Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

ivyne_25 naona umeleta tena hii mada kutoka huko WhatsApp na Facebook
Ukajuwa unaleta kitu kipya kutoka Fb,kumbe hapa jamaa barafu alishaleta mzigo mzima mzima
Huko Fb mmehariri kidogo tu mkairudisha...Ukiona mada yenye akili huko Fb na WhatsApp ujuwe imeanzia hapa hapa

Mimi ndio kwanza naiona leo! Mwache alete mkuu. Kwani tatizo ni nini? Au jf imejaa.
 
MJUE NYEGERE Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye
wivu sana hapa duniani. Chakula chake
kikubwa ni asali,yeye hupanda juu ya
mzinga wa asali na kuujambia, baada ya
mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye
kupakua asali na masega yake na kula. Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi
hata nyuki akimuuma hakuna chochote
kinatokea Nyegere ni mnyama mwenye wivu na
mapenzi makubwa sana kwa jike lake,
hutembea nyuma ya jike huku akiwa
ameziba sehemu za siri za jike, hata jani
tu likiigusa sehemu ya siri ya jike
litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani
litakuwa "limefaidi utamu" wa jike Nyegere anaweza kununua ugomvi
mpaka kijiji cha sita, Warina asali ndio
waathirika wakubwa wa hasira za
Nyegere,anaweza kuujambia mzinga
akala kidogo asali na kupeleka kwa
mke,mrina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu
ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani,
na akifika anavunja mlango na kuingia
ndani na kumvamia mwizi wa asali yake
(ukizingatia milango ya vijijini si imara).
Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii na huyu mnyama. Nyegere ndio mmoja kati ya "fearless
animal" duniani, huweza kuwakabili
Simba na Chui zaidi ya mmoja na
kuwashinda,anasaidiwa na ngozi yake
ngumu na kucha zake, awapo katika
hatari ya kushambuliwa hukakamaa na ngozi yake kuwa ngumu kama "defensive
mechanism" yake. Kuna makabila ambayo waganga wa
kienyeji hutumia mchanganyiko wa
Nyegere kutengenezea limbwata,Yaani
wamama huchukua dawa hiyo
kuwawekea waume zao ili wawe na
"upendo" wa Nyegere. Wivu wa Nyegere hufanya awachukie
sana binadamu wanaume,mwanaume
ukiwa porini ukakutana na Nyegere
akiwa na jike lake jiandae kupata kibano,
huona wivu kuwa utamtamani jike,hivyo
hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa
jeuri ya kumtamani jike lake. Nyegere hula nyoka wa aina yoyote,ana
sumu kali ambayo akimng'ata nyoka wa
aina yoyote haponi. Ogopa sana kukutana na mnyama
mwenye wivu Nyegere... Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya
kilomita saba usiku kwa usiku anafuata
harufu ya mtu aliyerina mzinga wa asali
aliyoijambia, alipofika akavunja mlango
na kukuta wamelala watu wanne kwenye
mkeka mmoja,akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi
porini kimya kimya.
Sifa ya mwisho aliyonayo ni kwamba
kama kakufata nyumbani kwako
ukampiga na kumzidi maarifa, atakumbia
na kuondoka maeneo hayo, lakini zake ukijua lazima atarudi tena hata kwa
kupitia juu ya Paa kuja ku revenge
ugomvi upya hadi ahakikishe
kakushughulikia hasawa. Huyo ndie mnyama Nyegere
 
Tusisaahu kwamba nyegere ndio mnyama anaeshikilia rekodi ya dunia ya Guinness kuwa mnyama asieogopa chochote chini ya jua. The most fearless animal on earth.

Ngozi yake ni ngumu kiasi kwamba risasi haiwezi kupenya kirahisi.

Nyoka mwenye Simu Kali zaidi black mamba anatakiwa amng'ate zaidi ya mara 10 huyu nyegere ili azimie sekunde kadhaa na akiamka anakuwa na nguvu na hasira kubwa.

Nani ni nyegere katika maantiki ya fumbo lako mkuu?
 
Tusisaahu kwamba nyegere ndio mnyama anaeshikilia rekodi ya dunia ya Guinness kuwa mnyama asieogopa chochote chini ya jua. The most fearless animal on earth.

Ngozi yake ni humu kiasi kwamba risasi haiwezi kupenya.

Nyoka mwenye Simu Kali zaidi black mamba anatakiwa amng'ate Mara 10 huyu njema ili azimie sekunde kadhaa na akiamka anakuwa na nguvu na hasira kubwa.
asante sana mkuu nilikuwa sifahamu kuhusu hilo.hakika ni hatari na adimu kuonekana
 
Tusisaahu kwamba nyegere ndio mnyama anaeshikilia rekodi ya dunia ya Guinness kuwa mnyama asieogopa chochote chini ya jua. The most fearless animal on earth.

Ngozi yake ni humu kiasi kwamba risasi haiwezi kupenya.

Nyoka mwenye Simu Kali zaidi black mamba anatakiwa amng'ate zaidi ya mara 10 huyu nyegere ili azimie sekunde kadhaa na akiamka anakuwa na nguvu na hasira kubwa.

Nani ni nyegere katika maantiki ya fumbo lako mkuu?
Mkuu risasi haiwezi kupenya? hapana si kweli, risasi ni mziki mwingine aisee.
Tabia ya risasi ni kupenya popote penye ugumu na haiwezi kupenya Sehemu laini, ndo maana haiwezi kupenya gunia la mchanga kwa sababu ni laini,lakini kwenye mwamba mgumu risasi hupenya.
 
Mkuu risasi haiwezi kupenya? hapana si kweli, risasi ni mziki mwingine aisee.
Tabia ya risasi ni kupenya popote penye ugumu na haiwezi kupenya Sehemu laini, ndo maana haiwezi kupenya gunia la mchanga kwa sababu ni laini,lakini kwenye mwamba mgumu risasi hupenya.
Tulipaswa kujiuliza kwanini haipenyi kwenye ngozi ya nyegere? Sababu ni nini ulaini wake au?

Maana wakulima wenye magobore ndio wanajua uimara wa ngozi yake. Anauliwa kilaini sana kwa kupigwa na kitu kizito sehemu maalumu kichwani.
 
Kiufupi huyu mdudu ni mtemi , sasa mkuu nikiunga dots napata shida kuelewa uzi umemlenga nani hapa kwa Nyerere /Tanzania
 
Haka ka mnyama kana ka hatar sana angalia ile movie ya bush Man kalivyo kiuma kiatu cha yule mzungu alikaburuza jangwan mpaka akachoka akavua kiatu akafikir Kata muacha akipumzika nakenyewe kanapumzika ni nomaa
 
Kuna mchaga mmoja aliniambia kwao wanamwita "Kilorani" Akikuona porini mwanaume ana kimbilia kula pumbu zako
Dah hii hatari sasa,si bora hata angekuwa anauma miguu..
 
Hahahah Nyegere yaani anaogopa binadamu atamwibia demu wake!! Hahahaha ametisha.
 
Nyegere, melesi au mhilu (Mellivora capensis ) ni
mnyama mdogo wa familia Mustelidae anayetokea Afrika , Mashariki ya Kati na Uhindi.

Nyegere huishi peke yao kwenye shimo analolichimba yeye mwenyewe. Ni wachimbaji wazuri sana. Vile vidole vyao vyenye kucha ndefu na ngumu humsaidia sana kwenye kazi hii. Hata kama ardhi ni ngumu sana, ana uwezo wa kuchimba shimo linalomtosha kujificha katika kipindi kinachokadiriwa kuwa ni dakika kumi tu.

NYEGERE (Honey burger) a.k.a "The fearless animal" TABIA NA MAMBO YAKE MENGINE Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike.

Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke,mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake (ukizingatia milango ya vijijini si imara).

Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii. Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja,akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi
porini kimya kimya Ni mnyama mdogo anayekula nyoka, kenge, majani, matunda, kenge, mizoga ya binadamu, chui, simba, duma, ndege n.k.

Kwa kifupi anakula kila kitu na ngozi yake ni ngumu sana kiasi kwamba mishale na mikuki au risasi ni ngumu kupenya..ukitaka kumuua ni kumpiga katika fuvu la kichwa chake na kitu kizito au risasi kichwani,katika guines world book of records yeye ndio the most fearless creature on the planet mwili wake haudhuriki na sumu ya nyoka wa kawaida na ikitokea ameumwa na nyoka mwenye sumu kali na sumu ikapenya kwenye damu yake itamfanya alale kwa masaa kadhaa tu kisha ataendelea na mambo yake. Ana meno makali/magumu sana yenye uwezo wa kupasua hata jumba la kobe.

Ashawahi kukutwa akipigana na simba na hata tembo na vifaru katika nyakati tofauti. Ni mvivu katika maswala ya nyumba yake hivyo basi anapojisikia uvivu hujilaza sehemu yoyote inayomfaa..ishaonekana akiwa kajiliza katika pango la mbwa mwitu kama kwake. Wanapatikana India,Kusini magharibi barani Asia na Afrika.

IMG_20191219_144516.jpeg
IMG_20191219_144512.jpeg
250px-Honey_badger.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom