Ni miaka 3 imefika toka hayati Magufuli kuiacha Tanzania katika majonzi yasiyotarajiwa hivyo kama Mtanzania bado namuombea kwa Mungu aweze kuishi salama kwenye maisha ya mbinguni,kwa uhakika Rais Magufuli ni Rais ambaye alikuwa ni mwenye maono ya kuifanya nchi kutoka kwenye ombwe la omba omba na umasikini kutuvukisha katika nchi ya ahadi kutokana na sababu zifatazo
KUIMARISHA PATO LA MWANANCHI
Aliweza kuifungua nchi hasa kwenye upande wa biashara na watu wengi walifanya ujasiriamali ambao ni msingi kwenye kukuza pato la mtu mmoja mmoja(individual income).
ITIKADI NA UCHUMI IMARA
Nimemuona Rais Samia Suluhu akifata nyazo za kikwete kuamini sana kwenye uchumi wa kibepari ambao,sio uchumi imara kwa nchi za kiafrika kitendo cha serikali kutoa kibali cha uwekezaji kwenye miradi mikubwa mfano bandari na mengine ni jambo ambalo linaweza kuwa linahatari sana,hasa kwa uchumi wa nchi kuna kuwa monopolism kwenye biashara pia kuna mambo mengi ya rushwa hufanyika wakati na baada ya kutafutwa investor ila ikiwa serikali itakuwa ni controller tunaweza kumaintain market na uchumi wetu ukawa imara,hivyo uchumi wa kibepari ni pasua kichwa.
MASHIRIKA NA TAASISI ZA SERIKALI KUJUA WAJIBU WAO KWA SERIKALI
Unaweza kushangaa inakuwaje vipindi vilivyopita nyingi za taasisi zilikuwa haziwajibiki kwenye marejesho ya faida kwa serikali na kila siku zilitangazwa hati chafu kwa baadhi ya mashirika ambapo ilipelekea mashirika mengi kufanya ufisadi kwa kuwa hakukuwa na wakuwauliza lakini kipindi cha magufuli ilikuwa ni tofauti kwababu itikadi ya kijamaa ilifanya mifuko kuwa mkusanyaji mkubwa wa mapato ya kiserekali hivyo hata huduma nazo zilikuwa bora.
My Take
Nimemkumbuka Rais wa awamu ya tano sababu ya kumuona makonda kwenye majukwaa ni zao pekee la magufuli lenye kustawi katika miba ila siyo vibaya Rais Samia Suluhu kufata nyendo za mtangulizi wake.