Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,584
- 6,136
Hawa watu wa Nutrition ukiwasikiliza waweza kupata ugonjwa wa moyo.
Nilishaongea na jamaa mmoja mwenye PhD kuhusu ulaji wa vyakula na vinywaji na hasa COLA na akasema kuwa hakuna kinywaji hatari duniani kama Cola. Ila hili halisemwi na cha ajabu ni kuwa wakati fulani walifanya kikao kikubwa cha kimataifa na aliyedhamini kikao ni COCACOLA (Mchawi mpe mtoto amlee). Katika kikao hicho, kwamba Cocacola nayo ni hatari, hakuna hata aliyethubutu kusema.
Hii inanikumbusha pia ubishi mkali kuhusu Bio-Diesel kwenye magari. Wanaotaka iwepo wanasema ni nzuri sana, inapunguza CO2 na inatunza uharibifu wa Engine. Wanaopinga wanasema "inaharibu sana Engine na ni ghali."
Ukiangalia ukweli, kila kitu mwilini kina madhara. Watakuambia hasara ya Beers, na pombe kwa ujumla. Watakuambia hasara ya kula chumvi, sukari,nk. Wasabato watakuambia hasara ya kunywa CHAI na ndiyo maana hawanywi. Utaambiwa hasara ya kahawa, Cocoa, nk. Utaambiwa hatari ya karanga na mafuta yake, Alizeti, ufuta nk Watakuambia hatari ya kula wali (Mchele) ulivyo hatari sana na ndiyo maana Wa-Asia wana miguu imepinda.
Sasa sijui ule nini? Ukiwasiliza sana hao watu ni kweli utakufa NJAA. Ni lazima ujuwe kuji-Balance. Anyway, ntamuandikia huyu jamaa wa NUTRITION na nikipata jibu basi ntawajulisheni.