Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Mitanzania unaiacha tu ife ipate taabu kwa sababu haijitambui. Nina uhakika leo Rais Samia akiamua akaze yataanza ohh dikiteta mara ohh maisha magumu. Komeni sana na bado

Wewe sio mtanzania. Huwezi kuongea hivyo. Nchi ni ya watanzania sio kiongozi, lazima uwasikilize wanataka Nini, sio kujiamulia Kama unakomoa watu.
 
Sheria ni sheria hata kama ni ngumu.
Je, wakazi hao walijenga kwenye eneo ambalo ni la barabara? Au barabara iliwafata wao?
Sheria lazima ifuatwe, na ndicho alichosimamia JPM.
JPM hakuwa na roho ya kumuumiza mtu mnyonge!!
Mafisadi na majangili waliyaumiza sababu kwanza yaliiumiza nchi hii, lakini pia, yalitumia nguvu kubwa kutaka kumfanya ashindwe uchaguzi.

Hata kama ni mimi, ningewashughulikia tu.

Unaongea kwa kujifurahisha. JPM alikuwa na Roho mbaya Sana. Mpaka leo saanane na Azory hawajulikani walipo. Yule Bora aliondoka alikuwa anakinai tu.
 
JPM was exceptional president, charismatic leader

Charismatic unaiba kura? Charismatic unaambulia asilimia 57 ya kura 2015 hata pamoja na wizi?. Linganisha charismatic ya Kikwete 2005 na Magufuli 2015 uniambie.

Exceptional ni Nyerere na Maalim Seif tu, huyo ibilisi kiongozi wa wasiojulikana tupa huko jalalani.
 
Babu Seya suala lake liko wazi linajulikana.

JPM hakua mjinga, hakua na faida yoyote ya kumuachia Papii na Babu Seya.

Ukweli nikwamba, wanapenda wote Hela, sio kwamba wanamakosa.


JK ndo alimpeleka Papii Jela . Ilo liko wazi na libaki kua hivohivo tu.

JPM alikuwa ana ego ya kutaka apendwe na kila mtu. Hata kumtoa baby seya ilikuwa kutengeneza base yake.
 
Magufuli hakuwahi kuunga mkono masuala hayo .

Na Kwa MANTIKI hiyohiyo aliamua kumpa Makonda Go ahead ya kupambana nao.


Babu S na Papii, walitiwa gerezen Kwa Stori za kutengeneza na kuzipachika kwenye magazeti Kila siku. .


Na ndio maana JPM aliwaachia, Mkapa akiwa hai.

Kitendo Cha Magufuli kuwaachia wafiraji ilikuwa ni kuunga mkono ushoga.
 
Aiseeee muacheni apumzike,mnavyozidi kuleta thread zenu ndivyo anavyozidi kupopolewa.

Kiranga anakwambia kwa watu walioona utawala wa magufuli hauwezi kuwaambia hivyo wakakubali labda usubiri vizazi vya mbele huko ambavyo vitakuwa havijauona utawala wake ndiyo uwadanganye.
Mkuu,

Mimi ndiye niliambiwa hivyo, mimi sikusema hivyo.

Kuna watu kweli huwezi kuwaambia kitu, jinsi wanavyompenda Magufuli.

Sababu ni ujinga wa kawaida tu wa Watanzania wengi.
 
JPM atabaki kuwa Rais bora kuwahi kutokea Tanzania.

Anakumbukwa na atakumbukwa daima.

Atakumbukwa kwa lipi? Halafu hiyo ya Rais Bora kutokea mnaiongea kinafiki. Akina Nyerere wasemeje?. Tatizo mnaangalia mambo mwisho wa pua zenu.
 
Tusubirini. Makamanda mnataka IGP, Paroko, Mufti, Refa, na Kapteni wa Yanga wote wachaguliwe na Mangi kwa ukabila, wamesahau kabisa hapo zamani Waziri Mkuu alitoka kwao mara 4, akiwamo Naibu Waziri Mkuu, na Waziri wa Fedha mara 4, watendaji wote Taasisi nyeti za Kitaifa walitoka kwa makamanda, sasa hamtaki wengine wawe na Waziri Mkuu au hata Meneja wa TAZARA, nao wajenge kwao? Huo ukabila utawatafuna, Nyerere aliufuta kwa kutumia JKT, shule za Boarding, Kanisa na TANU, nyie mnataka kurudisha Ukabila tena? Unamkumbuka Jenerali Muhidin Kimario, Shujaa wa Nchi hii, alikuwa Katibu wa CCM Kusini Pemba akaitwa vitani kuigomboa Nji yake dhidi ya nduli Idi Amin aliyejitia anatetea Uislamu, yaani mnataka General Kimario awe Mangi wa Uswaa tu asitutumikie Watanzania wengine? Kama mkianza tena jiwe litarudi au yatatokea mawe zaidi, hamtoyaweza good night.
Sukuma gang tupa kureeeeeeeee na hampati tena hiyo nafasi mpaka dunia itakapo geuka
 
Alipinga ushoga kwa kumzuia Makonda aka bashite asipambane nao, pia alitatuta matatizo ya wananchi kwa kuwauwa, kuwateka, kuwapiga risasi, kuanzisha genge la wasiojulikana, kufungulia kesi watu za uhujumu uchumi na kupora uchaguzi
Wacha uongo we gaidi.
Genge la Wasiojulikana halipo, genge unalo dai halijulikani linajulikana na muasisi wake ni Jakaya Mrisho Kikwete na alianzisha hao ki sheria na wapo karibu nchi zote Duniani, hivyo basi Umedanganya.
Watu waliofunguliwa kesi ni wahujumu Uchumi na wamekiri hayo kwa maandishi na rekodi zao zipo mahakamani. Ni wezi. Ni mufilisi. Ni mafisadi. Usihadae.

Uchaguzi umeporwa kivipi? Wanaodai uliporwa washachukuwa ruzuku, ikiwaina maana wamekubali, wameridhiana kuwa hakuna kura iliyoporwa. Waulize wakuu wako kuhusu saini walizopiga kukubali ruzuku....hakuna kitu kinafanyika bila makubaliano. Wacha Uwongo na Ugaidi.
 
Sheria ni sheria hata kama ni ngumu.
Je, wakazi hao walijenga kwenye eneo ambalo ni la barabara? Au barabara iliwafata wao?
Sheria lazima ifuatwe, na ndicho alichosimamia JPM.
JPM hakuwa na roho ya kumuumiza mtu mnyonge!!
Mafisadi na majangili waliyaumiza sababu kwanza yaliiumiza nchi hii, lakini pia, yalitumia nguvu kubwa kutaka kumfanya ashindwe uchaguzi.

Hata kama ni mimi, ningewashughulikia tu.
Walinyooka kweli kweli!
 
Jioneeni wenyewe Wakuu!

Hakuwahi kutokea mtu kama huyu, aisee JPM aligusa Maisha ya mnyonge yule wa chini Moja Kwa Moja kabisa.

Naomba Mungu anipe Angalau robo ya Roho ya JPM.

Huyu Mtu hapana, Eeehh, Kwakweli Mungu aliamua kuruhusu apumzike baada ya kazi kubwa aloifanya!
View attachment 2561435
Wakati huo bei za mazao zilikuwaje pamba hadi sh. 500 kwa kilo kutoka walizoahidiwa wakulima wanyonge 1,560 lakini sasa bei hadi Sh. 2,200 kwani kuna mnyonge zaidi ya sisi wakulima.
 
Zamani Jf ilikuwa ya great thinkers ila sasa imejaa wapumbavu wengi sana
 
Back
Top Bottom