Umuhirindahu
JF-Expert Member
- Feb 2, 2014
- 349
- 170
Wivu wake ni kwa upande wa "me" na upande wa "ke" hawana wivu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ila wewe ni jasiri,,,safi sanaaaaMkuu,hiyo haina sifa ya kuingia kwenye guiness book of records ila ipo tu kwenye record ya maisha yangu kilichonisaidia siku ile ni kwamba sikujua napambana na mnyama gani kwa hiyo sikuwa na hofu pili ni ule mpini mfupi wa mudu niliweza kuudhibiti na kuutumia barabara na isitoshe nilikuwa na taa mkononi pengine mwanga wa taa ulikuwa unamchanganya na mwisho kabisa nilikwa nimefunga taulo kiunoni labda kalidhani mimi ni ke vinginevyo kangejua mimi ni me ilikuwa rahisi kuondoka na ikulu yagu
Safi sana ila ile style yake ya kubong'oa kule kwenye haja kubwa kama mtego wa kumnasa kuku na kuku akidonoa tu hubanwa kwa misuli mikali sana huwa inanifanya nimuone huyu kiumbe kama ana vile vitabia vya mombasaView attachment 342896 View attachment 342897 View attachment 342899
Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani. Chakula chake kikubwa ni asali,yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula. Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma hakuna chochote kinatokea
Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike
Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke,mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake(ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii.
Nyegere ndio mmoja kati ya "fearless animal" duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda,anasaidiwa na ngozi yake ngumu na kucha zake, awapo katika hatari ya kushambuliwa hukakamaa na ngozi yake kuwa ngumu kama "defensive mechanism" yake.
Kuna makabila ambayo waganga wa kienyeji hutumia mchanganyiko wa Nyegere kutengenezea limbwata,Yaani wamama huchukua dawa hiyo kuwawekea waume zao ili wawe na "upendo" wa Nyegere.
Wivu wa Nyegere hufanya awachukie sana binadamu wanaume,mwanaume ukiwa porini ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano, huona wivu kuwa utamtamani jike,hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.
Nyegere hula nyoka wa aina yoyote,ana sumu kali ambayo akimng'ata nyoka wa aina yoyote haponi.
Ogopa sana kukutana na mnyama mwenye wivu Nyegere...
Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja,akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya.
Si jasiri ki hivyo ila kwa kutojua napambana na mnyama gani sikuwa na hofuIla wewe ni jasiri,,,safi sanaaaa
[emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] hii mpya tena!Safi sana ila ile style yake ya kubong'oa kule kwenye haja kubwa kama mtego wa kumnasa kuku na kuku akidonoa tu hubanwa kwa misuli mikali sana huwa inanifanya nimuone huyu kiumbe kama ana vile vitabia vya mombasa
Kuna documentary yake inaitwa SNAKE KILLERS;THE HONEY BADGERS OF KALAHARI..imerekodiwa na National Geographical Special.Zinapatikana hata kwenye maduka makubwa ya movie,Ukimaliza kuiangalia utamheshimu milele.Mwanaume wa shoka huyu.Basi atakuwa kiumbe cha kipekee sana
mmmh
I believe hii documentary nimeiona mkuu.. kama huyu Nyegere ndio anaitwa HONEY BADGER basi nishaona baadhi ya characteristics zake. Sema hiyo ya wivu kwa jike lake ndio imeniacha mdomo wazi..Kuna documentary yake inaitwa SNAKE KILLER;THE HONEY BADGER OF KALAHARI..imerekodiwa na National Geographical.Ukimaliza kuiona utamheshimu milele
Duh! Ha ha ha!
Asante kwa maarifa haya ... Ngoja ni mgoogle nimjue zaidi.
Duh! Nyegere bhana.
Hivi haka ndo kale kajamaa kabishi kwenye mkanda wa BUSH MEN?!!
Kanabong'oa...Kuku anagusa tu kanae!!Hatari sana..ila hii sio ile "Kubong'oa" kwa Mzee Mwanakijiji[emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] hii mpya tena!
Loooh..
Kwahiyo ni kweupe hadi kuku adonoe?
...acheni ligi za kipimbi!....imeruhusiwa avatar kufanana,sio id...yani mtu akitaka kuweka avatar afuatilie members wote kujua kama hakuna anaeitumia?kuweka avatar ya tupac sio shida, ila kuweka avatar ileile exactly kama aliyoweka mwenzako, unakuwa umekosa nyingine?
na avatar zina maana ndio maana jf wakaweka sehemu ya avatar na id, la sivyo wasingeweka
Huyu sio mnyama anaitwa kicheche kweli? au ndio nyegere jina lingine?Kanabong'oa...Kuku anagusa tu kanae!!Hatari sana..ila hii sio ile "Kubong'oa" kwa Mzee Mwanakijiji
Ni hatari Nifah...huyu mnyama msikie tu,yaani kana hasira sana asee,na ni kabishi hatariiiii....Babu alituambia ili kafe ni lazima upige rungu kwenye fuvu kichwani,ukipiga huko mgongoni ni kama unajisumbua tu,sbb kenyewe kana uweze wa kujitunisha rungu ukipiga linadunda kama mpira tu
Maisha ya Kijijini kuna mambo mengi ya kujifunza sana,huu u-mjini kuna mambo mengi tunakosa,kama panya tu mwanaume wa Dsm mpaka asafiri K'koo kununua sumu ya kumuua wakati bush mtu anamminya tu panya na mkono,huyo nyegere akija Sinza si wanaume wote nyeti zitakwanguliwa?Ha ha ha ha ha ha ha
Wacha kabisa habari ya nyegere...RIP my Babu...Alitufundisha mengi juu ya maisha ya wanyama wakali na jinsi ya kukabiliana nao
Mkuu kwa uelewa wangu na niwajuavyo vicheche ni wadogo tofauti na hawa Nyegere.Huyu sio mnyama anaitwa kicheche kweli? au ndio nyegere jina lingine?
Mhhhhhh mkuu hiyo sentesi yako ya mwisho imeniacha na maswali lukuki.Kanabong'oa...Kuku anagusa tu kanae!!Hatari sana..ila hii sio ile "Kubong'oa" kwa Mzee Mwanakijiji
Umemchanganya...anaebong'oa ni kichecheSafi sana ila ile style yake ya kubong'oa kule kwenye haja kubwa kama mtego wa kumnasa kuku na kuku akidonoa tu hubanwa kwa misuli mikali sana huwa inanifanya nimuone huyu kiumbe kama ana vile vitabia vya mombasa
Ooh ok ok asante kwa ufafanuziUmemchanganya...anaebong'oa ni kicheche
kuweka avatar kama ya mwenzako out of millions of avatars ndio upimbi haswa...acheni ligi za kipimbi!....imeruhusiwa avatar kufanana,sio id...yani mtu akitaka kuweka avatar afuatilie members wote kujua kama hakuna anaeitumia?
Nonsense!
Halafu vicheche vinakuwa kundi na huwa vinasimamia miguu ya nyuma na vinainua miguu ya mbele navyo vinamikwara hatar ukiwa mwogamwoga kama mwanaume wa dsm vinakuchenjiaMkuu kwa uelewa wangu na niwajuavyo vicheche ni wadogo tofauti na hawa Nyegere.
Na wale huwashambulia kuku shingoni na kuwanyonya damu,hawa ndio kama hivyo wanabong'oa.
Ila kuna some characters wanafanana,kama hiyo kutokufa haraka.....
Vicheche wana roho ngumu sana.
Nakumbuka nilipokuwa mdogo kijijini kwa bibi niliona wakipigwa sana,ila walichukua muda mrefu sana kufa.