Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Nimemkumbuka kalikuwa kanaitwa afande Msagati... Sikonge!!

cpl msagati. cpl mandevu. sgt. wela. sgt sijali. lt kajoro. lt mchaga mmoja tulimwita mchina. capt ngowo. major mznz. lt col sanga. bila kumsahau Frida. sasa hivi volunteer masanja ni ssgt yuko kigamboni
 
Last edited by a moderator:
Katika sehemu umenikumbusha ni Lwamkoma dah nakumbuka kipindi cha palizi nilipewa mstari mmoja na nusu! Dah nikapalilia ila nilikoma stasahau chakula kile maana hata nguruwe mpenda kula hakiwezi chakula ugali mbaya na dagaa zinamawe, nyasi wameloweka na kuchemsha wakatuletea shamba dah hapana op Kizota!! My force no W73.....
 
Kwa wale wa oparesheni Kambarage Mafinga JKT A Coy, kuna viumbe kama SS Mwakyosi, SS Shembiru, Korokoro II Mwakililo, Cpt Waziri na Copy ya Ajutant Frank Kalaghe - hii combination nayo mh!!! nakumbuka nilipoteza mess tin nikaambiwa songa mbele nilipofika usawa wa guduria nikaletewa kipande cha gazeti na Ss Shembiru nikaambiwa shika - kinga pale Frank mgawaji wa chakula akaweka kitu kwa gazeti, kasheshe ikaja nitachukuaje mboga, SS Mwakyosi akanambia kandamiza ngumi juu ya ugali tengeneza shimo na kumwamuru Mgawa mboga Nyakunga kuniwekea mboga kwakweli maisha yale niliyaona ni muhimu sana katika kupambana na mazingira
 

Haaaa haaaa KakaKiiza pole sana. Simulizi hizi ni tamu sana. Nani alikuwa CO wakati huo?
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha kamanda umenikumbusha mbali mimi nilikuwa Mafinga operation awamu ya pili namkubuka sana afande nusu Mungu alikuwa anafundisha somo la usalama wa taifa,E.COY alikuwa anajisifia kuwa alimsurubu Marehemu Kawawa. nakumbuka nyahenge (baridi) wakati tukichunga Ngo`mbe maeneo ya changalawe na shamba la mahindi idetero, namkumbuka marehemu Afande Nditi alivyokuwa akiongoza Brassband kwa mbwembwe kwelikweli, Mungu amampe raha ya milele na mwanga wa milele amwangazie
 
Da umenikumbusha nilikuwa msange jkt du kawa leli maisha ya jeshi ni mazuri ndio maana watoto wa sasa hivi hawana adabu aliyepitia jkt lazima awe na adabu mimi nakumbuka rootmarch tulitembea usiku mzima toka msange mpaka tabora mjini du jeshi ni kukomaa leo ukiniambia toka sinza mpaka mwenge sifiki
 
Op vyama vingi. 822KJ chini ya Col Ng'umbi. Zaina zaina...... Zaina kuruta zaina lete raha zaina. To be honest wasio enda jeshi wamemiss kitu muhimu maishani. One day nilijongo saa 9 usiku na kuruta mwenzangu tuko poli mara tunaona wajenda hawa tukala uchaka kumbe wale nao ni kuruta wanajongo tena wa kike. Matilida Sabai na.... Sikumbuki tulivyo kuja gundua ni majongolist wenzetu..... Kwenda kuiba miwa na SMG, maandazi na mihogo.Duhuuuuuu. Afande chacha mwanaume ana folenisha kikosi kizima peke yake.... Afande Richonjo...afande malaza kwa mapololo hahaaaaaa
 
Ingawa binafsi sijapitia JKT lakini katika story zote za JKT nilizozisikia sijawahi kusikia waungwana wakizungumzia maluteni kanali.

hahahahahahahahahahahahaha wengine waaaandika kumbe hata hawapita huko na mungu hamfichi muongo kama huyo alieandika luteni
 
Nilipitia kambi kadhaa za jeshi ambako kote ilikuw ni vurugu fujo tu; kwanza nilianzia Mgambo kwa Col Mtono ambako nilipoteza kama miezi miwili, baadaye nikaenda Ruvu kwa Col Makame kuhudhuria course ya leadership tukiwa chini ya Capt Sungura. Baada ya kumaliza kozi ile na kupata tepe zangu, nikaenda Mgulani kwa Col Karubi kwa ajili ya gwaride la Muungano; kipindi hicho pia nikashiriki ile operesheni ya walanguzi iliyokuwa imeanzishwa na Sokoine, mwishoni nikaenda kumaliza service yangu kule Mbweni ambapo sikumbuki hata jina la CO wake kwa vile nilikaa pale muda mfupi sana.

Nilifurahia sana maisha pale Mgulani na Mbweni baada ya kuwa nina tepe zangu begani kwani nilijua sana namana ya kuzitumia; usiniulize niliztumiaje.


Mambo manne makubwa ninayokumbukia JKT ni:

(a) Ukakamavu: Hili ni jambo lililonisumbua sana baada ya kurudi uraiani kwa vile ukosefu wa shughuli za musuli ukawa unanifanya niwe nashambuliwa na muscle cramps za mara kwa mara. Nilipenda sana maisha ya ukakamavu.

(b) Ujasiri: Jambo ambalo huenda wengine hawakukiona ni lile la ujasiri. Wakati huo nilikuwa niko tayari kufanya lolote bila kuogopa. Kwa hiyo upambanai na ma MP halikuwa tatizo kubwa kabisa kwangu.

(c) Uzalendo: Nadhani jambo moja kubwa sana ambalo limeshatoweka kabisa ni kuhusu uzalendo. Mafunzo yale ya JKT yalikuwa yanastimulate sana vijana kuipenda nchi yao kama taifa moja. Ni sehemu pekee ambayo ilikuwa inakutanisha vijana wenye kutoka sehemu mbalimbali za nchi na wenye background tofauti na kuwa treated kama wamoja.

(d) Unafiki: Jambo pekee ambalo sikulipenda JKT ni unafiki. Kulikuwa na unafiki mwingi sana ukiambatana na nidhamu za woga. Nadhani jambo hili lilikuwa ni baya zaidi ya faida zote za JKT kwa vile kuna walioendelea na maisha hayo ya unafiki hata pale walipokuwa na madaraka makubwa kiserikali; kwa hiyo matendo yao ya hadharani yakabaki siyo reflection ya imani na matendo yao halisi wanapokuwa peke yao.
 
Ambacho sitasahau ni siku moja afande alijisaidia kwenye mlango wa hanga akatusingizia. Tukapewa adhabu ya kuchukua kila mtu kidogo kidogo. Akajitolea mmjo kuzoa lakini wakakataa. Kila mtu alishika mpaka ikaisha.

hilo tukio ni la mgambo.

mahanga ya "serengeti" kwa kumbukumbu zangu

lilikuwa ni tukio la aina yake
 
kunyanyua mikono juu wanapima nn kwenye kifua?

daktari wa jeshi ndo anajua alikuwa anaangalia nn, alaf hii ni kwa ajil ya air force command sasa sijui taratibu zao zinatofautiana na land force command..lkn jamaa walisema hawana complicated tastes km wengine
 

hivi hii ya kwenda jw hadi kupitia jkt ipo kisheria..lkn mbona naskia wengine wanaenda jw direct...hii imekaaje wakuu
 
mmeshindikana uraiani ndio mmekuja hapa kushindanana ! ................. hapa hafukuzwi mtu !


Umenikumbusha mesemo huu "...aroo kuruta uliye vaa griinvesti ya njano kuja hapa..." Heheheheeee green vest ya njano
 
Matangazo ya kujiunga yanatoka lini?nilifuatilia kweli mwaka jana wakati nimemaliza chuo lakini sikufanikiwa napigiwa tu simu na wenzangu kuwa wameshapata kwa njia ya wakubwa,je kwa wale wa kufuata haki unapataje hiyo nafasi ya kujiunga JKT(taarifa nitapata wapi)?na pili ukiwa na target ya kwenda jwtz au intelligence inakuaje?
 

mkuu israel, mbona nafasi za jkt wametangaza trh 30/11 pia hata za jw direct wametoa..fika ofisi ya mshauri wa mgambo wilaya uliyopo...
 
Ahsante mheshimiwa.vipi kuhusu target ya kuingia jwtz au intelligence inakuaje hasa ili kukamata hizo nafasi?na kama una professional ya IT and Network Engineering uhakika upo wa kupangiwa hiyo au ndio unaweza kutupwa kitengo kingine?
 
1984 Mlale JKT sitasahau afande 'Nguvu ya Nyani, wa Chale Coy! Hii ni operation NGUVU KAZI wakuu!!! Meja Mandwa alivyotutesa silaha ilipoibiwa! Afande Ngunduguru watu walivyokuwa wakimdhihaki kwa kumwita Mku....nduguru!!!! Namisi Chipole kwa masista na mihogo ya Embakasi na kule kijijini kwenye Ulanzi na kitimotoz! Namisi Disco la kuimba huku mmekaa na kupiga makofi, namisi Mustini wangu kiunoni, na misi Kujongo kwenda magagula! Bustani ya tomato, Cabbage nk! Kweli duniani maisha ni historia!!!
 

Hapa pia nawakumbuka marafiki zangu wengi sana wa C coy, Mbogo,Anthony Nyarubamba,Kezia Mpumilwa, Eliza Mlelwa,Eliza Mlay,Elizabet Amenye Mwaipungu, Saimon Limo,Gwakisa,na Alfred Mwakivvike, na wengine wengi wengi sana!!!!!!
 
Ruvu jkt operation vyama vingi .d coy namkumbuka afade sanga .ruta.kibuyu.matron zela.du nakumbuka matusi ya matron zela km kapitia chuo cha matusi kuna cku niliforge sahihi ya dr omar nikapigwa 45m ex drill kesho yake nika sepa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…