Tusubirini. Makamanda mnataka IGP, Paroko, Mufti, Refa, na Kapteni wa Yanga wote wachaguliwe na Mangi kwa ukabila, wamesahau kabisa hapo zamani Waziri Mkuu alitoka kwao mara 4, akiwamo Naibu Waziri Mkuu, na Waziri wa Fedha mara 4, watendaji wote Taasisi nyeti za Kitaifa walitoka kwa makamanda, sasa hamtaki wengine wawe na Waziri Mkuu au hata Meneja wa TAZARA, nao wajenge kwao? Huo ukabila utawatafuna, Nyerere aliufuta kwa kutumia JKT, shule za Boarding, Kanisa na TANU, nyie mnataka kurudisha Ukabila tena? Unamkumbuka Jenerali Muhidin Kimario, Shujaa wa Nchi hii, alikuwa Katibu wa CCM Kusini Pemba akaitwa vitani kuigomboa Nji yake dhidi ya nduli Idi Amin aliyejitia anatetea Uislamu, yaani mnataka General Kimario awe Mangi wa Uswaa tu asitutumikie Watanzania wengine? Kama mkianza tena jiwe litarudi au yatatokea mawe zaidi, hamtoyaweza good night.