Uchaguzi 2020 Je, utabiri wa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM kuanza kutokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu?

Chonde chonde tupeane ukweli Nyerere hakuwahi kuwa nabii wa kweli ama uongo bali alikuwa mwalimu kisha akawa rais & mwenyekiti wa CCM kwa miongo mingi.

Kusema kuwa alitabiri kuwa mpinzani wa kweli atatoka CCM huo ni uongo mkubwa, nasema hivi kwa sababu Nyerere hakuwa na jipya bali alitetea fikra zake ili kuwapumbaza watu.

Ukweli ni huu Nyerere alibadili aya isemayo "adui yako ni mtu wa nyumbani mwako" kwa kuifanya iwe neno la "mpinzani wa kweli atatoka CCM"

Hapo Nyerere hakutabiri bali alikopi Bible kijana 😀
 
Hata lowasa mlisemaga hivyo hivyo jana tumwemwona kamdhamini yuleyule aliekuwa mpinzani wake.
 
Waswahili wanasema adui ni yule aliyeko nyumbani kwako.
Kwa usemi huu, upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM.
Hii ni kwa sababu viongozi wote hodari na walioiva Kisiasa wako ndani ya CCM au wametokana na CCM.
Hili pia halina ubishi kuwa upinzani wa kweli ndani ya vyama vya upinzani utatoka ndani ya vyama vyenyewe vya upinzani na siyo CCM. CCM inaweza kuwatumia watu wa upinzani ili kupingana wenyewe kwa wenyewe kwa maana ya kuwagawa. ( divide and rule).
Kwa Inchi za Afrika ambako utawala wa katiba bado hauzingatiwi sana kama Inchi zilizoendelea, ni hatari kuingiza vyama vichanga kwenye uongozi wa Inchi.
Tunavyoona sasa, vyama vingi vya Siasa havina Demokrasi ndani yake na vinamwonekano wa kumilikiwa na mtu moja ( mwanzilishi).
Toka CHADEMA, CUF, ACT na kadhalika vimeundwa, tumethibitisha bila shaka kuwa ni vyama ambavyo vinamilikiwa na waanzilishi na si wanachama na vimekaa kishabiki zaidi kuliko kisiasa. Kiongozi mwanzailishi anapohama kama CUF na NCCRA MAGEUZI anahama na wanachama/washabiki wake.
Ni kweli kwa mfano CCM ikimeguka na akina MEMBE, KINANA, MAKAMBA, NAUYE na kwa rais mstaafu moja au wawili wakajiingiza katika kundi hili basi CCM itakuwa imemeguka na kuanzisha upinzani wa kweli.
Kitendo hiki cha CCM kumeguka ni hatari sana kwa usalama wa Inchi kwa sababu kutakuwa na kulipizana kisasi.
Tunachoomba kwa Mungu ni kuwa Upinzani kwa kweli uendelee kuwa ndani ya CCM kwa kuimarisha Demokrasia ili kisionekane kuwa ni chama cha Wanachama.
Watu wote wafurahie na kunufaika na keki ya Inchi hii na kuwe na pesa za kutosha kwenye mzunguko ili watu waweze kufanya shughuli za maendeleo ( money works).
Hayati Mwaimu Nyerere alisema " pesa si msingi wa maendeleo ila ni matokeo yake"
Kwa usemi huu kama hakuna pesa kwenye mzunguko au zimepungua maana yake ni kuwa hakuna maendeleo kwa mwanainchi au kaya moja moja.
 
Una maoni gani kuhusu hili la Membe kubwata tu mitandaoni, wakati anajua fomu zinapopatikana ila haendi kuchukua?

Kwangu mimi Membe ni muhuni kama walivyo wahuni wengine wa ccm. Hilo halijalishi kaenda kuchukua fomu ya ccm ama la. Sisi kama taifa tuko hapa kwa ajili ya maamuzi mabovu ya wanaccm wote. Membe ni mmoja ya wanaccm walionajisi mchakato wa katiba mpya, hicho kilio chake cha sasa ni sehemu ya karma ya uhuni wake wa kunajisi katiba ya wananchi.
 
Nyinyi ni watu wa visasi na mnaendeleza vitisho vyenu
 
Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM.

Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa.

Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.

Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma

Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!
Kudai kwamba Membe hakufukuzwa uanachama wa CCM kihalali na kwamba anastahili kugombea Urais chini ya CCM ni ndoto za Alinacha. Membe alipewa fursa ya kukata rufaa, lakini kwa dharau yake akaipuuza na akasema wala hataomba msamaha kama wenzake walivyofanya. Hiki ni kiburi cha hali ya juu na sidhani kama kuna taasisi yo yote inayoweza kumstahimili mtu mwenye kiburi cha aina hii. Kulikuwa na fursa pia ya kwenda Mahakamani. Lakini nako wangemwambia amalize kwanza taratibu zote zilizowekwa na Chama za kukata rufaa. Ikishindikana ndipo arudi Mahakamani. Hivyo angerudishwa huko huko alikokudharau. Hitimisho ni kwamba sasa hivi habari ya Membe ni kwisha. Dirisha la rufaa Kikatiba limeisha fungwa. Labda akijitathmini, aondoe kiburi na kwenda kuomba msamaha ndipo anaweza kufikiriwa. Kule kwenda kwenye vyombo vya habari na kulalamika kwamba hakufukuzwa kihalali hakusaidii cho chote.
 
Unajua tatizo la Mwenyekiti wsko anapenda sana kunyenyekewa na anapenda asujudiwe na kuombwa msamaha.

Hebu nieleze unasema Membe anapaswa kumwomba msamaha Magu kwa kosa gani?

Anamuomba msamaha kwa kosa gani?

Kama ni kosa aliyefanya ni Musiba aliyewakashifu na kutoa taarifa za uwongo dhidi ya akina Membe.

Mbona huyo Musiba wenu amekuwa "untouchable" na hatakiwi kuhojiwa na chombo chochote kile?

Hivi mnadhani huku kutumia vyombo vya dola kuwaonea wote mnaodhani kuwa ni anti-Magu, itadumu hivyo mpaka lini?

Ndiyo maana yeye mwenyewe Membe ametamka "between now and October this year" lolote katika siasa za Tanzania litatokea.

Yetu macho, hebu tuwe na subira kwa vile yavuta heri.
 
Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM.

Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa.

Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.

Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma

Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!
Alishatokea Lyatonga Mrema!
 
Wanasiasa wengi ndani ya CCM ni wanafiki.....anakubali kutatua tatizo la tumbo lake na kuiacha Tanzania ikiteketea... kwa namna Bunge lilivyo, Mahakama ilivyo namna Tume ya Uchaguzi ilivyo....aisee inafikia hatua nasema kwa hatua hizi ndogo tu alizochukua Mh. Membe so far...... kweli Taifa litamkumbuka.

Tumebakia na wanasiasa wanaotumikia matumbo yao, yaani kumwita kiongozi ni Yesu ni uthibitisho tosha kwamba leo tunatumia matumbo kufikiri badala ya kichwa.

Mh. Membe nimekuelewa na mpaka ifikapo October 2020 watanzania karibia 80% watakuelewa kwamba - " Kazi na................."
 
Unajua tatizo la Mwenyekiti wsko anapenda sana kunyenyekewa na anapenda asujudiwe na kuombwa msamaha.

Hebu nieleze unasema Membe anapaswa kumwomba msamaha Magu kwa kosa gani?

Anamuomba msamaha kwa kosa gani?

Kama ni kosa aliyefanya ni Musiba aliyewakashifu na kutoa taarifa za uwongo dhidi ya akina Membe.

Mbona huyo Musiba wenu amekuwa "untouchable" na hatakiwi kuhojiwa na chombo chochote kile?

Hivi mnadhani huku kutumia vyombo vya dola kuwaonea wote mnaodhani kuwa ni anti-Magu, itadumu hivyo mpaka lini?

Ndiyo maana yeye mwenyewe Membe ametamka "between now and October this year" lolote katika siasa za Tanzania litatokea.

Yetu macho, hebu tuwe na subira kwa vile yavuta heri.
Membe nae ana Godfather sio bure.
Lakini kama Membe hatafanikiwa kupeperusha bendera ya CCM itakuwa kazi ngumu sana kuukwa u president.
Kura ya mpinzani haiwezi kuheshimika.
 
Wanasiasa wengi ndani ya CCM ni wanafiki.....anakubali kutatua tatizo la tumbo lake na kuiacha Tanzania ikiteketea... kwa namna Bunge lilivyo, Mahakama ilivyo namna Tume ya Uchaguzi ilivyo....aisee inafikia hatua nasema kwa hatua hizi ndogo tu alizochukua Mh. Membe so far...... kweli Taifa litamkumbuka.

Tumebakia na wanasiasa wanaotumikia matumbo yao, yaani kumwita kiongozi ni Yesu ni uthibitisho tosha kwamba leo tunatumia matumbo kufikiri badala ya kichwa.

Mh. Membe nimekuelewa na mpaka ifikapo October 2020 watanzania karibia 80% watakuelewa kwamba - " Kazi na................."
Absolutely true

Kwa namna ya utawala huu na namna Mheshimiwa Membe alivyojitoa mhanga, hakika ni lazima Umma wa wananchi tumpe pongezi
 
Mimi Ni Mtu Huru Kabisa na muumini wa utu.

Na nina Fikra zangu mwenyewe, wala siwezi kuwa msukule wa mtu wala chama chochote.

Huwezi kuuona uovu aliyotendewa Akwilini, Mdude au Tundu Lissu Kama wewe umekabidhi kichwa chako kwa mtu mwingine.
Sawa.

Lakini kuna nyakati unakengeuka kabisa na kuwa tofauti na hali hiyo uliyoielezea hapa!

Ninaweza kukutafutia mfano humu humu JF, maanake hakuna kinachofutika.
 
Weka huo mfano
 
Weka huo mfano
Nimetafuta, sijaona.

Basi niseme huenda huwa nakusoma bila ya kuweka umakini stahiri.

Lakini nimegundua mapya yasiyohusiana na hili lililotufanya tujibishane hapa. Hayo nayaweke kibindoni.
 
Mapya yapi ?
 
Back
Top Bottom