Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Nimemkumbuka kalikuwa kanaitwa afande Msagati... Sikonge!!

cpl msagati. cpl mandevu. sgt. wela. sgt sijali. lt kajoro. lt mchaga mmoja tulimwita mchina. capt ngowo. major mznz. lt col sanga. bila kumsahau Frida. sasa hivi volunteer masanja ni ssgt yuko kigamboni
 
Last edited by a moderator:
Wazalendo;

Moja ya shemu ya maisha yangu ambayo kamwe sitasahu ni kupitia JKT.

Nilijiunga na JKT Ruvu na baadaye nikaenda Service Buhemba Lwamkoma.

Sitosahau kamwe mafunzo ya ukakamavu, kwata, mchaka mchaka, disko na vitimbi mbalimbali kati ya Makuruta na Maafande. Nilikuwa Combania E.

Moja ya vituko vya kukumbuka ni simulizi kutoka- Operation OKOA, kulikuwa na huyu jamaa alikuwa ni mweusi sana anaitwa afande Lucas, badala ya kuwaaamsha kuruta kwa filimbi, alikuwa anaingia na kuvuta Sigara. Kuruta inatakiwa ukisikia harufu ya Sigara uamke na kufoleni nje. Usipotoka in time unakula mijeledi.

Basi siku moja Kuruta wakapanga wamfanyizie na wakatoka mapema nje na kujificha huku ndani kwenye Bweni wakiyaviringisha mablanketi mithili ya mtu amelala. Afande alipomaliza sigara hakuna aliyetoka akajua siku hiyo kuruta wamegoma kuamka na kuanza kuchapa viboko yale mablanketi yaliyovingirishwa. Alishtukia kaanza kushambuliwa yeye na kuruta toka nje ambao walikuwa na fimbo kibao mpaka akakoma. Kisha kuruta wakafoleni nje. Nakumbuka Mkuu wa Kombania alipata habari na kulikuwa na drill si kawaida na mpaka push ups za kunusa mkojo katika nyasi walizokuwa wanakojoa kuruta usiku. Hata hivyo yule afande naye alikoma kwani hakurudia mchezo wa kuwaamsha watu kwa sigara.

Kwa waliokuwa Ruvu Operation Okoa:

Na miss - Ugali na korosho mnapojongo kambini
Namiss Mihogo ya Vibwende kwa Babu
Wali na Maembe
Uji wa Mestin ya Jeshi
Bukta na Green Vest
Kuokota kuni
Bustani
Michezo
Disco . . . Ama Johnnnnn ambaaaa ambaaa John, amba Johnnn wa Tanzania . .

. . . . Arusha Mbali, Arusha Mbali, tukumbukane kwa Barua nk.

Nakumbuka pia siku moja sikuimbisha disco vizuri na kipindi kile 1985 bado kulikuwa kuna ubaguzi wa rangi Africa Kusini, basi afande akanipiga mkwala na kuniambia . . . .

"Kuruta nitakutemea mate yenye sumu usoni upofuke macho, na sijui utatibiwa wapi kwani mipaka yote Afrika Kusini imefungwa . . . (Kana kwamba hakukuwa na hospitali ya kutibu mate ya sumu hapa bongo"

Jamani mliokosa JKT, mlikosa mengi, japo tulipata tabu lakini tulijifunza mengi katika maisha.

Je, wewe unakumbuka nini?
Katika sehemu umenikumbusha ni Lwamkoma dah nakumbuka kipindi cha palizi nilipewa mstari mmoja na nusu! Dah nikapalilia ila nilikoma stasahau chakula kile maana hata nguruwe mpenda kula hakiwezi chakula ugali mbaya na dagaa zinamawe, nyasi wameloweka na kuchemsha wakatuletea shamba dah hapana op Kizota!! My force no W73.....
 
Kwa wale wa oparesheni Kambarage Mafinga JKT A Coy, kuna viumbe kama SS Mwakyosi, SS Shembiru, Korokoro II Mwakililo, Cpt Waziri na Copy ya Ajutant Frank Kalaghe - hii combination nayo mh!!! nakumbuka nilipoteza mess tin nikaambiwa songa mbele nilipofika usawa wa guduria nikaletewa kipande cha gazeti na Ss Shembiru nikaambiwa shika - kinga pale Frank mgawaji wa chakula akaweka kitu kwa gazeti, kasheshe ikaja nitachukuaje mboga, SS Mwakyosi akanambia kandamiza ngumi juu ya ugali tengeneza shimo na kumwamuru Mgawa mboga Nyakunga kuniwekea mboga kwakweli maisha yale niliyaona ni muhimu sana katika kupambana na mazingira
 
Katika sehemu umenikumbusha ni Lwamkoma dah nakumbuka kipindi cha palizi nilipewa mstari mmoja na nusu! Dah nikapalilia ila nilikoma stasahau chakula kile maana hata nguruwe mpenda kula hakiwezi chakula ugali mbaya na dagaa zinamawe, nyasi wameloweka na kuchemsha wakatuletea shamba dah hapana op Kizota!! My force no W73.....

Haaaa haaaa KakaKiiza pole sana. Simulizi hizi ni tamu sana. Nani alikuwa CO wakati huo?
 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha kamanda umenikumbusha mbali mimi nilikuwa Mafinga operation awamu ya pili namkubuka sana afande nusu Mungu alikuwa anafundisha somo la usalama wa taifa,E.COY alikuwa anajisifia kuwa alimsurubu Marehemu Kawawa. nakumbuka nyahenge (baridi) wakati tukichunga Ngo`mbe maeneo ya changalawe na shamba la mahindi idetero, namkumbuka marehemu Afande Nditi alivyokuwa akiongoza Brassband kwa mbwembwe kwelikweli, Mungu amampe raha ya milele na mwanga wa milele amwangazie
 
Da umenikumbusha nilikuwa msange jkt du kawa leli maisha ya jeshi ni mazuri ndio maana watoto wa sasa hivi hawana adabu aliyepitia jkt lazima awe na adabu mimi nakumbuka rootmarch tulitembea usiku mzima toka msange mpaka tabora mjini du jeshi ni kukomaa leo ukiniambia toka sinza mpaka mwenge sifiki
 
Op vyama vingi. 822KJ chini ya Col Ng'umbi. Zaina zaina...... Zaina kuruta zaina lete raha zaina. To be honest wasio enda jeshi wamemiss kitu muhimu maishani. One day nilijongo saa 9 usiku na kuruta mwenzangu tuko poli mara tunaona wajenda hawa tukala uchaka kumbe wale nao ni kuruta wanajongo tena wa kike. Matilida Sabai na.... Sikumbuki tulivyo kuja gundua ni majongolist wenzetu..... Kwenda kuiba miwa na SMG, maandazi na mihogo.Duhuuuuuu. Afande chacha mwanaume ana folenisha kikosi kizima peke yake.... Afande Richonjo...afande malaza kwa mapololo hahaaaaaa
 
Ingawa binafsi sijapitia JKT lakini katika story zote za JKT nilizozisikia sijawahi kusikia waungwana wakizungumzia maluteni kanali.

hahahahahahahahahahahahaha wengine waaaandika kumbe hata hawapita huko na mungu hamfichi muongo kama huyo alieandika luteni
 
Nilipitia kambi kadhaa za jeshi ambako kote ilikuw ni vurugu fujo tu; kwanza nilianzia Mgambo kwa Col Mtono ambako nilipoteza kama miezi miwili, baadaye nikaenda Ruvu kwa Col Makame kuhudhuria course ya leadership tukiwa chini ya Capt Sungura. Baada ya kumaliza kozi ile na kupata tepe zangu, nikaenda Mgulani kwa Col Karubi kwa ajili ya gwaride la Muungano; kipindi hicho pia nikashiriki ile operesheni ya walanguzi iliyokuwa imeanzishwa na Sokoine, mwishoni nikaenda kumaliza service yangu kule Mbweni ambapo sikumbuki hata jina la CO wake kwa vile nilikaa pale muda mfupi sana.

Nilifurahia sana maisha pale Mgulani na Mbweni baada ya kuwa nina tepe zangu begani kwani nilijua sana namana ya kuzitumia; usiniulize niliztumiaje.


Mambo manne makubwa ninayokumbukia JKT ni:

(a) Ukakamavu: Hili ni jambo lililonisumbua sana baada ya kurudi uraiani kwa vile ukosefu wa shughuli za musuli ukawa unanifanya niwe nashambuliwa na muscle cramps za mara kwa mara. Nilipenda sana maisha ya ukakamavu.

(b) Ujasiri: Jambo ambalo huenda wengine hawakukiona ni lile la ujasiri. Wakati huo nilikuwa niko tayari kufanya lolote bila kuogopa. Kwa hiyo upambanai na ma MP halikuwa tatizo kubwa kabisa kwangu.

(c) Uzalendo: Nadhani jambo moja kubwa sana ambalo limeshatoweka kabisa ni kuhusu uzalendo. Mafunzo yale ya JKT yalikuwa yanastimulate sana vijana kuipenda nchi yao kama taifa moja. Ni sehemu pekee ambayo ilikuwa inakutanisha vijana wenye kutoka sehemu mbalimbali za nchi na wenye background tofauti na kuwa treated kama wamoja.

(d) Unafiki: Jambo pekee ambalo sikulipenda JKT ni unafiki. Kulikuwa na unafiki mwingi sana ukiambatana na nidhamu za woga. Nadhani jambo hili lilikuwa ni baya zaidi ya faida zote za JKT kwa vile kuna walioendelea na maisha hayo ya unafiki hata pale walipokuwa na madaraka makubwa kiserikali; kwa hiyo matendo yao ya hadharani yakabaki siyo reflection ya imani na matendo yao halisi wanapokuwa peke yao.
 
Ambacho sitasahau ni siku moja afande alijisaidia kwenye mlango wa hanga akatusingizia. Tukapewa adhabu ya kuchukua kila mtu kidogo kidogo. Akajitolea mmjo kuzoa lakini wakakataa. Kila mtu alishika mpaka ikaisha.

hilo tukio ni la mgambo.

mahanga ya "serengeti" kwa kumbukumbu zangu

lilikuwa ni tukio la aina yake
 
kunyanyua mikono juu wanapima nn kwenye kifua?

daktari wa jeshi ndo anajua alikuwa anaangalia nn, alaf hii ni kwa ajil ya air force command sasa sijui taratibu zao zinatofautiana na land force command..lkn jamaa walisema hawana complicated tastes km wengine
 
mkakati wa watarajiwa wa jwtz kupitishwa jkt ni ugoro wa watawala kutafuta kuingiza watu wao ndani ya jwtz. Jkt ni jeshi la kujenga taifa, liliwekwa kwa ajili ya wasio na ajira wakajiunge na kujifunza kujiajiri pamoja na kuwa wanajesi wa akiba wanaoweza kuitwa wakati wa dharura kutoa huduma za mwelekeo wa kijeshi. Waliokuwa wakilazimishwa kujiunga ni school leavers (x-formvi na x-university) kabla hawajaiingia katika ajira. Madhumuni ilikuwa kujenga nidhamu yao, na kweli walikuwa na nidhamu hata kazi zao zilionekana hivyo. Mafisadi walikuwepo wachache sana.

Hawa wajanja wanaopeleka watoto wao jkt miezi 4 halafu wanawafanya ndio wenye sifa ya kujiunga na jwtz ni waharibifu na matokeo yake mtayaona karibuni. Kuna "shamsi vuai nahodha" mwingine atajiuzulu tu kwa ugoro wa wanajeshi hao.

Halafu mnasema mnashangaa mawaziri sasa wanashindwa kuongoza wizara zao huku mkipeleka nyenzo zenyewe za kuwafanya washindwe kufanya kazi. Mama sitta alipeleka walimu bambuccha sasa masahibu yanamkuta kawambwa. Na kwa nini kawambwa na si majaliwa hapo pia unabaki kinywa wazi. Heri yake jakaya maana yeye wakijiuzulu anateua wengine, yeye aaaaaaaah!!!!!! Walioshindwa ni wao siyo yeye, yeye yuka amerika.

hivi hii ya kwenda jw hadi kupitia jkt ipo kisheria..lkn mbona naskia wengine wanaenda jw direct...hii imekaaje wakuu
 
mmeshindikana uraiani ndio mmekuja hapa kushindanana ! ................. hapa hafukuzwi mtu !

Hii ilikuwa mitaa ya afande Mlimba,Maduma, Masabo,Tyetyetye,Bahati,Bandeke.Mirudy,Chilumba aka Chiluba n.k..Kule kwenye shamba la dunia tumekula sana bisi kabla hujaja usawa wa gudulia.Week end mnachomokea Mirongo Inne kula konyagi mwitu na kuku wa kienyeji.Raha ajabu.

Umenikumbusha mesemo huu "...aroo kuruta uliye vaa griinvesti ya njano kuja hapa..." Heheheheeee green vest ya njano
 
Swala la JKT limekua compulsory kwa wale wote tunaosubiri nafasi za professionals za jeshi kwani ni lazima kwanza tu serve jkt for four months then ndio miezi sita ya officer cadet. Mimi naomba kwa wale ambao mmepitia huko (hususan walioapa juzi juzi) mtu habarishe nini cha ku expect huko, na since day 1 mlivowasili kambini ilikuaje etc. Hii itasaidia wengi kujiandaa psychologically and physically kwaajili ya mafunzo. Kwani huku mtaani speculations ni nyingi sana, wengine wanasema wiki sita za kwanza hamna kuvua mabuti wala kulala na rumours nyingine kama hizo hivyo kwa ambaye hatojali basi tungefurahi kama ata share na sisi hapa.
Regards,
Don Lucchese cc xir jyerphy
Matangazo ya kujiunga yanatoka lini?nilifuatilia kweli mwaka jana wakati nimemaliza chuo lakini sikufanikiwa napigiwa tu simu na wenzangu kuwa wameshapata kwa njia ya wakubwa,je kwa wale wa kufuata haki unapataje hiyo nafasi ya kujiunga JKT(taarifa nitapata wapi)?na pili ukiwa na target ya kwenda jwtz au intelligence inakuaje?
 
matangazo ya kujiunga yanatoka lini?nilifuatilia kweli mwaka jana wakati nimemaliza chuo lakini sikufanikiwa napigiwa tu simu na wenzangu kuwa wameshapata kwa njia ya wakubwa,je kwa wale wa kufuata haki unapataje hiyo nafasi ya kujiunga jkt(taarifa nitapata wapi)?na pili ukiwa na target ya kwenda jwtz au intelligence inakuaje?

mkuu israel, mbona nafasi za jkt wametangaza trh 30/11 pia hata za jw direct wametoa..fika ofisi ya mshauri wa mgambo wilaya uliyopo...
 
Ahsante mheshimiwa.vipi kuhusu target ya kuingia jwtz au intelligence inakuaje hasa ili kukamata hizo nafasi?na kama una professional ya IT and Network Engineering uhakika upo wa kupangiwa hiyo au ndio unaweza kutupwa kitengo kingine?
 
1984 Mlale JKT sitasahau afande 'Nguvu ya Nyani, wa Chale Coy! Hii ni operation NGUVU KAZI wakuu!!! Meja Mandwa alivyotutesa silaha ilipoibiwa! Afande Ngunduguru watu walivyokuwa wakimdhihaki kwa kumwita Mku....nduguru!!!! Namisi Chipole kwa masista na mihogo ya Embakasi na kule kijijini kwenye Ulanzi na kitimotoz! Namisi Disco la kuimba huku mmekaa na kupiga makofi, namisi Mustini wangu kiunoni, na misi Kujongo kwenda magagula! Bustani ya tomato, Cabbage nk! Kweli duniani maisha ni historia!!!
 
1984 Mlale JKT sitasahau afande 'Nguvu ya Nyani, wa Chale Coy! Hii ni operation NGUVU KAZI wakuu!!! Meja Mandwa alivyotutesa silaha ilipoibiwa! Afande Ngunduguru watu walivyokuwa wakimdhihaki kwa kumwita Mku....nduguru!!!! Namisi Chipole kwa masista na mihogo ya Embakasi na kule kijijini kwenye Ulanzi na kitimotoz! Namisi Disco la kuimba huku mmekaa na kupiga makofi, namisi Mustini wangu kiunoni, na misi Kujongo kwenda magagula! Bustani ya tomato, Cabbage nk! Kweli duniani maisha ni historia!!!

Hapa pia nawakumbuka marafiki zangu wengi sana wa C coy, Mbogo,Anthony Nyarubamba,Kezia Mpumilwa, Eliza Mlelwa,Eliza Mlay,Elizabet Amenye Mwaipungu, Saimon Limo,Gwakisa,na Alfred Mwakivvike, na wengine wengi wengi sana!!!!!!
 
Ruvu jkt operation vyama vingi .d coy namkumbuka afade sanga .ruta.kibuyu.matron zela.du nakumbuka matusi ya matron zela km kapitia chuo cha matusi kuna cku niliforge sahihi ya dr omar nikapigwa 45m ex drill kesho yake nika sepa
 
Back
Top Bottom