Baada ya kuuona uzi huu, ghafla nimemkumbuka Yesu!
Sio Yesu wa Nazareth, hapana. Ni kijana mmoja tu wa kichaga aliefanya muujiza akazawadiwa hilo jina!
832 KJ Danger Coy, OP miaka 50 ya jkt.
Tuliharibu kazi tukaanza kupewa doso mpaka mida ya saa nane usiku.
Ndipo huyu mshkaji wetu wa kichaga akaamua kutoka nduki kuelekea kusikojulikana.
Makamanda walikuepo arround wakamuunganishia, na wakamkamata.
Kilichofuatia ni kwamba wengine wote tuliruhusiwa kwenda kulala, jamaa ndo akala kazi mpaka asubuhi. Ikabidi apewe jina la Yesu kwa kujitoa mhanga kuokoa kombania nzima!
Pale Muhuga mess, afande aliweka simu juu ya TV then akakaa kuangalia mpira mbele kabisa ya TV. Kuruti waliiba simu na hakumuona mwizi. Afande alibaki anacheka!
Nakumbuka tulivyokua tunatoroka saa kumi za usiku kuja dar, na kurudi kambini usiku muda wa kuhesabiwa tumetimia.
Yes, nakumbuka totoz za kiskazini zilivyokua za moto.
Namkumbuka msabato aliegoma kufanya kazi siku ya sabato. Adhabu zote zilifeli kwa huyu jamaa, hadi getini kofia nyekundu walimshindwa. Good thing ni kwamba siku nyingine alikua anapiga kazi kweli kweli, shambani anabeba ndoo mbili kwa mpigo.
Nakumbuka mshkaji wangu alivyoibiwa simu akiwa anaichaji na ameishikilia. Alisinzia, kushtuka akajikuta ameshikilia chaja pekee!
Naikumbuka route match kilomita 30 kuitafuta Bagamoyo, achilia mbali mbio za kilomita 16 kila siku kwenda shamba na kutafuta kuponi.
Namkumbuka mshkaji kibonge aliekuja na mwili kama wa Le mutuzi akarudi na mwili kama wa joti.
Na mkumbuka kamanda Bafeni, baba hansi na service man maneno!
Mwisho nakumbuka nilivyopiga kwata kikakamavu mbele ya mkuu wa majeshi wa kipindi hicho General Mwamunyange.
Jeshi ni noma wakuu!