interegenciadick
JF-Expert Member
- Nov 26, 2016
- 698
- 1,090
Hivi hizi haki za binadamu zinazoongelewa sana ni zipi haswaa....mbona wengine tunachapa tu kazi na kupata pesa.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, inawezekana ulibadili jina?Mapya yapi ?
Hapana huyo ni mwingine.Mkuu, inawezekana ulibadili jina?
Kuna mtu alikuwa na jina la 'Mkaruka itajanu...' au kitu kama hicho, ni wewe?
Mapya niliyoyaelewa nilipotafuta habari zako ili nikupe jibu sahihi.
Maisha kwa binaadam wengi ni zaidi ya "kuchapa kazi na kupata pesa."Hivi hizi haki za binadamu zinazoongelewa sana ni zipi haswaa....mbona wengine tunachapa tu kazi na kupata pesa.
Basi niliwachanganya, maana sikuona chochote kuhusu wewe kinachokaribiana na niliyoyaandika kukuhusu hadi tukafika hapa.
Lazima mtambue ya kwamba kina Nyerere walikubali mfumo wa vyama vingi kumuhadaa mzungu mshenzi anayependa kuona tuna misuguano,kina Nyerer,Kenyata na kina Nkuruma pia Patric Lumumba wakashauliana kukubali lakini kwa kuutengeneza upinzani hewa ili kumlaghai mzungu awe mpole na aendelee kutoa pesa za misaada,maana unapokua na vyama vitajikuta vyote vina wafadhiri kutoka kwa washenzi ili kwamba ukiingia wewe mamlakani utatuachia kadhaa kadhaa,kisha vyama hivyo vinachota pesa na inakuja hapa hapa nchini,so upinzani siyo ule wa kweli kama watu wengi wafikiriavyo,na nchi kama nchi ikiukataa basi mzungu mshenzi anaweza kutengeneza uasi.Huo Msemo ukiutafakari sana,Utakuja kuelewa ni kama Siri aliyowaachi Marais wote,na ndio pekee wanajua ukweli wa huo msemo,
Ila tafakari kidogo,Kwanini kila uchaguzi lazima Ccm wenyewe Wasigane,lazima atokee mgombea haelewani na mwenyekiti...
Toka enzi za kambona,mtei,Mrema,Mamvi,ni kama tunaimbishwa nyimbo zile zile kila siku,na tunazicheza vizuri tu..
Ni kama secret code flani,ila wenye kuuelewa huo msemo ni marais tu,trust me,sio msemo wa kawaida...
Siasa bongo tunachezeshwa gere tu........
Mwanoko!!Maisha kwa binaadam wengi ni zaidi ya "kuchapa kazi na kupata pesa."
Kama hilo ndilo lingekuwa lengo, pengine pasingekuwepo na sababu ya kutafuta uhuru na kuwaondoa wakoloni.
Lakini najua haya yote unayajua. Ni kujitia ujinga, hapana upumbavu tu kuuliza swali kama hilo enzi hizi.
Eeenh, tutegemee nini cha ziada toka kwa mtu kama wewe uliyejitambulisha mwenyewe!Mwanoko!!
Hakuna nchi isiyo na upinzani, Upinzani upo si lazima uwe na jina tofauti na chama, chama kinaweza kuwa kimoja ila upinzani ukawepo.Lazima mtambue ya kwamba kina Nyerere walikubali mfumo wa vyama vingi kumuhadaa mzungu mshenzi anayependa kuona tuna misuguano,kina Nyerer,Kenyata na kina Nkuruma pia Patric Lumumba wakashauliana kukubali lakini kwa kuutengeneza upinzani hewa ili kumlaghai mzungu awe mpole na aendelee kutoa pesa za misaada,maana unapokua na vyama vitajikuta vyote vina wafadhiri kutoka kwa washenzi ili kwamba ukiingia wewe mamlakani utatuachia kadhaa kadhaa,kisha vyama hivyo vinachota pesa na inakuja hapa hapa nchini,so upinzani siyo ule wa kweli kama watu wengi wafikiriavyo,na nchi kama nchi ikiukataa basi mzungu mshenzi anaweza kutengeneza uasi.
Ikumbukwe ya kwamba kubali kataa sisi kama waafrika hatuna haja ya vyama vya siasa maana vinasababisha kutumia pesa na muda badala ya kufanya kazi kujikwamua kwenye umasikini,nasema vyama vya siasa havina maana hapa Afrika isipokua kufanya kazi kwa bidii kama wafanyavyo wachina. Kwa hiyo kuona kumeguka kwa CCM kunaweza siku moja kukaja lakini bado watu watakua ni wamoja na mmeguko wao utalenga njia hizo hizo za kumuhadaa mshenzi mweupe na sisi tutaendelea na yetu,kiufupi viongozi wana akili nyingi na wako kwa ajili ya kupambania amani ktk nchi bila wananchi wengi kujua ukweli,unakutana na mtu anapiga kelele kuhusu siasa na kiukweli hajui lolote zaidi ya kufuata mkumbo tu.
Mfano rahisi unaweza ona mtu anatoka chama hiki kwenda kingine na watu wanashabikia halafu baada ya muda mtu yule anabadilisha gear
Upinzani leo hii unaweza ukashauli jambo na likitekelezwa leo, kesho kutwa wanarudi kuliponda tena. Lazima kutumia akili kujua ABC ya kinachoendelea nchini.
Mimi nipo naendelea kuwakanyaga
Katiba ya chama imefutwa vizuri tu. Kamati kuu imeamua afukuzwe chama. Kikatiba itapeleka maamuzi hayo NEC kwa maamuzi ya mwisho. Hali halisi imeonyesha kuwa kamati kuu huwa haipingwi na NEC. Membe anakuja hilo kwani ni mzoefu kwenye chama. Mimi naona anachofanya ni kujitambulisha kwa wananchi kwa kutumia hoja ilyokosa nguvu lakini yenye kumfanya ajulikane kuwa yupo kwenye ushindani.chagu wa malunde
Hebu tuambie namna mlivyomfukuza uanachama wake Membe , ndivyo inavyotakiwa katika Katiba ya CCM?
Kama wewe unalijua hilo kuwa ni LAZIMA suala la Membe lilipaswa kupelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya CCM, je ni kwanini akina Dkt Bashiru, wali-skip hatua hiyo?Katiba ya chama imefutwa vizuri tu. Kamati kuu imeamua afukuzwe chama. Kikatiba itapeleka maamuzi hayo NEC kwa maamuzi ya mwisho. Hali halisi imeonyesha kuwa kamati kuu huwa haipingwi na NEC. Membe anakuja hilo kwani ni mzoefu kwenye chama. Mimi naona anachofanya ni kujitambulisha kwa wananchi kwa kutumia hoja ilyokosa nguvu lakini yenye kumfanya ajulikane kuwa yupo kwenye ushindani.
Halmashauri kuu siyo cc.
Cc inatoa mapendekezo tu. Katiba ya chama ndivyo inavyosema.
Katiba ya chama imefutwa vizuri tu. Kamati kuu imeamua afukuzwe chama. Kikatiba itapeleka maamuzi hayo NEC kwa maamuzi ya mwisho. Hali halisi imeonyesha kuwa kamati kuu huwa haipingwi na NEC. Membe anakuja hilo kwani ni mzoefu kwenye chama. Mimi naona anachofanya ni kujitambulisha kwa wananchi kwa kutumia hoja ilyokosa nguvu lakini yenye kumfanya ajulikane kuwa yupo kwenye ushindani.
Ipo googleHivi ni vigumu sana kuipata hiyo katiba ya CCM na tusome wote ibara inayoeleza namna mwanachama anavyopaswa kufutiwa uanachama wake?
Maana naona watu wanajadili kwa hisia na mihemko binafsi tu bila uthibitisho...
Mwenye soft copy ya katiba ya CCM ingalau ibara hiyo tu ya "mtu kukoma kuwa mwanachama na utaratibu wa kumfutia mtu uanachama" aiweke hapa ili mjadala unoge...
Mimi I am sure Membe siyo mjinga. Ni lazima anazungumza hayo kwa reference ya katiba yao huko CCM...
Na hapo zamani za kale alikuwapo na MZEE MUKARUKA!
Hivi watu wa vyama vya upinzani hamjifunzi kutokana na matukio mbalimbali ya kisiasa hasa unapowadia wakati wa Uchaguzi Mkuu kila wakati unapofika? Mwaka 2015 mliowaona akina Mh.Lowassa walivyo papatikiwa na vyama vya upinzani kwa malengo yao tofauti. Timu Lowassa na timu CHADEMA walikuwa na malengo tofauti. Kambi moja ilikuwa inaitaka IKULU, kambi nyingine ilikuwa inataka wabunge wengi ili ipige RUZUKU. Wote tunajua what happened, in fact that is now history. Sasa inaingia Timu Membe, nayaona yale ya 2015 yakujirudia tena. Timu Membe inaitaka IKULU kwa udi na uvumba Timu Membe haina haja ya pesa, inataka sifa na kuwatumikia walioituma, haitaki pesa, pesa wanazo za kutosha yaani zile za CHANGE YA RADAR na zile LIBYA! Nasikia ACT - Wananchi nao wanamtaka, nao wana malengo ya kupata wabunge kupitia kwa Timu Membe ili waongeze RUZUKU hiyo ya Mbunge mmoja haina tija. Pia kwa mkakati huo wanadhani wanaweza kufanya kazi waliyopewa na "donors" wao na kutoa mahesabu sahihi; kwani hakuna pesa ya "donor" isiyotolewa mahesabu - You have to account for it! Hivyo basi tungoje tuone their next move.Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM.
Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa.
Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.
Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma
Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!