Uchaguzi 2020 Je, utabiri wa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM kuanza kutokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu?

Hivi hizi haki za binadamu zinazoongelewa sana ni zipi haswaa....mbona wengine tunachapa tu kazi na kupata pesa.
 
Hivi hizi haki za binadamu zinazoongelewa sana ni zipi haswaa....mbona wengine tunachapa tu kazi na kupata pesa.
Maisha kwa binaadam wengi ni zaidi ya "kuchapa kazi na kupata pesa."

Kama hilo ndilo lingekuwa lengo, pengine pasingekuwepo na sababu ya kutafuta uhuru na kuwaondoa wakoloni.

Lakini najua haya yote unayajua. Ni kujitia ujinga, hapana upumbavu tu kuuliza swali kama hilo enzi hizi.
 
Lazima mtambue ya kwamba kina Nyerere walikubali mfumo wa vyama vingi kumuhadaa mzungu mshenzi anayependa kuona tuna misuguano,kina Nyerer,Kenyata na kina Nkuruma pia Patric Lumumba wakashauliana kukubali lakini kwa kuutengeneza upinzani hewa ili kumlaghai mzungu awe mpole na aendelee kutoa pesa za misaada,maana unapokua na vyama vitajikuta vyote vina wafadhiri kutoka kwa washenzi ili kwamba ukiingia wewe mamlakani utatuachia kadhaa kadhaa,kisha vyama hivyo vinachota pesa na inakuja hapa hapa nchini,so upinzani siyo ule wa kweli kama watu wengi wafikiriavyo,na nchi kama nchi ikiukataa basi mzungu mshenzi anaweza kutengeneza uasi.

Ikumbukwe ya kwamba kubali kataa sisi kama waafrika hatuna haja ya vyama vya siasa maana vinasababisha kutumia pesa na muda badala ya kufanya kazi kujikwamua kwenye umasikini,nasema vyama vya siasa havina maana hapa Afrika isipokua kufanya kazi kwa bidii kama wafanyavyo wachina. Kwa hiyo kuona kumeguka kwa CCM kunaweza siku moja kukaja lakini bado watu watakua ni wamoja na mmeguko wao utalenga njia hizo hizo za kumuhadaa mshenzi mweupe na sisi tutaendelea na yetu,kiufupi viongozi wana akili nyingi na wako kwa ajili ya kupambania amani ktk nchi bila wananchi wengi kujua ukweli,unakutana na mtu anapiga kelele kuhusu siasa na kiukweli hajui lolote zaidi ya kufuata mkumbo tu.

Mfano rahisi unaweza ona mtu anatoka chama hiki kwenda kingine na watu wanashabikia halafu baada ya muda mtu yule anabadilisha gear

Upinzani leo hii unaweza ukashauli jambo na likitekelezwa leo, kesho kutwa wanarudi kuliponda tena. Lazima kutumia akili kujua ABC ya kinachoendelea nchini.
 
hivi izi twits za membe watu wanauhakika gani kama ni yeye kweli huwa anaandika🤔🤔🤔🤔
 
Mwanoko!!
 
Acha tu wauee upinzani
Ila ccm watakuja kuboana
Wenyewe

Ova
 
Hakuna nchi isiyo na upinzani, Upinzani upo si lazima uwe na jina tofauti na chama, chama kinaweza kuwa kimoja ila upinzani ukawepo.

Ni lazima kujikosoa. China pia upinzani upo fuatilia, kuna watu lazima hawakubaliani na viongozi na huwa wanaadhibiwa tena nasikia kunyongwa.

Ni asili ya binadamu kukosoana. Hata kama umedhibitiwa na huwezi kufanya lolote utakosoa kama si kwa mkeo basi moyoni mwako.
 
chagu wa malunde
Hebu tuambie namna mlivyomfukuza uanachama wake Membe , ndivyo inavyotakiwa katika Katiba ya CCM?
Katiba ya chama imefutwa vizuri tu. Kamati kuu imeamua afukuzwe chama. Kikatiba itapeleka maamuzi hayo NEC kwa maamuzi ya mwisho. Hali halisi imeonyesha kuwa kamati kuu huwa haipingwi na NEC. Membe anakuja hilo kwani ni mzoefu kwenye chama. Mimi naona anachofanya ni kujitambulisha kwa wananchi kwa kutumia hoja ilyokosa nguvu lakini yenye kumfanya ajulikane kuwa yupo kwenye ushindani.
 
Kama wewe unalijua hilo kuwa ni LAZIMA suala la Membe lilipaswa kupelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya CCM, je ni kwanini akina Dkt Bashiru, wali-skip hatua hiyo?
 
Halmashauri kuu siyo cc.
Cc inatoa mapendekezo tu. Katiba ya chama ndivyo inavyosema.

Hivi ni vigumu sana kuipata hiyo katiba ya CCM na tusome wote ibara inayoeleza namna mwanachama anavyopaswa kufutiwa uanachama wake?

Maana naona watu wanajadili kwa hisia na mihemko binafsi tu bila uthibitisho...

Mwenye soft copy ya katiba ya CCM ingalau ibara hiyo tu ya "mtu kukoma kuwa mwanachama na utaratibu wa kumfutia mtu uanachama" aiweke hapa ili mjadala unoge...

Mimi I am sure Membe siyo mjinga. Ni lazima anazungumza hayo kwa reference ya katiba yao huko CCM...
 

Hili ndilo kosa...

Usiseme "....imeamua afutwe uanachama..."

Sema "....imependekeza apewe adhabu ya kufutiwa uanachama wake..."

CC ingekuwa " imeamua" kama unavyoandika hapa, basi hakuna haja ya maamuzi hayo kupelekwa ktk kikao kingine tena. Yapelekwe huko kwa lipi sasa kama ina maamuzi ya mwisho ya "kufuta?"

Japo tunajadili jambo hili bila kuweka vipengere vya katiba ya CCM hapa juu ya namna mwanachama anavyoweza kufutiwa uanachama wake, lakini kama unavyoeleza hapa ndivyo ilivyo, basi hai - make sense hata kidogo hata kwa mtu asiyeisoma katiba ya CCM...!;

Kinachopelekwa kwenye kikao kingine cha juu kwa uamuzi wa mwisho huwa ni "mapendekezo" na siyo "maamuzi"...

Kwa maana hiyo kama mapendezo ya CC yatapelekwa Halmshauri kuu? Mkutano mkuu?, ina maana lazima sababu za kufutwa uanachama mwanachama zipitiwe upya na naamini na mwanachama muhusika anaweza kupewa nafasi nyingine tena kujitetea kabla ya final judgement ya kuridhia maamuzi ya CC kuwa iko sawa ama kuyafanyia marekebisho ama kuyakataa/futa kabisa...

Huo ndiyo utaratibu wa kidemokrasia...
 
Ipo google
 
Hivi watu wa vyama vya upinzani hamjifunzi kutokana na matukio mbalimbali ya kisiasa hasa unapowadia wakati wa Uchaguzi Mkuu kila wakati unapofika? Mwaka 2015 mliowaona akina Mh.Lowassa walivyo papatikiwa na vyama vya upinzani kwa malengo yao tofauti. Timu Lowassa na timu CHADEMA walikuwa na malengo tofauti. Kambi moja ilikuwa inaitaka IKULU, kambi nyingine ilikuwa inataka wabunge wengi ili ipige RUZUKU. Wote tunajua what happened, in fact that is now history. Sasa inaingia Timu Membe, nayaona yale ya 2015 yakujirudia tena. Timu Membe inaitaka IKULU kwa udi na uvumba Timu Membe haina haja ya pesa, inataka sifa na kuwatumikia walioituma, haitaki pesa, pesa wanazo za kutosha yaani zile za CHANGE YA RADAR na zile LIBYA! Nasikia ACT - Wananchi nao wanamtaka, nao wana malengo ya kupata wabunge kupitia kwa Timu Membe ili waongeze RUZUKU hiyo ya Mbunge mmoja haina tija. Pia kwa mkakati huo wanadhani wanaweza kufanya kazi waliyopewa na "donors" wao na kutoa mahesabu sahihi; kwani hakuna pesa ya "donor" isiyotolewa mahesabu - You have to account for it! Hivyo basi tungoje tuone their next move.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…