Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Hahaaa hayo matukio nimebaki nacheka tu, jeshi bana mchana kumetulia kazikazi tu za hapa na pale ila ikifika jioni duuh hilo doso lake + maovyoovyo hatari mpk midnight huhuuu
 
Magera namkumbuka mkuu.Kama sikosei OP yetu alikuwa Danger au Eagle Coy ..

Kuna koplo alikuwa anaitwa MAYAI.Huyu jamaa ukikutana nae tu ujue umeisha(hata kama huna kosa).

Kuna kamanda mwingine anaitwa KABEYA na BABU WA LOLIONDO..
Sir Major Mayai alikuwa Danger Coy kwa intake yetu, nikiwa chini ya usimamizi wake.

Kwa kifupi vipi unakumbuka yule mwanadada aliyekwenda kutangaza uwanja wa damu kuwa ametongozwa na afande halafu akamkataa?
 
Namkumbuka mkuu.Ni yule bonge sana akawa anasimulia mbele ya CO Kanole na watu wote tulikuwa kimya.Afande akampigia magoti yule dada na jamaa akaenda jera.Kwa kifupi yule jamaa alikosea ila pia jamaa alikuwa bonge la afande yani full amani tu.Ilikuwa ukikutana nae atakuita "Kurutu njoo haya shika pua,shika mdomo,shika kiuno" hahaha yani wkati anasema shika kiuno kabla mkono haujafika kiunoni anasema sheka pua...

Alikuwa akija kombania ataulia cheichei yuko wa kombania yuko wapi..

Je unamkumbuka yule dogo wa kike alitoroka jeshi halafu akarudishwa na baba yake? Unakumbuka tulikunja ngumi wakati anasimulia? Ilikuwa noma siku ile maana anahadirhia kama mtoto yani hatua moja moja kutoka kambini mpaka kwao.
 
Hahaaa mjinga sana yule alituumiza kweli kweli anasimulia polepole wakati watu tunaumia.

Kama ulikuwa danger coy unanifahamu Katika list ya madoja tatu bora nilikuwa sikosi!
 
Hahaaa mjinga sana yule alituumiza kweli kweli anasimulia polepole wakati watu tunaumia.

Kama ulikuwa danger coy unanifahamu Katika list ya madoja tatu bora nilikuwa sikosi!
Mimi nilikuwa BRAVO mkuu.Ila yule jamaa yenu sijui mnamwita CHACHA akiwahi nidaka na simu .

Ilikuwa ni shida mkuu.

Ile nyie Danger mlikuwa mnakula sana kazi.

Me nilikuwa Doja pale nyuma ya kombania yenu kwenye kuchoma takataka kila asubuhi sana .Kama kijiwe kile uliwahi kuja basi utanikumbuka maana ndio nilikuwa main talker .

MP Chaula jamaa alikuwa mwepesi kama mchina .
 
Hahaa kijiwe cha taka nimekikumbuka tumelala sana pale mkuu [emoji1].

Yule chacha hafai kabisa kuna kipindi alinipiga stick za mgongo acha kabisa yule jamaa mpaka kesho simpendi kabisa.
 
Rwamkoma jkt OP kikwete nilikua c coy chini ya Marwa! nawakumbuka sana marafiki zangu tuliokutana Rwamkoma kama kuna mtu kapita pale basi tukumbushane
Mzee bangu ukila mihogo Shamba dunia .anazingua kinomaa...
Bila kusahau kina jeneza...kenge... Walinishikilia kutoka resort nkaokolewa na sir mang'ombe
 
Mambo ya jeshini jamani hapana ,nakumbuka nilivyokua naambiwa kwenye mazoezi ya kwata 'Nanga huyu wa Demo kwa mwendo wa haraka mbele tembea basi nikianza kutembea watu wote hoi kwa kicheko sijui kwanini hahaaaa'
Kibangala hiki cha mananga mguuuuuu pandeee
 
Mzee bangu ukila mihogo Shamba dunia .anazingua kinomaa...
Bila kusahau kina jeneza...kenge... Walinishikilia kutoka resort nkaokolewa na sir mang'ombe
Kumbe na wewe ulikua pale mkuu?
 
Vijana Wa Matanga Mbushi na Ghadafi tunapaki magari yetu wapi humu.... Charlie Coy ya Demo CCP. Platoon 11. Nyambizi moja....
 
Mambo ya jeshini jamani hapana ,nakumbuka nilivyokua naambiwa kwenye mazoezi ya kwata 'Nanga huyu wa Demo kwa mwendo wa haraka mbele tembea basi nikianza kutembea watu wote hoi kwa kicheko sijui kwanini hahaaaa'
Wee inaonyesha ulikuwa unaanza kutanguliza mguu wa kulia ndo maana u nanga ulikuwa hauishi
 
OP ni moja tu,inayoitwa OP MKAPA ilikuwa ruvu na makutopora dodoma hiyo mingine ni mifano tu2001/02
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…