Mungu ampumzishe kwa amani Rais wetu mpendwa ambae bado alikuwa na kiu yakuwafanyia makubwa wa Tanzania. Kwa muda mchache sana amefanya mambo makubwa yafuatayo ambayo yatakuwa na manufaa kwa miaka mingine mingi.
1. Kurudisha discipline Serikalini
2. Kukarabati shule kongwe
3. Kutoa elimu bure
4. Matibabu bure
5. Miundo mbinu y umeme, maji, barabara, reli, meli, ndege, vivuko
6. Usalama wa Raia - Ujambazi umepungua sana
7. Kaondoa ubadhirifu Serikalini
8. Kapambana na rushwa
9. Amedhibiti mapato ya Serikali
10. Wafanyakazi hewa
Inakuhitaji kuwa mwehu wa kiwango cha juu sana kama utakuwa hujayaona haya, pamoja na hayo kuna vilio vifuatavyo katika Serikali yake ila sina uhakika kama tafiti zimefanyika za kutosha.
1. Kwamba amekandamiza demokrasia
2. Ameuwa sekta binfsi kwa maana ya kwamba kila kitu kinafanywa na Serikali yenyewe
3. Kwamba mazingira ya uwekezaji hayakuwa rafiki kuvutia FDI's
Nawakilisha