Huwa namuwaza Sana Raisi wangu mpendwa JPM!
MUNGU amlaze mahali pema
Alipokuwa mtoto bwana Yule wa Yerusalemu alinusurika kuuwawa!
Hayo yalimfika JPM, ingawa yeye si wakati angali mtoto!
Bwana yule wa Yerusalemu aliishi maisha ya watu wanyonge, ooh ni sawasawa na ndugu yetu JPM
Alipoanza kazi bwana yule wa Yerusalemu alikemea uonevu kwa wanyonge, na tabaka la Wala Nchi halikumpenda,,
Alichukiwa pia na serikali ya kibeberu ya Rumi.!!
Raia weengi wa Taifa lile, hususani wanyonge walimpenda
Duuh yaani vivyo hivyo kwa Magufuli.
Bwana wa Yerusalemu alizunguka kila mkoa wa Israel kufundisha na kutatua matatizo mengi ya wenye shida.
Hii ndio kazi aliyoamini comrade Magufuli!
Alipambana na wafanya biashara haramu hekaluni na akaharibu biashara zao, walimchukia kwa tendo Hilo, hivyo walikuwa miongoni mwa walioshangilia kifo chake baadae!
Sote tunakumbuka wafanyabiashara haramu walivyofunga biashara zao huku wanamtukana JPM, na baadae kusherehekea kifo Cha Magufuli.
Bwana yule aliuwawa kule Yerusalemu,
Bado Raia wanajiuliza Hadi Leo the real cause of death of JPM the hero!
Baada ya kifo chake Bwana wa Yerusalemu, wafuasi wake waliishi kwa mahangaiko na wengi wao waliuwawa na serikali ya kibeberu ya Rumi ktk kuhakikisha Legacy ya bwana yule haidumu!!
Leo kauli mbiu ni chama kimerudi kwa wenyewe, Vita ya wahuni na viroboto!
Hakika ukweli utabaki kuwa wahuni wanashinda!!
Nenda JPM, raia wengi walikupenda!
Watakukumbuka daima