Uchaguzi 2020 Je, utabiri wa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM kuanza kutokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu?

Aliwafukuza waliompinga....

Na kama taratibu ni pamoja na kikao...

Hakumfukuza kwa barua ya utenguzi[emoji3][emoji3]
Aliwafukuza kwa mujibu wa Katiba ya CCM.............

Yaani kwa kutumia vikao halali vilivyoainishwa katika Katiba ya CCM

Sivyo afanyavyo Jiwe, ambaye wala hafuati Katiba ya CCM, wala Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Yeye ni kutembeza ubabe na vitisho kwa kwenda mbele..................
 
Membe hana hata nusu ya ule ushawishi wa Lowasa wa 2015 ndani na nje ya CCM.

Mnaotegemea muujiza kutoka kwake mnapoteza muda tu.
 
Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM

Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu

Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa

Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.

Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma

Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!
Hiyo ya Nyerere kuwa upinzani utatoka CCM ilisha timia - ni Lowassa aliyeitimiza
 
Kwa hiyo kafukuzwa na mkutano mkuu au halmashauri kuu na cc ikaridhia?
Hapana

Hajafukuzwa na mkutano Mkuu wala Halmashauri Kuu, bali ni hiyo Kamati Kuu ambayo katika utawala huu wa awamu ya tano "inajimwambafai" na kujona yenyewe ni sawasawa na mungu mtu
 
Membe ni another false hope..
As long hakuna katiba mpya hata aje nani hana atakachopata
Membe ni sehemu ya game wanayo-play CCM kuendelea kuwa madarakani kirahisi.

Haya ni maigizo tu, ndio maana anaongea bila vitendo, hutamwona akienda kuchukua form.

Wapinzani nao kwa kukosa focus wanashabikia haya maigizo yatakayowapoteza.

Na kwa uhakika miezi michache after election hutasikia hizi mbwembwe za Membe kama ilivyo kwa Lowassa sasa.
 
Hiyo hali ya kumtetemekea huyo Magu, ndiko ambako kwa ujasiri mkubwa Mheshimiwa Membe amekugomea.......

Na yeye mwenyewe amesema upo umati mkubwa sana wa wanaccm ambao wapo nyuma yake, ambao hawakubali mfumo wa utawala wa hivi sasa wa ONE MAN SHOW
Unahangaika bure tu na huyo Membe wako!
Nakushauri rudi nyuma utafute threads za kuanzia julai 2015 kuelekea uchaguzi mkuu utajifunza kitu. Na uhakika ukisoma zile nyuzi utagundua kumbe hapa unafanya kazi ya kuchosha.
 
Wacha uongo.. sanduku la kura halihusiki kwny ushindi awamu hii
antimatter
Bora umemwambia ukweli huyo kada wa Lumumba

Kwani yeye hajui kuwa katika awamu hii ushindi unapatikana kwa kuporwa masanduku ya kura waziwazi, kwa kutumia mitutu ya bunduki?
 
Unahangaika bure tu na huyo Membe wako!
Nakushauri rudi nyuma utafute threads za kuanzia julai 2015 kuelekea uchaguzi mkuu utajifunza kitu. Na uhakika ukisoma zile nyuzi utagundua kumbe hapa unafanya kazi ya kuchosha.
Mbona swali langu la msingi hutaki kunijibu, je ni halali Membe kufukuzwa kupitia kikao cha Kamati Kuu pekee?
 
Mbina swaki langu la msingi hutaki kunijibu, je ni halali Membe kufukuzwa kupitia kikao cha Kamati Kuu pekee?
Kwani Membe amekwambia kuna kamati gani nyingine inapaswa kumfukuza?

Je, hiyo kamati imeshakaa kikao? May be ikikaa ndio itamfukuza? Kwani kuna timeframe kwamba ni lazima hiyo kamati ikae ndani ya muda flani ili kuridhia kufukuzwa kwa Membe?
 
~Labda mbingu igusane na ardhi sio kwa utawala huu...zzm!
 
Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM

Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu

Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa

Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.

Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma

Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!
Hio fomu atapatia wapi.
 
~Labda mbingu igusane na ardhi sio kwa utawala huu...zzm!
Wewe unawaza kibinadamu na Mungu ana mipango yake........

Lisilowezekana kwa binadamu, linawezekana kirahisi sana kwa Mungu wetu Mkuu kushinda vitu vyote
 
Bado.. kikao kilichomfukuza ni batili kwa mujibu wa katiba, hivyo bado ni mwanachama hai
Sasa kama Membe anaona hajafukuzwa chama, mwambie form hazipatikani twiter!
Mwambie aende makao makuu ya ccm akachukue form aache kelele.
 
Back
Top Bottom