Je Unakunywa Juice za Mixed Fruits?...

Je Unakunywa Juice za Mixed Fruits?...

Hawa watu wa Nutrition ukiwasikiliza waweza kupata ugonjwa wa moyo.

Nilishaongea na jamaa mmoja mwenye PhD kuhusu ulaji wa vyakula na vinywaji na hasa COLA na akasema kuwa hakuna kinywaji hatari duniani kama Cola. Ila hili halisemwi na cha ajabu ni kuwa wakati fulani walifanya kikao kikubwa cha kimataifa na aliyedhamini kikao ni COCACOLA (Mchawi mpe mtoto amlee). Katika kikao hicho, kwamba Cocacola nayo ni hatari, hakuna hata aliyethubutu kusema.

Hii inanikumbusha pia ubishi mkali kuhusu Bio-Diesel kwenye magari. Wanaotaka iwepo wanasema ni nzuri sana, inapunguza CO2 na inatunza uharibifu wa Engine. Wanaopinga wanasema "inaharibu sana Engine na ni ghali."

Ukiangalia ukweli, kila kitu mwilini kina madhara. Watakuambia hasara ya Beers, na pombe kwa ujumla. Watakuambia hasara ya kula chumvi, sukari,nk. Wasabato watakuambia hasara ya kunywa CHAI na ndiyo maana hawanywi. Utaambiwa hasara ya kahawa, Cocoa, nk. Utaambiwa hatari ya karanga na mafuta yake, Alizeti, ufuta nk Watakuambia hatari ya kula wali (Mchele) ulivyo hatari sana na ndiyo maana Wa-Asia wana miguu imepinda.

Sasa sijui ule nini? Ukiwasiliza sana hao watu ni kweli utakufa NJAA. Ni lazima ujuwe kuji-Balance. Anyway, ntamuandikia huyu jamaa wa NUTRITION na nikipata jibu basi ntawajulisheni.
 
...ni heri yetu sisi tunaokula neno tu...binadam hataishi kwa mkate peke yake...
 
Juzi tu tulijulishwa juu ya hiki kinywaji MIRACLE JUICE (Carrot, Beet Roor and Apple).

juice.bmp


From: Tasty Appetite: Miracle Drink : Carrot, Beet Root and Apple:
 
Kwa mujibu wa baiolojia na sayansi ya kilimo, kuna ukweli fulani kwenye statement ya hao jamaa, ila with exceptions. Nafafanua.

  1. Matunda kama matufaa (najua unashangaa hili jina, ni Kiswahili), machungwa, Mananasi na maembe yana citric tinndikali nyingi zenye viwango vya kutofautiana. Yakichanganywa hayo niliyoyataja na kufanya juisi basi lazima kuwe na madhara, yanaweza yasiwe ya muda huo huo (slow death), hasa vidonda vya tumbo. Waliosoma kilimo na baiolojia kidogo wanajua hili.
  2. Tunda kama parachichi ambalo halina tindikali, ila lina mafuta, likichanganywa na ndizi mbivu au tikiti ama mojawapo ya matunda ya hapo juu na kutengeneza juisi kunakuwa hakuna madhara, kwa sababu 'Chemical composition' za mchanganyiko huu ni anuwai. Hii ndio exception ambayo nimeitaja kwenye utangulizi, kwa hiyo ni vema kuzingatia uchaguzi wa matunda wakati wa kusaga juisi ama wakati wa kula matunda yenyewe.
  3. Ni kweli kwamba yale matunda mchanganyiko yanayouzwa njiani ni sahani ya kifo, hasa unapochanganyiwa matunda ya kundi namba moja hapo juu (maembe, matufaa, mananasi au machungwa).
Nawasilisha

Waheshimiwa..., msishtuke wala kutishika na maneno ya huyo jamaa.!
Kwanza hajatoa scientific evidance..., hajasema ni mchanganyiko wa matunda ya aina gani ndio yapelekea kuongezeka kwa kiwango cha uric acid mwilini...! Kwa ujumla jamaa anaelekea ni mfanya biashara zaidi.!

Wengi wetu tunaelewa umuhimu wa kula matunda ya aina mbalimbali kama chanzo cha virutubisho vya aina mbali mbali..., mfano vitamins (aina mbali mbali), madini (aina mbali mbali), fibers (insoluble & soluble), maji na chemical za aina mbali mbali (bioactive compounds) zinazosaidia mwili kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama cancer, kisukari, magonjwa ya moyo n.k. Hivyo ni muhimu kula matunda mchanganyiko iwe ni ktk mfumo wa juice au mazima ili kuweza kupata virutubisho vingi iwezekanavyo.

Pamoja na kwamba baadhi ya matunda na mboga za majani zina sumu..., kuathirika na sumu husika pia kunahitaji ule kiwango (dose) ya kutosha.., hivyo wengi wetu huwa hatuli kiwango cha sumu cha kuweza kuathiri afya zetu..., japo mf., baadhi ya aina za uyoga huitaji kiwango kikubwa cha sumu kuathirika kiafya na hata kupelekea kifo.

Rejea chapisho kwenye wavuti hii; Lishe Bora: Mboga Za Majani Na Matunda | Mwakilishi.com

Nami naelekea chimboni kutafuta ukweli wa kuhusu uhusiano wa kiwango cha uric acid na juice ya matunda mchanganyiko.
Nawakilisha kama mtaalamu (nguli) wa chakula (chakula-afya na chakula-dawa).
Scientific arguments!
Hapa sasa tunaelekea kunako majibu.
On glance at least sasa tuanze kukubali kuwa wale waganga wana ukweli fulani at the end of a tunnel! Hii inatokana na arguments za hirorobert, Idimi na Himawari hapo juu!
Bila shaka Himawari ukienda chimboni utaweza kutuwekea hapa japo tovuti au kijarida cha maelezo.
 
Last edited by a moderator:
Hivi PakaJimmy unawezaje kuunganisha thread za watu zaidi ya mmoja kufanya kama ulivofanya hapo kwenye hii?nifundishe tafazali!
Kusema ukweli mimi mwenyewe nilishtuka sana, maana kawaida mchana huwa nakula matunda tu, na huwa ni hayo ya mixed fruits...on serious note niko njipanda ukizingatia saa 6 ndo hii hapa!....huh!

Inabidi sasa kila mtu aingie chimbo kujua ukweli ama uongo wa jambo hili, maana vinginevyo wajinga ndio waliwao.
 
Last edited by a moderator:
usile mkuu maana unapokula ndio unajiweka karibu na kifo, bacteria wanazaliwa kwenye uwepo wa maji maji na vyakula..... Tena wengne ni hatari... Vyakula vingi vinawekwa mbolea zenye sumu na hata yale madawa ya kuhifadhia vyakula nayo sumu. Hebu fikiria mashine za kusaga huwa zinaisha, unafkri vyuma vinaenda wapi kama havijimix kwenye unga!
Usile mkuu, kama unajipenda say no to misosi.

Hii ni kali. Usipokula manake si ndo kifo jamani.
 
Msiwabishie hao Jamaa, walicho ongea ni ukweli mtupu, sasa watu wanapinga tu , Pinga kwa evidenci, mimi ninacho kitabi kinahayo maelezo, na nendeni mka google mtapata story zaidi,
 
SASAAAA matunda ni sumu, nafaka ni sumu, mbogamboga ni sumu, pombe ni sumu, dawa za kututibu ni sumu, hata maziwa ya kupooza sumu ni sumu. TUSIPOKULA PIA tutakufanjaa ni sumu .Huenda hata hii comment nayo sumu!.Na hiyo sumu pia nayo ni sumu.
 
Wakubwa,

Jana nilikuwa nasikiliza RFA kulikuwa na kipindi cha Afya, kuna jamaa wa dizaini kama ya Dr Ndodi, wanapima magonjwa kwa kutumia mashine inayoitwa Quantum ambayo ina uwezo wa kuainisha magonjwa mengi yanayomsumbua mtu, kwa kushika handle fulani kama 'mouse' inayoingia kwenye computer hiyo. Baada ya hapo wanauza dawa za aina ya vyakula ili kutibu magonjwa yaliyoonekana kwa mgonjwa.

Kilichonishitua ni kwamba walifika mahala wakawa wanataja vitu vinavyopelekea mtu kuwa na Uric acid nyingi mwilini, wakasema kuwa ulaji wa matunda mchanganyiko KWA MUDA MMOJA ni source kubwa na mbaya sana ya Uric acid!

Walisema wale wauzaji wa matunda wanaokata chungwa, embe, papai, pesheni, avocado, tango, ndizi etc, na kukuzia kwenye sahani waogope kama ukoma, maana wanakuletea sahani ya kifo.
Walieleza kuwa kinachotakiwa ni kula tunda la aina moja lililopo kwenye msimu, basi na si kula matunda mchanganyiko.

Najiuliza, kuna packed juice za mixed fruit, aidha huko majumbani tunablend na kunywa juice za kuchanganya matunda, je ndio tunajimaliza?
Mkuu hawa jamaa ni waongo sana wanatuona Wabongo wengi hatupendi kusoma na ni wepesi wa kufata kila kitu kwa urahisi iwapo kitakuwa kimetangazwa publicly kama hivo kwenye tv.
Kwa uchache wa elimu hiyo kuhusu uric acid ni compound inayozalishwa kutokana na metabolic breakdown ya substance nyingine iitwayo purine ambayo ni sehemu ya tissue ya kiumbe hai,hivyo wanavyozungumzia kuwa matunda mixer uongeza kiasi kikubwa cha uric acid hilo kwa kweli ni Tango pori kwani ni kweli kuna vyakula vingi vyenye kiasi kikubwa cha source ya uric acid navyo mainly ni vitu vya asili ya nyama nyama kama vile maini,figo na other meat extract.
hata hivyo mwili umeumbwa kuweza kucontrol kiasi cha uric acid ambacho kinatakiwa.Uric acid inaweza kuzidi kama tu figo alifanyi kazi sawa au kiasi kinachozalishwa mwilini ni kikubwa sana kutokana na uwepo wa kiasi kikubwa cha purine katika chakula,sasa basi kwa kuwa purine ina harufu nzuri kama ya matunda hivyo wanadhani matunda yana kiasi kikubwa cha purine kitu ambacho si sahihi.
heri wangetutisha na uyoga,spinach au caulflower kuliko matunda meen........
so tusiogope matunda mix bana kama maandalizi yake yako powah.

 
Ukisikia Madokta feki au wanatoka shule za kata ujue ndio hao, Matunda mixed tangu lini yanasababisha kifo? Wendawazimu hao madokta. Haki ya nani hii nchi inatatizo kubwa sana sio la uongozi tu hata madokta, walimu, wafanyakazi na raia nao wapo wapo kusikilizia wanadanganywa na kila mtu anayepata nafasi ya kuwadanganya. Watanzania tuna safari ndefu ya kuamka kwenye huu usingizi mzito sijui taifa limerogwa nani.
 
Ndo maana Mungu hajakosea kila tunda lina msimu wake na tofauti na lingine.
 
nshasikia kitu kama hii kwa docta fulani hivi....kuna ukweli ndani yake...tusubiri MziziMkavu ,Riwa na wengine wakuje kutupa lecture hapa....
 
Last edited by a moderator:
Ndo maana Mungu hajakosea kila tunda lina msimu wake na tofauti na lingine.
Kuna point tamu sana hapa, lakini mkuu hutaki kuireveal.
Unamaanisha Mungu alipoweka misimu mbalimbali ya matunda alikuwa anazuia watu kujilia matunda kwa kuchanganya aina saba kwenye sahani moja, sio?
 
me naombeni msaada wakuu....huwa natengeneza juice ya mchanganyiko wa tikiti,passion,embe,tango na nanasi, nipo salama kweli?
 
Mkuu hawa jamaa ni waongo sana wanatuona Wabongo wengi hatupendi kusoma na ni wepesi wa kufata kila kitu kwa urahisi iwapo kitakuwa kimetangazwa publicly kama hivo kwenye tv.
Kwa uchache wa elimu hiyo kuhusu uric acid ni compound inayozalishwa kutokana na metabolic breakdown ya substance nyingine iitwayo purine ambayo ni sehemu ya tissue ya kiumbe hai,hivyo wanavyozungumzia kuwa matunda mixer uongeza kiasi kikubwa cha uric acid hilo kwa kweli ni Tango pori kwani ni kweli kuna vyakula vingi vyenye kiasi kikubwa cha source ya uric acid navyo mainly ni vitu vya asili ya nyama nyama kama vile maini,figo na other meat extract.
hata hivyo mwili umeumbwa kuweza kucontrol kiasi cha uric acid ambacho kinatakiwa.Uric acid inaweza kuzidi kama tu figo alifanyi kazi sawa au kiasi kinachozalishwa mwilini ni kikubwa sana kutokana na uwepo wa kiasi kikubwa cha purine katika chakula,sasa basi kwa kuwa purine ina harufu nzuri kama ya matunda hivyo wanadhani matunda yana kiasi kikubwa cha purine kitu ambacho si sahihi.
heri wangetutisha na uyoga,spinach au caulflower kuliko matunda meen........
so tusiogope matunda mix bana kama maandalizi yake yako powah.


Tena spinach mi nafa
 
Uric acid ni end product ya digestion ya protein, sasa kula muda mwingi vyakula vya protein kwa ujumla wake ndivyo vinavyo sababisha uwe na uric acid nyingi. Lakini matumizi ya alcohol, antipain like paracetamol are the most causative of hyperuricemia. Na most protein ni zile first class kama meat, beans etc. Kwa msaada Google HYPERURICEMIA utapata majibu achanani na waganga njaa hao. Na ndiyo maana magonjwa ya gout ni common kwa wanywa pombe na wale wanaokula sana red meat.
 
Tena spinach mi nafa
Usiogope hivi vitu bana havina madhara kwa wabongo,we umemsikia nani ktk umri wote ulioishi kafa kwa ajiri ya axcess of uric acid bana..lol!.....hiyo micompee ya wazungu sisi hata hatuna habariiiiiiiiiiiiiii

 
me naombeni msaada wakuu....huwa natengeneza juice ya mchanganyiko wa tikiti,passion,embe,tango na nanasi, nipo salama kweli?
Hapo kinachoharibu ni pasheni na nanasi.
Ukitaka kusalimika tengeneza juisi ya pesheni, nanasi na chungwa pekee, usiweke humo ndizi na embe tena.

Kwa juis yako hiyo unapata glasi ya kifo.
 
Back
Top Bottom