Kasiano Muyenzi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,858
- 22,729
Alikuwa sahihi kwa mazingira ya wakati ule. Kwa sasa siyoNyerere alikuwa mkono wa chuma....
Jifunze zaidi...
Unavyo visikia ni vitamu tu na nukuu zake nzuri
Umeona like yangu huko?Membe ni another false hope..
As long hakuna katiba mpya hata aje nani hana atakachopata
Alikuwa sahihi kwa mazingira ya wakati ule. Kwa sasa siyo
Una maoni gani kuhusu hili la Membe kubwata tu mitandaoni, wakati anajua fomu zinapopatikana ila haendi kuchukua?
Kudai kwamba Membe hakufukuzwa uanachama wa CCM kihalali na kwamba anastahili kugombea Urais chini ya CCM ni ndoto za Alinacha. Membe alipewa fursa ya kukata rufaa, lakini kwa dharau yake akaipuuza na akasema wala hataomba msamaha kama wenzake walivyofanya. Hiki ni kiburi cha hali ya juu na sidhani kama kuna taasisi yo yote inayoweza kumstahimili mtu mwenye kiburi cha aina hii. Kulikuwa na fursa pia ya kwenda Mahakamani. Lakini nako wangemwambia amalize kwanza taratibu zote zilizowekwa na Chama za kukata rufaa. Ikishindikana ndipo arudi Mahakamani. Hivyo angerudishwa huko huko alikokudharau. Hitimisho ni kwamba sasa hivi habari ya Membe ni kwisha. Dirisha la rufaa Kikatiba limeisha fungwa. Labda akijitathmini, aondoe kiburi na kwenda kuomba msamaha ndipo anaweza kufikiriwa. Kule kwenda kwenye vyombo vya habari na kulalamika kwamba hakufukuzwa kihalali hakusaidii cho chote.Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM.
Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa.
Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.
Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma
Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!
Unajua tatizo la Mwenyekiti wsko anapenda sana kunyenyekewa na anapenda asujudiwe na kuombwa msamaha.Kudai kwamba Membe hakufukuzwa uanachama wa CCM kihalali na kwamba anastahili kugombea Urais chini ya CCM ni ndoto za Alinacha. Membe alipewa fursa ya kukata rufaa, lakini kwa dharau yake akaipuuza na akasema wala hataomba msamaha kama wenzake walivyofanya. Hiki ni kiburi cha hali ya juu na sidhani kama kuna taasisi yo yote inayoweza kumstahimili mtu mwenye kiburi cha aina hii. Kulikuwa na fursa pia ya kwenda Mahakamani. Lakini nako wangemwambia amalize kwanza taratibu zote zilizowekwa na Chama za kukata rufaa. Ikishindikana ndipo arudi Mahakamani. Hivyo angerudishwa huko huko alikokudharau. Hitimisho ni kwamba sasa hivi habari ya Membe ni kwisha. Dirisha la rufaa Kikatiba limeisha fungwa. Labda akijitathmini, aondoe kiburi na kwenda kuomba msamaha ndipo anaweza kufikiriwa. Kule kwenda kwenye vyombo vya habari na kulalamika kwamba hakufukuzwa kihalali hakusaidii cho chote.
Alishatokea Lyatonga Mrema!Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM.
Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa.
Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.
Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma
Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!
Membe nae ana Godfather sio bure.Unajua tatizo la Mwenyekiti wsko anapenda sana kunyenyekewa na anapenda asujudiwe na kuombwa msamaha.
Hebu nieleze unasema Membe anapaswa kumwomba msamaha Magu kwa kosa gani?
Anamuomba msamaha kwa kosa gani?
Kama ni kosa aliyefanya ni Musiba aliyewakashifu na kutoa taarifa za uwongo dhidi ya akina Membe.
Mbona huyo Musiba wenu amekuwa "untouchable" na hatakiwi kuhojiwa na chombo chochote kile?
Hivi mnadhani huku kutumia vyombo vya dola kuwaonea wote mnaodhani kuwa ni anti-Magu, itadumu hivyo mpaka lini?
Ndiyo maana yeye mwenyewe Membe ametamka "between now and October this year" lolote katika siasa za Tanzania litatokea.
Yetu macho, hebu tuwe na subira kwa vile yavuta heri.
Absolutely trueWanasiasa wengi ndani ya CCM ni wanafiki.....anakubali kutatua tatizo la tumbo lake na kuiacha Tanzania ikiteketea... kwa namna Bunge lilivyo, Mahakama ilivyo namna Tume ya Uchaguzi ilivyo....aisee inafikia hatua nasema kwa hatua hizi ndogo tu alizochukua Mh. Membe so far...... kweli Taifa litamkumbuka.
Tumebakia na wanasiasa wanaotumikia matumbo yao, yaani kumwita kiongozi ni Yesu ni uthibitisho tosha kwamba leo tunatumia matumbo kufikiri badala ya kichwa.
Mh. Membe nimekuelewa na mpaka ifikapo October 2020 watanzania karibia 80% watakuelewa kwamba - " Kazi na................."
Sawa.Mimi Ni Mtu Huru Kabisa na muumini wa utu.
Na nina Fikra zangu mwenyewe, wala siwezi kuwa msukule wa mtu wala chama chochote.
Huwezi kuuona uovu aliyotendewa Akwilini, Mdude au Tundu Lissu Kama wewe umekabidhi kichwa chako kwa mtu mwingine.
Weka huo mfanoSawa.
Lakini kuna nyakati unakengeuka kabisa na kuwa tofauti na hali hiyo uliyoielezea hapa!
Ninaweza kukutafutia mfano humu humu JF, maanake hakuna kinachofutika.
Nimetafuta, sijaona.Weka huo mfano
Mapya yapi ?Nimetafuta, sijaona.
Basi niseme huenda huwa nakusoma bila ya kuweka umakini stahiri.
Lakini nimegundua mapya yasiyohusiana na hili lililotufanya tujibishane hapa. Hayo nayaweke kibindoni.