Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Daaah nimemmiss sana maisha ya 841kj, kipindi hicho unakutana na Captain Moshi hakuna, ukizubaa ukamkuta mesi mda wa chai basi mnakimbia Hadi uwanja wa damu mnakuja kunywa chai.

Kitu pekee nlichokuwa cpend ni kukesha usiku Hadi saa 6 7 na kuamshwa saa 9 na Afande Madoso.

Ila kwenye mazoezi na mabio nlikuwa mstari wa mbele sana na ni michezo nayo ipenda
Ulikuaga kombania ipi? [emoji3]
 
Mabio jamaniii mamaee kuna ilee route za jioni mmetoka kula zilikuwa zinakera sana...!! Toka kambini pitia Rest house mpaka kwa Msange na kurudi...[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Bila kusahau Yombo, mbola kwa mshuhuma n.k
 
Huyu anaongelea hii ya watoto.
JKT ilikua miaka ya 88 kurudi chini.
Enzi za afande Sanga, afande Mlay afande Mtono. Meja Jenerali Mkisi na tabia zake za ajabu.
Kwenye mbuzi alikua anakula Figo tuh. Sasa niambie Figo za mbuzi ngapi anaweza kushiba Jenerali?
JKT ya zile kambi nane.
Oljoro
Mgambo
Makutpora
Msange
Bulombora
Mafinga
Ruvu
Mlale.
Enzi zile kila kitu unakikuta kule kuanzia
Bukta
Green vest
Kombati
Buti
Mess tin Tena mbili
Blankerti
Yaani wewe unakwenda na mwili tu.
Bila kusahau ulikuwa unapewa ''warrant'' ili utumie kusafiri kwenda, na pia wakati wa kurudi.
 
Kuna ile kazi ya kufata mbolea kwa msukuma duuh[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]ilikua inaniboa sana japo tulikua tukirud tunapitia malimao porini kwa ajili ya mchuzi wa nyama na kupaka kwenye kipara ukinyoa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mabio ya asubui mabio ya asubui mabio ya asubui......unalala saa 7 huko hoi hafu saa kumi li afande linakuja na maji linamwaga tu ovyo ovyo
 
Mwendo wa kukwepa ndege ile ni balaa yuko afande nusu Mungu semi God huyo ni hatari aise. Usiende JKT na fomyula yako ya kuishi utashinndwa maisha utakayoyakuta kule ndio yatakutengenezea namna gani ushi
 
Pamoja man.

mnabahati mlikua hampangiwi maafande wanaa kama wenzenu wa Charlie, Danger na Eagle

Dakika sifuri tu watu washapigwa nua, wamesimika, mara wana-roll [emoji3]
Mwaka gani hiyo mkuu mie 2017
 
Mwaka gani hiyo mkuu mie 2017

Jasho mzinguaji [emoji3], commando kipingu wa Charlie coy unamkumbuka? Madoso miyeyusho? Koplo Rambo wa Danger? Mkorofi daily analala mahabusu, matron kikosi je?
[emoji3]

Capt Moshi miyeyusho sana
 
Bila kusahau Yombo, mbola kwa mshuhuma n.k
Mkuu kweli ulikuwa msange Hata Mimi nilikuwa huko pande hizo nazijua vizuri Kwa msukuma...Kuna Ile inshu ya kwenda kuzima moto Mimi nilikuwa eagle Kwa sameja Michael Kasembe na ofisa cardate Bakari
 
Mi niliamua kufanya kila niambiwacho kwa 100%.

Hakuna kutegea, kujificha wala nini.
Na siku nyingine nikimaliza mraba wangu mapema namsaidia yeyote yule.

Kila tabu au adha niliifanya kuwa fursa na raha.

Hiyo kanuni ninaitumia huku uraiani pia hakuna kulialia.
inashort ulikuwa unajila sio
 
Mkuu hili shamba dunia liko maeneo gani?? mimi nilikuwa nimesahau IDETERO, kuna mkuu hapo juu amenikumbusha.
Halafu kuna CHANGARAWE (Kuna lijengo kubwaaa sijui ni hoteli, tulisota sana kipindi linajengwa
Hilo lihoteli umesotea linaitwa RECREATION tunaendaga kupiga vyombo na kuruka majoka kila weekend
 
Back
Top Bottom