tulivyokatwa bogi kutoka Ruvu kwenda mlale! Its a along and interesting story. Naikumbuka Rukumbulu mountains isiyokuwa na lami na kusimama kuonyeshwa kaburi la askari waliokufa wakitoka vitani uganda. Hii ilikuwa operesheni kujihami. Maisha yalikuwa magumu lakini natamani kuyaona tena
 
Mie nilikuwa Mafinga JKT 1991/92,Kombania DANGER - Operesheni Miaka 30 ya Uhuru. Mliokuwa Mafinga mnawakumbuka CO Mlay, Saa Meja Ndosa, Staff Sajenti Sagaya? Waliokuwa Kombania A, mnamkumbuka OC Singano? Mafinga ilikuwa na Winta la ajabu. Unaamshwa saa 10 usiku kufagia, huoni takataka kutokana na giza nene, lakini unafagia hivyo hiyo. Kukicha ni kusafiiiiiiiiiiii ajabu.

Mlay alikuwa kiboko mshikaji wangu. Alikuwa anawatia lupango hata mbuzi wakilisha maeneo ya jeshi. Kale katoto kake kaliokuwa kanasoma darasa la tatu aliwahi kukatia lupango kwa kukataa kwenda shule.

Yule Danda wa danger coy alikwepo wakati wenu? Singano CCM tulimkuta pamoja na Kakakuona bila kumsahau kamata Rwakutununta. Alikuwa mchafu kwa watoto kupita kiasa.

Itetelo, dubuluganga unapakumbuka. Yule CO wa Dubuluganga ulimkuta? One Leg mlizikuta story zake.

Du umenikumbuza mengi nitalala vizuri leo
 
Back
Top Bottom