Je unawakumbuka herbalist maarufu wa kitambo hicho?

Je unawakumbuka herbalist maarufu wa kitambo hicho?

Huyo Matunge Herbalist kuna mwaka nilienda kwenye ofisi yake maeneo ya Kijitonyama kama sijakosea! Nilipewa dawa feki tu kama ilivyokuwa kwa yule Mwaka wa Ilala Bungoni! Yaani ilikuwa ni wizi tu.
pole mkuu kumbe nawewe ulikuwa muhanga
 
Hii Tanzania 🇹🇿 Kazi Ipo Kubwa Sana Sana
 
Dr MISI. Huyu alikuwa anazunguka Nchi nzima na Landrover lake, akiwa na manesi wake. Nilionana naye miaka ya mwanzoni mwa 1990 pale Mwanza, Nsimbo Hotel. Ugonjwa nikaja kuponea Hospitali ya YMCA Moshi!
 
Mimi nimewakumbuka hawa

- Profesa Matunge r.i.p

- Hawa Nyamichwo r.i.p

- Ng'winzukulu Jilala r.i.p

- Profesa Majimarefu r.i.p

- Dr. Rahabu Lubago

- Dr. Isaac Ndodi
Tumbo
Mwenye jina Tandare kwa Tumbo.
 
Jaman kama hii list isingemtaja Isaac ndodi mimi ningejiuzulu, huyu bwana nlikuwa namwita Dr haleluya, kipindi anaaza, alikuwa anasema ukimkuta mtu ana kitambi piga viboko vya kutosha, alikuwa kakondeana hana hela alivyopata hela kanenepa kawa wa duara ukimuuliza imekuwaje unakula matusi....nimeweka picha ya wakati anaweza career yake na kusema tupigwe viboko na alivyo sasa 😂😂😂. Nlikuwa nkikaa star tv kwa kipindi chake nacheka sana....
 

Attachments

  • images.jpeg-8.jpg
    images.jpeg-8.jpg
    30.1 KB · Views: 1
  • images.jpeg-7.jpg
    images.jpeg-7.jpg
    7.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom