Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Ukiondoa tofauti ya kiitikadi na kivyama ila huyu mtu kaniliza aisee.

Jamani kaniuma sana pamoja na mapungufu yake ila daaah tukubali pia tumempoteza mtu ambaye kuna mitazamo yake tutaimiss tu.

Magu alikua na kitu cha kipekee na aina yake despite mapungufu yake.

Kila mtu ana mchango wake ktk life. Nenda baba najua pengi uliteleza lakini pengi uliwezea.

Daaah issue za korona,mradi wa nyerere dam,na msimamo kuhusu madini nitakukumbuka daima
Pia uzuri wa jamaa alikua ni nationalist yaani anasimamia anachoamini sio mtu wa kuuza nchi kwa vipande vya fedha au kusaini mikataba feki.

Sawa tu ngoja niliee[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Magufulu Baba umeniliza sana. Mimi ni CDM, pamoja na yote uliyowafanyia viogozi wetu lakn tumekusamehe. Daima tutakuombea kwa Mungu upate pumziko jema.. Nenda Baba..
 
Huyu mwamba mm nilikua nampenda maana alikua hapendi unafiki ukizngua anazingua tena mbele ya watu haina sijui kuitana chemba yy anakumaliza hapo hapo.Sijui km Mh Suluhu ataweza hivi viatu.
Ataweza nae atakuwa na staili yakw,Mungu katuumba na talanta tofauti roho ni yuleyule anaetuongoza,binadamu huwezi kuwaridhisha watu wote,nae atafanya kwa kiwango chake,atasimamia sheria na katiba mengine yatajipa yenyewe!
 
Upumzike kwa amani JIWE.

Kiukweli,John alitisha na hakubabishwa na iwe mzungu,mwarabu na hata na yeyote.

Jamaa nguvu aliyopata kuwa nayo hakika haimithiriki!

Ni kiongozi aliyetamka kwa kumaanisha na alisikilizwa.

Ni kiongozi aliyesema vile na ikawa.

Sielewi ni kwa namna gani ninaweza kumuelezea mwamba yule zaidi tu itoshe kusema JPM ALIKUWA NI ZAIDI YA SIMBA!

Huenda huko mbele ya safari mwamba hatokuwa na tofauti ya kumbukizi na kina Nyerere.
 
Ufunuo 3:15-16

Nayajua mambo yako yote! Najua kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali ungekuwa kimojawapo: Baridi au moto. Basi, kwa kuwa hali yako ni vuguvugu, si baridi wala si moto, nitakutapika!
 
Mungu ampumzishe kwa amani Rais wetu mpendwa ambae bado alikuwa na kiu yakuwafanyia makubwa wa Tanzania. Kwa muda mchache sana amefanya mambo makubwa yafuatayo ambayo yatakuwa na manufaa kwa miaka mingine mingi.

1. Kurudisha discipline Serikalini
2. Kukarabati shule kongwe
3. Kutoa elimu bure
4. Matibabu bure
5. Miundo mbinu y umeme, maji, barabara, reli, meli, ndege, vivuko
6. Usalama wa Raia - Ujambazi umepungua sana
7. Kaondoa ubadhirifu Serikalini
8. Kapambana na rushwa
9. Amedhibiti mapato ya Serikali
10. Wafanyakazi hewa

Inakuhitaji kuwa mwehu wa kiwango cha juu sana kama utakuwa hujayaona haya, pamoja na hayo kuna vilio vifuatavyo katika Serikali yake ila sina uhakika kama tafiti zimefanyika za kutosha.

1. Kwamba amekandamiza demokrasia
2. Ameuwa sekta binfsi kwa maana ya kwamba kila kitu kinafanywa na Serikali yenyewe
3. Kwamba mazingira ya uwekezaji hayakuwa rafiki kuvutia FDI's

Nawakilisha
 
Alianza vizuri Sana alikosea alipowafanya wale majirani wabaya waliokacha kumuaga maswaiba zake wakampotosha.Japo alianza rejea kwenye mstari ila ndo hivyo tena
 
Ana yote mazuri na mabaya pia.Sisi tutamuenzi kwa mazuri yake.
 
1.Chato International Airport
2.Chato National Park
3.Trafic light Chato
4.3 star hotel Chato (TANAPA)
5.Bohari ya kanda madawa Chato
6.Hospital ya rufaa Chato
7.Stadium (proposa)
8.CRDB Chato
hapa ulisahau na chuo cha veta,hospitali ya rufaa kubwa na nzuri kabisaa,jamaa aliwajari sana kwao,aliogopa nyie nyie mliowatukana marais wengine kuwa waliterekeza kwao msije mkamtukana pia akimaliza uongozi wake
 
Magufuli aka bulldozer
Amekimbiza wazembe wengi katika miradi kote Tanzania na hata Waziri wake wa maji Ni kiboko ya ufisadi awesso Ni chuma kama alivyo Magufuli.Ninaamini anaweza kutembeza miradi yote na kuijenga Kama alivyotakiwa ashike.maisha ya Magufuli yametupa michongo mingi ya kushine Magufuli Ni top kila sehemu.wewe kaa chini fikiri Ni wapi Magufuli hakupenyeza fikra zake.kote ame cover na watu wamebadilika jamii imepata faida na nguvu za kutosha Sasa tutegemee kula matunda yetu.tujiamini tumakinike kwenye kazi ili tuiletee nchi ubingwa.sawasawa Tuacheni kinyongo peace kwa wote ambao Wana jua mapigo ya Magufuli sio laana ilikuwa Ni baraka.hakuna ufisadi kwa Sasa tuna viongozi wazalendo tumewapata hawajifichi wakina rais samia, polepole, bashiru,n.k
images.jpg
 
Haya twende haraka haraka

Katika utawala wake watumishi wa umma hawakuoandishiwa mishahara. Ukizingatia gharama za maisha zilipanda,watumishi waliendelea kuwa maskini.

Katika utawala wake upandaji wa madaraja ulikuwa mgumu sana. Kuna kipindi wanasema walisitisha kupisha vyeti feki.

Katika utawala wake motisha kwa watumishi walipigwa chini kwa vyeti feki bila kupewa chochote licha ya kutumikia nchi.

Watumishi wamkumbe kwa lipi John Pombe? Ni mtazamo tu,usijenge chuki.
 
Back
Top Bottom