Je, utamkumbuka Hayati Ali Hassan Mwinyi kwa mambo gani?

Alitupa vibarua na wamakonde fulani kina mandanga cha kupanda ukoka kwenye nyumba yake msasani,na yeye pia alikuwa anapanda pamoja nasi...Mara zote anatupa maneno ya kihekima hasa baada ya kugundua miongoni mwetu wanapiga stori za vinywaji na mademu....aisee alitupa usia sana yaani bado sauti yake bado naisikia masikioni......
 
Ulikua wapi?
 
Huo ukarimu kaurithisha kwa vijana wake wote

kuna mmoja ni Daktari pale Muhimbili, akivyomkarimu unaweza ukadhan ni wale Madakatari wanafunzi, halikadhalika Hussein na wengine
 
Hah
Mimi nimeanza kushika pesa wakati wa Mwinyi na nikanunua TV na VHS wakati wa Mzee Ally Hassan Mwinyi.

Mungu amlaze huyu Mzee mahala pema peponi.
Hahahaa alikuwa shemeji yetu pale Azania HS. Alioa mtoto wa KK aliyekuwa anasoma Jangwani SS.
Alikuwa akipita tunatoka na kushangilia shemeeejiiii shemeeeejiii! Siku moja kidogo itutokee puani.
 
Sababu kubwa ni hii hapa 👇
 
Jirani uliondoka Mikocheni huku , tutakukumbuka sana kwa ukarimu wako
 
Hivi sakata la OIC ilikuwa wakati wa Mwinyi? sio wakati wa Dr. Salmin Amour na Mkapa miaka ya 95 Mwalimu akiwa hai? mbona unachanganya madawa?
 
Kila nafsi itaonja mauti huo ni ukweli ambao hatuwezi kuupinga. Kifo cha mzee Mwinyi binafsi kimenigusa hata kama hakikunishtua pengine kwa sababu alikuwa mgonjwa muda mrefu na pia umri ulishasonga sana.

Kwanini kifo cha mzee Mwinyi kimenigusa zaidi ya kifo cha wengine kama Magufuli nk ni kwamba licha ya mapungufu yake mzee Mwinyi alikuwa mtu muungwana sana!

Mzee Mwinyi alikuwa mtu wa watu, muungwana na mwenye kusamehe. Wakati wa mwalimu Nyerere Mwinyi akiwa waziri aliwahi kufukuzwa kwenye nyumba ya serikali Mikocheni na waziri mmoja ambaye Mwinyi hakumtaja katika kitabu chake. Pamoja na kwamba jambo hilo lilimpa fedheha kubwa lakini cha ajabu mzee Mwinyi baada ya kuwa rais bado alimwacha mtu yule kwenye baraza la mawaziri!

Maandiko yanatuambia wema hushinda uovu. Naamini kabisa kuwa mzee Mwinyi atakuwa amefariki katika hali ya moyo safi na kupata mastahili ya Mbingu.
 





Huyu Mwinyi alikuwa AKILI kubwa Sana
 
Ni
Mtazami wako tu mtoa hukumu ni Mungu acheni porojo
 
Moja kati ya maneno ya hekima sana kutoka kwa Raisi wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi

Maneno haya, yataendelea kudumu katika maisha yetu. Pumzika kwa amani mzee wetu

Your browser is not able to display this video.
 
Ndugu zangu, nafsi yangu imenisukuma kuandika jambo wakati huu tunapoomboleza msiba wa rais wetu mstaafu "Mzee Ruksa" kama ifuatavyo;-

Aliuza Loliondo kwa waarabu pamoja na kelele nyingi zilizopigwa.

Alileta ada kwa vyuo vyote vya serikali IFM, Mzumbe, UDSM, n.k wakati wa Mwalimu vyuo vyote ilikuwa hulipi chochote ni sifa tu za kujiunga zinakupeleka.

Alianzisha utaratibu wa kulipia matibabu katika hospitali za serikali, kabla ya hapo matibabu yalikuwa bure hadi Muhimbili. Maana yake ni kwamba serikali iligharamia.

Alianzisha utaratibu wa kulipia ada katika shule za sekondari za serikali, kabla ya hapo ilikuwa bure kabisa.

Alivunja miiko ya viongozi. Sasa, viongozi wakawa hawana miiko tena, hapa ndipo ufisadi wa viongozi ulipoanzia.

Alianzisha upendeleo wa waziwazi kwa watu wake hata kama wamefanya makosa kiasi gani aliwakingia kifua na kuwasamehe...mfano Ruban Aziz aliyefungwa kwa kutorosha madini alimsamehe kwa madai "eti" mama Aziz alienda Ikulu kumlilia.

Yeye ndiye muasisi wa viongozi kuanza kujimilikisha mali za umma.

Yeye ndiye alianza kuuza viwanda vya umma kwa matajiri.

Yeye ndiye alisitisha ajira za moja kwa moja toka vyuoni, baada ya kukosa ubunifu wa kupanua wigo wa ajira kwa kuanza kuua viwanda, mashirika n.k vya umma.

Ndiye alianza kuogopa midahalo katika vyuo vikuu...alisisitiza vyuoni kumefuatwa vyeti tu siyo siasa. Hapo ndipo tatizo lilipoanzia anguko la wasomi wa nchi hii kuwa na vyeti vizuri lkn hawana "akili" kabisa.

Heshima ya taifa ilianza kushuka sana, majirani hata mataifa ya nje yaliyokuwa yanatuheshimu yalianza kutudharau kwakuwa kiongozi wetu hakuwa makini sana kwenye mambo ya msingi, mfano alitoa amri ikawa sheria sikukuu yoyote ikiangukia jumamosi au jumapili ilikuwa inalipiziwa kwa watu kupumzika siku za kazi juma linalofuata, ulikuwa ujinga fulani hivi na ulitushushia hadhi sana kama taifa kwa wenzetu.

Alianzisha utaratibu wa kusafiri na "kijiji" akienda nje ya nchi. Lengo lilikuwa kwenda kula maisha na marafiki zake. Safari ya mwisho ilikuwa ya Copenhagen...vyombo (hasa magazeti) yaliandika na kulalamika sana kuhusu hili.

Aliondoa udhibiti kisheria wa bei za bidhaa mbalimbali. Bidhaa zilikuwepo lkn mfumuko wa bei ukawa juu, wafanyabiashara wakaneemeka sana wananchi wa kawaida wakazidi kuwa masikini.

Aliongeza pengo kati ya tajiri na masikini, nchi ilianza kuwa ya matabaka ya matajiri na masikini wakati wake. Kabla yake ilikuwa kawaida mtoto wa mkulima wa jembe la mkono na mtoto wa rais, waziri n.k kusoma shule moja, lkn alipokuja "akawatenga" nchi hii sasa hawa watu wanakutana wakati wa uchaguzi tu hohehahe wanapo ombwa kura.

****

Ninapenda nimalizie hivi ndugu zangu.

Nimeamua nimkumbuke mzee wetu kwa baadhi ya mambo hayo ambayo naamini ni muhimu kizazi ambacho hakikuwepo wakati wa utawala wake kikayafahamu au hata waliokuwepo wanaweza kuwa wamesahau.

Lengo la hayo hapo juu siyo kubeza, kuchafua, ama nia yeyote mbaya, la si hivyo. Lengo ni kwetu tuliobaki, kila tutendalo kwa watu liwe jema ktk macho yao au baya litakumbukwa siku tutakapo "fumba macho".
 
Inasikitisha sana
 
Wanasema "Tishukuru Mungu Mwalimu alikuwepo coz alizuia Mengi sana" ila asingekuwepo Tz ingekoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…