Je, utamkumbuka Hayati Ali Hassan Mwinyi kwa mambo gani?

1. Kupenda Dini na Kusali sana.

2. Kupenda Utani na Ucheshi.

3. Kukitukuza Kiswahili na Kujivunia Kukiongea Kiufasaha...
Namba 7 ni sifa yake kubwa

ni Mwinyi pekee ndie hakujaribu kupandisha mabega akiwa Amiri jeshi , marais wote watano wengine kuna nyakati walikuwa wanajisahau na kujiona kama vile hawajaumbwa kwa udongo
 
Kuna malofa walikuwa wakivamia mabucha ya kitimoto hawataki kuona nyama ya nguruwe inauzwa, nakumbuka mzee Ruksa alitoa amri kuwa wote wanaofanya huo uvamizi wakamatwe na apelekewe anajua pa kuwaficha
 
Ruksa.. ilisema kila kitu ruksa..
Yapi haswa yalikuwa ndio ya ruksa yake?
 
Namba 7 ni sifa yake kubwa

ni Mwinyi pekee ndie hakujaribu kupandisha mabega akiwa Amiri jeshi , marais wote watano wengine kuna nyakati walikuwa wanajisahau na kujiona kama vile hawajaumbwa kwa udongo
Umesema kweli.

Maisha ya mwanadamu ya siri kubwa sana ndani yake.
Tuishi kwa kuto kujikweza.
 
Daima tutamkumbuka Mzee ruksa.
 
Huyu mzee alikua safi sana, mtu flani mweupe pee hana baya, kila mtu afanye kwa nafasi yake atimize majukumu yake apumzike.

kuna kauli alitoa akasema maisha ni kama kitabu cha hadithi tujitahidi tuishi vizuri na watu ili tuwe hadithi nzuri kwa wengine, na ndivyo alivyokuwa,, apumzike kwa amani.
 
1. Kupenda Dini na Kusali sana.

2. Kupenda Utani na Ucheshi.

3. Kukitukuza Kiswahili na Kujivunia Kukiongea Kiufasaha...
R.I.P The Rt. Hon. Pres. Ali Hassan Mwinyi

kama kweli umeyarithi hayo yote kwa huyu Mzee,
basi sitegemei kuona onyo, vitisho wala angalizo kwenye bandiko zako zinazofata...πŸ’
 
Mengi ni ya kuhadithiwa, kipindi cha uongozi wake nilikua bado mtoto. Nimekua nakuambiwa alikua mzee wa ruksa. Aliruhusu vitu vingi kutoka nje ya nchi kuingia ndani tofauti na raisi wa awamu ya kwanza
 
Salaam,

Leo Februari 29, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi. Soma...
Mzee wetu Mwinyi azikwe kwenye ardhi ya chimbuko lake (Tanganyika yetu)
 
Ni kile kibao tu Alipigwa na yule Mwehu Diamond Jubilee.
Hela Enzi zake tulichezea hilo nampa πŸ‘Š.
Rip
 
Je, wewe utamkumbuka Mzee wetu huyu kwa mambo gani hasa?
Alisimama jukwaani akasema, "anayetaka kula chura na ale asiwepo mtu wa kumpangia ale nini na akiwa wapi"
Alisimama jukwaani akasema "gonjwa hili limeingia pahala pale ambapo sote wakubwa na wadogo twapapenda"
Alikuwa ndiye mlezi wa Baraza la huduma za jamii la kikristo CSSC
 
Reactions: Ame
Rais wa kwanza Kupigwa Kofi hadharani na raia.
Ndiyo hapo ujue kwenye mambo ya imani watu wengine wamepinda ubongo, yule kijana sijui alifikiria nini lakini ajabu Mzee Mwinyi hakuchukia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…