Uchaguzi 2020 Je, utabiri wa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM kuanza kutokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu?

Uchaguzi 2020 Je, utabiri wa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM kuanza kutokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu?

Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM

Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu..
CCM imewaweka wanachama wake kwenye CAGE.

Hakuna anaeweza kuishi nje ya mfumo huo unaomtegemea Mwenyekiti aka yesu mgawa pesa na vyeo.

Ndio maana hata hata wakikukata hawataki uhame.
WanaCCM hawana UHURU
1593053169057.png
 
View attachment 1488177
Hiyo hali ya kumtetemekea huyo Magu, ndiko ambako kwa ujasiri mkubwa Mheshimiwa Membe amekugomea.......

Na yeye mwenyewe amesema upo umati mkubwa sana wa wanaccm ambao wapo nyuma yake, ambao hawakubali mfumo wa utawala wa hivi sasa wa ONE MAN SHOW
 
Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM
Mkuu 'Mystery', hata mimi niliisha isikia hotuba hiyo ya Mwalimu, lakini nadhani nikaielewa tofauti na wewe ulivyoielewa.

Bila kueleza mengi:

CCM aliyokuwa akiizungumzia Mwalimu, siyo CCM hii iliyopo sasa, ambayo ni mali ya mtu (sijui kama unanielewa).

Pili, kwa nini uuone "upinzani huu wa Membe" ndio uweze kutimiza aliyotabiri Mwalimu na siyo "upinzani ule ndani ya CCM uliotokea 2015"?

Ninakubaliana nawe sana, kama CCM kingekuwa ni chama kama kile alichokuwa anakizungumzia Mwalimu wakati ule, huu ungekuwa ni wakati mwafaka sana wa upinzani ndani ya chama chenyewe kuleta mabadiliko, kutokana na baadhi ya sababu ulizoziorodhesha ndani ya mada yako.

Lakini kwa bahati mbaya sana, CCM kama hiyo haipo tena.

Sasa sijui kama ninaeleweka vizuri, au mpaka nifafanue kwa kirefu chake, haya niliyoandika hapa?
 
'Mystery'

Nisisahau kukupongeza kwa kubuni mada zinazofikirisha.

Hilii limekuwa jambo adimu sana siku hizi kuliona hapa JF, hasa kwenye ukumbi huu wa Siasa..
 
CCM imewaweka wanachama wake kwenye CAGE.

Hakuna anaeweza kuishi nje ya mfumo huo unaomtegemea Mwenyekiti aka yesu mgawa pesa na vyeo.

Ndio maana hata hata wakikukata hawataki uhame.
WanaCCM hawana UHURU
View attachment 1488177
Kati ya watu ambao nashindwa kuwatabiri wapo wapi, mmoja wapo ni wewe 'Mkaruka.'
Kama jina lako lina maana yoyote, basi nadhani hiyo ndiyo sababu.
 
'Mystery'

Nisisahau kukupongeza kwa kubuni mada zinazofikirisha.

Hilii limekuwa jambo adimu sana siku hizi kuliona hapa JF, hasa kwenye ukumbi huu wa Siasa..
Kalamu1
Nashukuru sana kwa "appreciation" yako
 
Kati ya watu ambao nashindwa kuwatabiri wapo wapi, mmoja wapo ni wewe 'Mkaruka.'
Kama jina lako lina maana yoyote, basi nadhani hiyo ndiyo sababu.
Mimi Ni Mtu Huru Kabisa na muumini wa utu.

Na nina Fikra zangu mwenyewe, wala siwezi kuwa msukule wa mtu wala chama chochote.

Huwezi kuuona uovu aliyotendewa Akwilini, Mdude au Tundu Lissu Kama wewe umekabidhi kichwa chako kwa mtu mwingine.
 
Miaka yote sijawahi kumsikia akidai tume huru, ila ndani ya miaka mitano akiwa benchi anadai tume huru. Huyu huyu alishawahi kudai 2015 akishinda urais ndoto yake ni baadhi ya watu watafute nchi za kukimbilia. Sikuwahi kumsikia 2015 akidai tume huru wala umuhimu wa tume huru.

Acha aonje joto la jiwe na yeye ndio atatafuta pa kulimbilia baada ya 2020 na kuwaacha aliotaka kuwambiza 2015 watu wa kambi ya Lowassa na Lowassa mwenyewe wakila maisha ndani ya nchi yao huru.

Huyu jamaa ni kama amechanganyikiwa hasa baada ya mizizi yake pale mambo ya nje alipojitengenezea mtandao kukatwa. Anaweweseka
 
Back
Top Bottom