JPM ndiye chanzo (source) cha kila baya linaloendelea hapa nchini hivi sasa....tozo, mikopo, vitu kupanda bei, kuparaganyika kwa demokrasia, umeme kukatika hovyo, n.k.
TOZO
Mama kakuta nchi inaendeshwa kwa kupora fedha za wafanyabiashara. Ulitaka mama afanyeje sasa? Aendeleze uporaji? Ndiyo maana kaanzisha tozo. JPM alaumiwe na alaniwe.
MIKOPO
Mama analazimika kukopa sana ili aweze kulipa riba kubwa za mikopo ya biashara ambayo JPM aliichukuwa.
KUPARAGANYIKA KWA DEMOKRASIA
JPM ndiye muasisi wa uporaji wa haki za watu ktk chaguzi. Aliharibu uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na akaharibu pia uchaguzi mkuu wa 2020 na wala hakushinda.
Pia ALIZIMA INTERNET kipindi cha uchaguzi mkuu. Jambo hili ni la kihuni na kidikteta na hatukuwahi kuwa na ujinga huu huko nyuma.
Kwa haya na mengine mengi KAMWE SIWEZI KUMSAMEHE JPM.
"He must be punished multiple times where he is now"