Je, utamkumbuka Hayati Magufuli kwa mambo gani?
Mtu mwenye uthubutu wa Hali ya juu. Hata kama pesa ya mradi ni kubwa na haipo atasema "pesa ipo mkandarasi maliza kazi"
 
Nidhamu kwenye taasisi za serikali...now .mama Samia ameturushisha nyuma sana aisee
 
Ni miaka 3 imefika toka hayati Magufuli kuiacha Tanzania katika majonzi yasiyotarajiwa hivyo kama Mtanzania bado namuombea kwa Mungu aweze kuishi salama kwenye maisha ya mbinguni,kwa uhakika Rais Magufuli ni Rais ambaye alikuwa ni mwenye maono ya kuifanya nchi kutoka kwenye ombwe la omba omba na umasikini kutuvukisha katika nchi ya ahadi kutokana na sababu zifatazo

KUIMARISHA PATO LA MWANANCHI

Aliweza kuifungua nchi hasa kwenye upande wa biashara na watu wengi walifanya ujasiriamali ambao ni msingi kwenye kukuza pato la mtu mmoja mmoja(individual income).

ITIKADI NA UCHUMI IMARA

Nimemuona Rais Samia Suluhu akifata nyazo za kikwete kuamini sana kwenye uchumi wa kibepari ambao,sio uchumi imara kwa nchi za kiafrika kitendo cha serikali kutoa kibali cha uwekezaji kwenye miradi mikubwa mfano bandari na mengine ni jambo ambalo linaweza kuwa linahatari sana,hasa kwa uchumi wa nchi kuna kuwa monopolism kwenye biashara pia kuna mambo mengi ya rushwa hufanyika wakati na baada ya kutafutwa investor ila ikiwa serikali itakuwa ni controller tunaweza kumaintain market na uchumi wetu ukawa imara,hivyo uchumi wa kibepari ni pasua kichwa.

MASHIRIKA NA TAASISI ZA SERIKALI KUJUA WAJIBU WAO KWA SERIKALI

Unaweza kushangaa inakuwaje vipindi vilivyopita nyingi za taasisi zilikuwa haziwajibiki kwenye marejesho ya faida kwa serikali na kila siku zilitangazwa hati chafu kwa baadhi ya mashirika ambapo ilipelekea mashirika mengi kufanya ufisadi kwa kuwa hakukuwa na wakuwauliza lakini kipindi cha magufuli ilikuwa ni tofauti kwababu itikadi ya kijamaa ilifanya mifuko kuwa mkusanyaji mkubwa wa mapato ya kiserekali hivyo hata huduma nazo zilikuwa bora.

My Take

Nimemkumbuka Rais wa awamu ya tano sababu ya kumuona makonda kwenye majukwaa ni zao pekee la magufuli lenye kustawi katika miba ila siyo vibaya Rais Samia Suluhu kufata nyendo za mtangulizi wake.
 
Mfumuko wa bei ni wa kutisha kiasi kwamba ukimuona mtu anajenga sasa ujue yuko kwenye mrija wa ufisadi au ni kampuni fulani.

Sukari hakuna

Maji hakuna

Umeme hakuna

Bwawa la mtera halina maji licha ya kwamba mvua zimenyesha za kutosha na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.

Michango shuleni ni balaa na hakuna wa kukemea.

Maandamano ya chadema yamerudi kwa kasi na kilio kikubwa kwao ni kupanda kwa gharama za maisha! Sasa walishangilia ili iweje?
 
Hahaha,ni Majuto kwa kweli.Bora tuliolia maana machozi yetu yalikuwa ni halali.
 
Kwani waliokuwa wanaongoza serikali wameondoka?Unacheza kombolela ukiwa peke yako?Serikali isiyokuwa na mifumo thabiti kujiendesha hugeuka kituko mara zote.Mtu mmoja hawezi kutatua matatizo yote kwa pamoja.Ni kujidanganya in a broad daylight.
 
Mfumuko wa bei ni wa kutisha kiasi kwamba ukimuona mtu anajenga sasa ujue yuko kwenye mrija wa ufisadi au ni kampuni fulani.

Sukari hakuna

Maji hakuna

Umeme hakuna

Bwawa la mtera halina maji licha ya kwamba mvua zimenyesha za kutosha na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.

Michango shuleni ni balaa na hakuna wa kukemea.

Maandamano ya chadema yamerudi kwa kasi na kilio kikubwa kwao ni kupanda kwa gharama za maisha! Sasa walishangilia ili iweje?

Hawawezi wakakwambia mana imekuwa aibu kwao na kuusema ukweli sasa kwao ni kama kujipiga na ncha ya upanga shingoni. Acha mwamba alale hajaacha Deni kwa Watanganyika
 
Back
Top Bottom