Themagufulianz
JF-Expert Member
- Apr 15, 2017
- 4,548
- 1,988
Aliwafukuza kwa mujibu wa Katiba ya CCM.............
Yaani kwa kutumia vikao halali vilivyoainishwa katika Katiba ya CCM
Sivyo afanyavyo Jiwe, ambaye wala hafuati Katiba ya CCM, wala Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Yeye ni kutembeza ubabe na vitisho kwa kwenda mbele..................
Hiyo ya Nyerere kuwa upinzani utatoka CCM ilisha timia - ni Lowassa aliyeitimizaKatika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM
Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa
Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.
Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma
Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!
HapanaKwa hiyo kafukuzwa na mkutano mkuu au halmashauri kuu na cc ikaridhia?
Wacha uongo.. sanduku la kura halihusiki kwny ushindi awamu hiiKUWA MZALENDO SHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020 (RAIS, WABUNGE NA MADIWANI) KWA MAANA NI HAKI YAKO YA MSINGI SANA KIKATIBA
Mwambie atoke hadharani aje field huku ndio kuna watu aachane na hako ka twiter kake ka watu elfu 4
Membe ni sehemu ya game wanayo-play CCM kuendelea kuwa madarakani kirahisi.Membe ni another false hope..
As long hakuna katiba mpya hata aje nani hana atakachopata
Unahangaika bure tu na huyo Membe wako!Hiyo hali ya kumtetemekea huyo Magu, ndiko ambako kwa ujasiri mkubwa Mheshimiwa Membe amekugomea.......
Na yeye mwenyewe amesema upo umati mkubwa sana wa wanaccm ambao wapo nyuma yake, ambao hawakubali mfumo wa utawala wa hivi sasa wa ONE MAN SHOW
antimatterWacha uongo.. sanduku la kura halihusiki kwny ushindi awamu hii
Kumbe huyu Membe ni makini sana
Mbona swali langu la msingi hutaki kunijibu, je ni halali Membe kufukuzwa kupitia kikao cha Kamati Kuu pekee?Unahangaika bure tu na huyo Membe wako!
Nakushauri rudi nyuma utafute threads za kuanzia julai 2015 kuelekea uchaguzi mkuu utajifunza kitu. Na uhakika ukisoma zile nyuzi utagundua kumbe hapa unafanya kazi ya kuchosha.
Hiyo shida ya "kutoboa" inasababishwa na nini??Mwaka huu hauna mabadiliko. Wapinzani watatoboa kwa shida sana.
Najua nitapigwa mawe. But note me.
Kwani Membe amekwambia kuna kamati gani nyingine inapaswa kumfukuza?Mbina swaki langu la msingi hutaki kunijibu, je ni halali Membe kufukuzwa kupitia kikao cha Kamati Kuu pekee?
Hio fomu atapatia wapi.Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM
Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa
Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.
Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma
Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!
Bado.. kikao kilichomfukuza ni batili kwa mujibu wa katiba, hivyo bado ni mwanachama haiKwa hiyo hajafukuzwa?
Mgombea wa chama chetu ccm 2020 ni mheshimiwa Benard K. MembeAnaota!
Sasa kama Membe anaona hajafukuzwa chama, mwambie form hazipatikani twiter!Bado.. kikao kilichomfukuza ni batili kwa mujibu wa katiba, hivyo bado ni mwanachama hai